Friday, February 9, 2018
Thursday, September 21, 2017
Hongera Kwa Kazi Kaka Gabriel,,naomba Nikupongeze Kwa Kazi Nzuri Unayoifanya M&U Hasa Machapisho Kwa Waliokata Tamaa Kabisa Ya Maisha,,binafsi Nilikata Tamaa Baada Ya Kupitia Mikasa Ya Majaribu Magumu Sana,,naamini Mungu Anakutumia Haswa Kuganga Mioyo Ya Watu,,ombi Langu Nisaidie Niyapate Niwe Nayapitia Mara Kwa Mara,,kiukweli Natamani Sana Nitimize Ndoto Zangu,,ila Nimeumizwa Sana Moyo.Asante.
Wednesday, September 20, 2017
Mwanamke mzuri, tabasamu murua, meno mazuri, meupe yaliyopangwa yakapangika.
Kwa nini ukate tamaa kumalizia safari yako kwa sababu uliyekuwa naye safarini kashindwa kuimaliza safari yenu. Ahadi ni kufika mwisho kama yeye kashindwa Pambana na hali yako.
Maisha yapo, komaa unaweza kuishi na kufanya mambo yako bila huyo uliyedhani ndiyo KILA KITU, NDIYO MAISHA YAKO, NDIYO UHAI WAKO, NDIYO KODI YAKO, NDIYO FURAHA YAKO, NDIYO NDOTO YAKO, NDIYO AMANI YA MOYO. Kama imefika mwisho basi imefika tu hata kaka utalia na kusaga meno.
Kwa maoni na ushauri wa Uhusiano jiunge na Mi&u WhatsApp:0679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano
Monday, September 18, 2017
Mume mwema mwenye mapenzi ya dhati ndiyo hasa anayenifanya nifurahi na kutabasamu maishani mwangu.
Kwa ushauri jiunge na Mi&u WhatsApp:0679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano
Kweli dunia ni tambara mbovu, siku hii nakimbuka vifo vya wazazi wangu ambao walifariki siku kama hii.
Mungu nisimamie katika maisha yangu, kwani changamoto ni nyingi sana pekee yangu sitaweza.
Kwa ushauri jiunge na Mi&u WhatsApp:0679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano
Saturday, September 16, 2017
Thursday, September 14, 2017
Thursday, September 7, 2017
#Miminauhusiano#
Wednesday, July 12, 2017
Mi&u@mimi_na_uhusiano
Tuesday, February 21, 2017
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
Monday, February 20, 2017
Na GABRIEL NG`OSHA| IJUMAA WIKIENDA| XXLOVE
NI siku nyingine tunakutana katika safu yetu hii nzuri ya kuelimishana juu ya mambo mbalimbali yahusuyo maisha ya mapenzi. Nikushukuru msomaji wangu ambaye umekuwa ukinitumia SMS au kunipigia na kutoa maoni na ushauri wako juu ya mada mbalimbali ninazokuwekea hapa.
Pole sana, kwako wewe ambaye uliambulia manundu, matusi au kudhalilika kwa namna yoyote ile kwa sababu tu uliiparamia vibaya Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day).
Kwa kulewa na kufanya kila aina ya anasa jambo ambalo si maana halisi ya siku hiyo. Naomba nielekee moja kwa moja kwenye mada yetu ya leo; huna uwezo wa kumuumba umtakaye, acha uumbiwe.
Nikuhakikishie tu msomaji wangu kwamba makala ambazo ninaendelea kukuletea hapa kama kweli utazisoma na kuzielewa vizuri kisha kuzifanyia kazi, basi kila siku utakuwa mpya kwenye suala zima la uhusiano wako wa kimapenzi.
Akili za binadamu wakati mwingine hushangaza sana, kwani mtu anapohitaji mke au mume basi kwa harakaharaka uifanyisha kazi akili yake ya kuhakikisha inamtengenezea au kuumuumbia mwanaume au mwanamke mzuri ambaye anamtaka katika maisha yake bila kujua kuwa hiyo siyo kazi yake yeye kama mwanadamu bali ni kazi ya Mwenyezi Mungu ambaye kimsingi anakuwa amekwishamuumbia mwenza wake.
Maisha ya mwanadamu ni kama kitabu ambacho kimeshaandikwa, kinachofanyika ni kufunua ukurasa wa kwanza na kusoma.
Huna sababu ya kuanza kumuumba mtu unayemuhitaji kuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi wakati umeshaumbiwa, kilichopo ni kusubiri muda na mahali ambapo Mungu atakukutanisha naye. Usiteseke sana kwani hata kama utateseka kwa akili ya kibinadamu ni ngumu ila teseka kwa autaweza kubaini ni mwanamke au mwanaume yupi uliyeumbiwa na Mungu.
Watu wengi wamekuwa wakiwatengeneza wanawake au wanaume wanaowataka kuishi nao katika maisha ya ndoa, mtu anamtengeneza mwenza wake kuanzia muonekano (maumbile) na hata mambo mengine, jambo ambalo hakuna mwanadamu mwenye uwezo nalo. Kinachoshangaza ni mtu kumuumba mke wake awe ni yule mwenye hipsi kubwa au mwembamba au mwenye makalio makubwa.
Mwingine yeye anamuumba mwenza wake kuwa awe mwanaume mwenye fedha nyingi, elimu kubwa, awe siyo bahili ilimradi aweze kutumia holela fedha zake.
Kama ulikuwa hujui Mungu anayekuumbia siye unayemtaka bali anayekustahili katika maisha yako, mwanamke au mwanaume atakayekuwa nawe kwenye shida na raha, atakayekupenda wewe na ndugu zako, atakayekusikiliza na kukulinda na maadui.
Mwanaume au mwanamke mwenye hofu ya Mungu na mwenye kuheshimu ndoa na familia yake kwa jumla. Unaweza kujiumbia mwenza wako kwa kudhani mwenye umbo zuri, kiuno kipana, macho mazuri na mwendo matata ndiye anayekufaa kumbe si kweli. Mpenzi msomaji, usikose wiki ijayo kwenye mada nzuri zaidi.
Kwa maoni na ushauri tembelea ukurasa wetu wa Gazeti la Ijumaa Wikienda kwenye ukurasa wetu wa Facebook.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U







