Mpenzi msomaji ni nakukaribisha kwenye jamvi letu la Ujasiriamali tujifunze namna ya
kutengeneza fedha. Baada harakati za Uchaguzi Mkuu, hatimaye jana tumemaliza
mtihani huo na tunachosubiri ni matokeo ya kumtangaza rais wa awamu ya tano
atayetuongoza Watanzania.
Rai yangu, ni vema
tukakubaliana na matokeo yatakayotangazwa na tume husika ili kuepusha malumbano
na tuendelee na harakati zetu za kutafuta fedha.
Leo kwenye Ujasiriamali nitaelezea
namna ya kufanya biashara ya kuuza uji maeneo mbalimbali mitaani. Biashara hii ni
ndogo lakini inaweza kuwa ni kubwa kwa mtu mwenye nia na maono ya kufika mbali
kwa kutumia biashara hii.
Kuna msemo husemao ‘kazi ni
kazi ilimardi mkono uende kinywani’. Kwa mantiki hiyo, kazi yoyote yenye
kuingiza fedha fanya! Kikubwa ni kipato.
Kimsingi katika biashara
ya kuuza uji unaweza kuanza na mtaji mdogo. Kwa mfano unaweza kuanza na chupa
moja ya uji wa ulezi kwa gharama shilingi elfu kumi na mbili.
Kabla ya kuianza ni lazima
uwajue wateja wako, eneo utakalofanyia biashara na bei wanayoweza kuimudu
wateja wako watarajiwa.
Baada ya kufahamu vitu
hivyo vichache, kinachofuatia nikujua namna ya kuandaa uji wako katika hali
nzuri na salama kiafya.
Ni lazima ujue uji wako
utakuwa na mchanganyiko wa vitu gani ili kuleta ladha tofauti kwa wateja wako.
Kama kuna kuna aina f’lani ya ladha waliyozoe basi wewe uje na nyingine ili
kushindana na mshindani wako kama yupo eneo hilo.
MCHANGANYIKO UFUATAO UNAFAA KATIKA UJI WAKO;
Ili kuufanya uji wako kuwa
na ladha tofauti unaweza kuwa na vitu vifuatavyo utakavyovichanganya katika uji
wako;
PILIPILI MANGA
Kwa kutumia kiungo hiki,
kitachangamsha kiasi f’lani uji wako na kuufanya uwe na ladha ya ukali kidogo, pamoja
na harufu nzuri iliyonacho kiungo hicho. Inashauriwa iwe kiasi kwa maana
wengine si wapenzi sana.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U