Jana nilianza kuzungumzia ni kwa jinsi gani akili yako inaweza kujibu maswali magumu yote ambayo unayo au yanakusumbuka.
Ili kupata majibu au mafanikio ya jambo lolote ni lazima uumize kichwa kwa maana nyingine lazima ufikirie utatokaje, au utafanikiwa kivipi.
Watu wengi sana ni wavivu wa kufikiri na niwasemaji sana huku wanaofikiri ni wachache ni watu wakutenda.
Kama umefikiria sana lakini bado hujapata jibu la swali au changamoto inayokusumbua basi pumzika kufikiri kwa nguvu na akili nyingi. Relax.
Namaani s a ukiona umeshindwa kuendelea kuwaza au kupata majibu achana nayo, kalale, pumzika kisha endelea kujiuliza kwa nini # MIMI NI MASKINI, #KWA NINI MIMI SIJASOMA, #KWA NINI NIMESOMA LAKINI SINA AJIRA WALA #SIJAAJIRIWA, #KWA NINI NAKULA #MLO MMOJA#KWA NINI NAACHWA KILA SIKU#
Endelea kujiuliza kuhusu magumu na mapito yote ambayo unayoyapitia. Kisha jiulize swali au maswali hayo magumu kwa wepesi kwa mfano:
Hivi hakuna watu wanaokula milo mitatu tena milo inayostahili kwa maana ya kujenga mwili-WAPO. Hivi hakuna maskini aliyezaliwa hana kitu lakini leo anatamba au ana miliki pesa kibao-YUPO. Hivi hakuna mtu ambaye hakusoma kama wasomi wengine lakini leo ni tajiri na anaheshimika-YUPO/WAPO.
Hivi hakuna mwanamke ambaye alitelekezwa na mzazi mwenzake na leo anasongesha maisha yake mwenyewe bila huyo mwenza tena wakati mwingine maisha yake ni bora kuliko alivyokuwa na mwenza wake-YUPO.
Hivi hakuna mtu ambaye alikuwa na pesa lakini akafilisika ila hakukataa tamaa na leo hii amefanikiwa tena. Jibu-/YUPO.
Hivi hakuna binti ambaye amekuwa akihitaji kuolewa kwa muda mrefu lakini alipomlilia Mungu akamkutanisha na mume mwema-YUPO.
Hivi hakuna MJANE /MGANE ambaye aliumizwa na kifo cha mwenza wake lakini mwisho wa siku akakubali ukweli na leo hii anasomesha watoto wake yeye mwenyewe-YUPO TENA JIRANI YAKO. Sasa kama wao wameweza kwa nini wewe ushindwe. Jiulize hapo utakuwa ba shida kubwa sana.
Sasa wewe endelea kusubiri miujiza bila kujishughulisha utaona miujiza ya kufa maskini.
#ACHAWOGATHUBUTU#MIMINAUHUSIANO#
Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com