Tuesday, January 5, 2016

Published 1/05/2016 12:08:00 PM by with 0 comment

CHOMBEZO: MTUMBUA MAJIPU WA KITAA



“Walimu leo ni siku ya Skuli Baraza, nina wanafunzi wawili nimepokea malalamiko yao na ninataka niwatumbue mbele ya wanafunzi wote na ninyi walimu  ili kukemea kabisa tabia zao chafu waliozianzisha hapa shuleni,” Mwalimu mkuu msaidizi, Dustan Mtanange wa Shule ya Msingi Kilima, wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga alikuwa akiwaeleza walimu wenzake ofisini.

Mara tu baada ya yeye kupata taarifa za msichana Maliamu kukutwa na barua yenye ujumbe wa mzito wa mapenzi ambao alidai ametumiwa mwanafunzi mwenzake wa kiume aliyejulikana kwa jina la Kangasu.
‘’ Nikiwa naenda zangu kunywa chai, mara nasikia sauti ya kitoto ikiniita ‘mwalimu, mwalimu’ ile nageuka hivi namuona mtoto ananikimbilia aliponikaribia akaniambia mama Maliamu anakuita, nilimweleza akamwambie nitapita nikiwa narudi. 

“Kweli nilipita na kumkuta mama yule kapandwa na jazba na kudaia sisi walimu hatutimizi majukumu yetu kwa kuwaangalia wanafunzi wawapo shuleni, kwani amekutana na barua chumbani kwa mwanaye ikiwa imewekwa kwenye bahasha nzuri ya maua na kwa juu imeandikwa kwa mwandiko mzuri sana maneno yanayosomeka ‘Kwako M,’ akimaanisha Kwako Maliamu.’ 

Na hata  alipoifungua  kuisoma alikutana na ujumbe mzito, mzuri mtamu sana wa kimapenzi uliomshangaza kwani ulionekana kuandikwa na mwanaume mwenye kumzidi umri Maliamu lakini pia ni mzoefu wa mambo hayo.
Kitendo cha kuisoma barua ile kilimuumiza sana mama yule na kuamua kumsubiri kwa hamu mwanaye atoke shule ili amuhoji.
Ilikuwa ni majira ya 10 jioni ambapo Maliamu alirudi kutoka shule na kuingia ndani kama kawaida hupenda kujitupa katika kitanda chake cha chuma chenye godoro la pamba lililotengenezwa na fundi mmoja maarufu sana wilayani hapo.

Ghafla alisikia mlango ukisukumwa kwa nguvu sana na kumfanya ashituke.
“Hivi Maliamu siku hizi umekuwa si ndiyo?” Mama yake aliuliza.
“Kwani mama, mimi nimefanyaje!?
Mama alimjibu “Hujui ulichokifanya, si ndiyo, haya niambie haraka sana hii barua imetoka kwa nani?” 
Mama aliuliza huku akiitoa barua ile aliyokuwa ameificha kwa nyumba kisha alimuonesha Maliamu. “Nataka uniambie haraka sana, nani kakutumia hii barua ya ujingaujinga, umeanza michezo ya ajabu si ndiyo.”
Maliamu aling’ata vidole vyake na kupindisha shingo upande wa kushoto, hamna mama sio ya…
Sio yako si mbona imeandikwa Kifupi cha jina lako ‘M’
Kweli mama sio yangu ni ya … kabla hajamaliza tena kujibu fyaaaa! Akapata kiboko cha begani, ile anajishika akachapwa kingine, ajakaa sawa akaanza kuchapwa viboko vingivingi.
“Hiiii hiii hiiiii! Mama unanionea barua hiyo kanipa Kangasu nimpelekee Mery sio yangu mama, mama sio yangu, kweli mama nakwambia sio yangu,” Maliamu alilia kwa uchungu sana.

Mama Maliamu baada ya kusikia maneo yale kidogo yaliingia akilini mwake na kuacha kuendelea kumchapa kisha akashika kiunoni mkono mmoja haya niambie “Mery gani, huyu rafiki yako.
“Ndiyo mama.’’
‘’Wewe ndiyo umekuwa mshenga si ndiyo?’’
‘’Hapana mama, mimi kangasu alinipa tu akasema nimpe Mery hata sijaisoa.’’
Haja badilisha haraka hizo nguo zako za shule twende huko, fanya haraka, pumbavu sana wewe, mama  Maliamu alisema kwa jazba huku kifua chake kikipanda na kushuka kwa hasira.
Je, mama Maliamu anataka kumpeleka wapi mwanaye? Usikose Jumanne ijayo sehemu inayofuatia.
      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.