Thursday, August 17, 2017

Published 8/17/2017 04:52:00 PM by with 0 comment

NILIOLEWA NA KUACHIKA SIKU YA HARUSI YANGU



Kila nikikumbuka nashindwa hata kulia, nimejaribu kujiua zaidi ya mara tano lakini ilishindikana, sasa hivi naamini Mungu anataka niishi na nimeamua kupiga moyo konde ili niendelee na maisha kwani kama nipo hai leo basi naamini Mungu ana sababu zake.

Mimi ni Binti wa miaka 30, sijaolewa lakini miaka mitatu iliyopita nilifunga ndoa ya kiislamu lakini mume wangu alinipa talaka tatu siku hiyo hiyo ya harusi, yaani ndoa tulifunga asubuhi akanipa talaka saa nne usiku siku hiyo hiyo ya harusi.
Nimeamua kundika kisa changu Kaka kwasababu umeniponya, umenipa matumaini mapya na nataka wanawake wenzangu kujigunza kutokana na ujinga wangu. Kuna mambo mengi ambayo wanawake tunayafanya kwaajili ya kukomoa watu wengine lakini yanakuja kutugeukia huko baadaye.
******
Kwakifupi nikuwa wakati niko chuo mwaka wa kwanza nilipata Baba mmoja, mtu mkubwa tu serikalini, sasa kama unavyojua wanaume watu wazima wanavyojua kuhonga, alikua akinihudumia kwa kila kitu, alinipangia chumba na kunilipia ada.

Mwanzoni nilimuambia nampenda lakini amheshimu mke wake, mambo yalivyoendelea nikapata kiburi cha pesa tukaacha kufanya kificho tukawa tunatoka dhahiri. Lakini yule mwanaume nilimuweka kiganjani hivyo nilikua namuendesha.
Zamani alikua hataki nimpigie wakati akiwa na mkewe, lakini wivu ukanijaa hivyo nikajikuta nampigia wakati wowote na kwakua nilishamuweka kiganjani alikua anapokea simu hata mbele ya mkewe.
Siku hiyo mkewe alinipigia simu na kuniomba niachane na mume wake, kusema kweli nilimtukana kama mtoto mdogo, nikimuambia mume ni wakwake akiwa kwake lakini akitoka ni wetu sote.
Lakini Mama wa watu hakuishia hapo alinifuata kabisa, ni Mama mtu mzima karibu kufikia umri wa Mama yangu. sikumjali, sikua tayari kuachana na pesa hivyo nilijikuta naingiwa na shetani nataka hata kumpindua yule Mama.
Sikuishia kupiga simu tu, nilikua natuma mpaka mapicha na vizeo za uchi, namtumia yule mwanaume nikiwa bafuni, nikiwa chumbani, na kila kitu. Sikujali kama mkewe anajua wala nini na nilituma hivyo ili kumkomoa yule Mama kwa kunifuatafuata.
Maisha yaliendelea, nilimazlia chuo na kupata kazi yangu nzuri tu, baada ya kupata kazi nilipata mchumba ambaye ni mfanyakazi mwenzangu hivyo niliachana na yule mzee na kwa bahati nzuri nilipomuambia hakuning’ang’ania sana alinielewa.
Miaka miwili baadaye nilichumbiwa na kuandaliwa harusi kubwa tu. Sherehe ilifana kwani tulikua tunapendana sana, sasa kilichotoke siku ya harusi yangu kilibadilisha maisha yangu kabisa na mpaka leo ninalia na najutia kwnaini nilifanyaujinga ule.
******
Ilikua ni siku ya furaha sana kwangu, lakini iliingia kinyongo wakati wa zawadi, watu wakiwa bado hawajala chakula zawadi zilianza kumiminika huku mziki mkubwa ukipigwa.

Wakati zawadi zinatolewa kama mnafahamu katika ukumbi kunakua na Projectile ambazo huwekwa kwajaili ya kuonyesha picha za matukio ukutani kwa wale walioko mbali. Lakini pia kuna zile CD ambazo huwekwa kwaajili ya kuonyesha picha za zamani za Bwana na Bibi harusi enzi za utoto wao kama historia flani.
Sasa kuna kijana mmoja aliomba kuwekewa CD yake, ilinza kwa mziki, lakini ghafla picha kwenye Projectile ukutani zilibadilika, zilikua ni picha zangu za uchi, zile zile mabazo nilimtumia yule Baba wakati nikiwa chuoni.
Mwanzoni sikujua mpaka niliposikia kelele, ilibidi DJ kuzima harakaharaka lakini alishachelewa kila mtu alikua ameona. Lakini haikuishia hapo simu ya mume wangu iliingia meseji ya whatsapp.
Kulikua na video ambazo pia nilimtumia yule Baba, nikijifanyia mambo ya ajabu ili kumtega. Simu ya Mwenyekiti wa kamati nayo iliingia meseji na baadhi ya ndugu wa upande wa mume wangu, ikiwemo Baba mkwe wangu.
Harusi ilibadilika na kuwa kelele, kila mtu akiongea chake, wakwe zangu walikasirika, mume wangu hakusubiri hata kutoka ukumbini alinipa talaka tatu palepale, akaniacha huku akisema nimemdhalilisha mbele ya ndugu zake na wafanyakazi wenzake.
*****
Hakuna siku ambayo niliwahi kuaibika kama siku ile, watu walimsihi mume wangu lakini wapi, hakusikiliza. Aliondoka kabisa na kuniacha ukumbini, nilijikuta na dondoka na kupoteza fahamu, walinipeleka hospitali.

Lakini haikuishia hapo, kesho yake picha na video zilisambaa Ofisi nzima. Nilikaa ndani wiki tatu nalia tu, nilishindwa hata kwenda kazini kutokana na aibu, nilijaribu kunywa sumu mara tatu lakini zote hizo niliwahiwa na kupona.
Nilijaribu kunjinyonga na hata kujichoma kisu lakini niliokolewa. Kazini niliacha kabisa kazi kwani mbali ya aibu sikutaka kwenda kuonana na mume wangu ambaye wiki mbili baada ya lile tukio alioa mwanamke mwingine.
Sasa hivi naendelee vizuri na namshukuru Mungu kwamba ni watu wachache tu wale wakatribu wanajua kwani haikutumwa sana kwneye mitandao. Nimehama mkoa na sasa nafanyabishara ndogondogo sitaki hata kwenda kuomba kazi sehemu.
Nimeamua kuandika kisa changu kwakua bado kuna wanawake wanatembea na waume za watu na wanawatumia picha za uchi wakidhani kuwa wanawakomoa wake zao. Wanawaona wale wake zao wajinga labda wataziangalia na kuziacha tu.
Ingawa yule Mama kitendo alichonifanyia kilikua cha kinyama lakini simalaumu sana kwani hata mimi niliyomfanyia yalikua ni ya kinyama pia. Bado wanawke wengi tuna ule ujinga kuwa ukishaangalia picha zifute.
Humkomoi mtu yeyote zaidi ya kujidhalilisha kwani hakuna mwanamke atamuacha mumewe wametoka mbali kwasababu ya kimalaya flani kimetuma uchi wake kunuka katika simu yake!
Hivyo badilika, yule ni mkewe na ipo siku atajitambua ataenda kumuomba msamaha na atamsamehe, wewe atakuaibisha na kukuharibia maisha yako yote.
Mimi mpaka sasa hivi naogopa hata kuolewa tena kwani najua kuwa yanaweza kunitokea yaleyale. Hata nisipoolewa harusi vipi akituma picha zangu za uchi ofisini kwa mume wangu, akawatumia marafiki zake.
Mimi nitavumilia aibu, nitazoea lakini je huyo mwanaume atavumilia, vipi wakwe zangu wakaitumiwa watakuaje. Naumia sana na nina wasiwasi sana, ujinga kidogo umeniharibia maisha yangu. usifanye ujinga kama mimi.
Nimejaribu kumuomba msamaha yule Mama lakini anasema sio yeye kafanya vile labda ni wanaume wengine niliokua nawatumia, ukweli sikua na mwanaume mwingine lakini siwezi fanya chochote zaidi ya kulia tu na kumuomba Mungu ampe roho ya imani aisizidi kunishalilisha.

Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com



Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com
Read More
      edit

Wednesday, August 16, 2017

Published 8/16/2017 01:45:00 PM by with 0 comment

ANALAZIMISHA PENZI

Habari wana ME&U mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 hivi karibuni nimetokea kuanzisha mahusiano na kijana mmoja ambaye ni mfanya kazi wa kampuni moja ya uwandishi. Kitu ambacho kinachonisumbua ni kwamba ndani ya mwezi mmoja na mpenzi wangu huyo hatujawai kujihusisha na mapenzi licha ya yeye mwenzangu kunisumbua mara kwa mara.

kwa kipindi chote hicho uwa namzungusha kumpa tunda hivyo juzi akaniambia kwamba siku ya jpili tukutane na kupeana tunda lakini mimi nikaona ni mapema mno.Hivyo akatoa kiapo na kusema kwamba hiyo jumapili nisipoenda atachukua maamuzi mengine sasa sijui maamuzi hayo ni ya nini nisimpa unyumba nami sitegemei kwenda kukutana nae. naona kama amekuwa aking'ang'ania sana tufanye mapenzi.sijui kama ananipenda kweli huyu maana naona kama anataka tu penzi kisha anachukua hamsini zake.Naomba mnishauri maana anadai kwamba ananipenda na hana hisia za mapenzi kwangu?



Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com


Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com
Read More
      edit
Published 8/16/2017 01:22:00 PM by with 0 comment

AMBER LULU AFUNGUKA

Video queen aliyeikacha fani yake na kuzamia kwenye muziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu amekiri kuwa anajichubua rangi ya ngozi yake na kuwatolea mapovu wanaomsemasema kuhusu ishu hiyo.
Staa huyo anayetamba na ngoma yake ya Watakoma, aliyomshirikisha mkali wa Hip Hop Bongo, Country Boy, amewatolea mapovu watu wenye tabia ya kuchukua picha zake za miaka ya nyuma na kuzifananisha na za sasa, kisha kumsema kuwa anajichubua.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, amejibu mapigo kama ifuatavyo:


“Pale unapoona watu mapovu kibao ooh mweusi sasa na wewe si ujichubue. Au huna hela za kiduka cha usiku? Maisha ni mafupi sana.
“Mimi na feki, sasa mbona mnani-follow mna-like tena kuiga ndo msiseme, muulize tu Amber unatumia mkorogo gani, maana sio kwa mabadiliko hayo.

“Mimi napambana na tube zangu, pambana tu na wewe na hali yako. Kujichubua nijichubue mimi hasira upate wewe duh! Unazionea huruma pesa zangu wakati natafuta kwa jasho langu, kivipi.

“Na mwisho wake haimhusu mtu ngozi yangu pesa yangu mikono yangu naupaka vizuri maisha yangu.
Na hizo TBT ni za kitoto hapo nimekuwa mtu kabisa ngoja niwape kiboko kabisa sasa.



“Siogopi kwa sababu ndiyo mimi ndipo nilipotokea na ndivyo nilivyo kuwa wewe.
Tena sasa hivi nataka wa Kiarabu niwe Mhindi kabisa Waarabu nicheki Dm nizidi mie,” ameandika Amber Lulu.


Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com


Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com
CHANZO: GPL
Read More
      edit

Sunday, August 13, 2017

Published 8/13/2017 09:28:00 AM by with 0 comment

NANI ATAANZA KUSEPA, MWANAUME/MWANAMKE:


Kati ya mwanamke na mwanaume nani akiachishwa kazi uwezekano wa kuharibu uhusiano au kumuacha mwenziye ni mkubwa?

Naomba karibu kwa maoni na ushauri wako. Kwa elimu zaidi ya UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp: +255679979785.

Read More
      edit

Saturday, August 12, 2017

Published 8/12/2017 07:33:00 PM by with 0 comment

USILIOUS UKIZIDI SANA UNAHARIBU LADHA YA MAPENZI


Mapenzi yana raha kama pande mbili zikiwa na amani. Mwanamke awe na amani, mwanaume pia. Tofauti na hapo, penzi hugeuka mateso kwa mmoja wapo. Uhusiano unapoteza mvuto, mtaishia kuachana. Mapenzi yanapendeza wawili mkifanana.

Mkiendana kitabia, kifikra. Mtainjoi zaidi uhusiano kama mkiwa mnazungumza lugha moja na mwezi wako. Mnakwenda sawa katika kila jambo. Kwenye wakati wa furaha, mnakuwa pamoja na kwenye huzuni hali kadhalika. Mapenzi yanahitaji lugha rafiki. Wakati mwingine yanahitaji kuchombezana, kuliwazana na kama haitoshi kudekezana.

Kuna wakati mwenzako anaweza kufanya jambo unaloweza kuliona ni la ‘kijinga’, kakutania, yote hiyo ni mapenzi tu. Anahitaji kukuona unacheka. Anapenda kukuona una furaha wakati wote. Anakutania anakusemesha hata mambo ambayo wakati mwingine unaweza kuona hayana maana. Anakuuliza vitu ambavyo havina kichwa wala miguu.

Katika hili wanaume wengi ni waathirika. Ukizungumza na wanaume wengi watakupa ushuhuda wa aina hii; ‘wanawake bwana sijui wapoje? Wakati mwingine wanakuwa na mazunguzo yasiyo na msingi. Wanaboa kweli wakati mwingine’ Mathalan, anauliza swali ambalo jibu lake analo. Anataka tu umjibu. Si kwamba hafahamu jibu lake, anajisikia tu furaha ukimjibu wewe mpenzi wake.

Akiwa na wewe anataka mcheke. Anatamani umdekeze, moyo wake unasuuzika. Kutokana na pilikapilika za kila siku za maisha au kutokana na hulka za baadhi ya watu, wapo baadhi ya watu ambao kwa namna moja au nyingine suala la kuwa ‘romantic’ linawashinda. Yeye wakati wote yupo serious. Humuoni akicheka. Muda wote sura yake ni ya kazi.

Hana mazungumzo ya utani hata kidogo. Sura anayokuwa nayo anapokuwa na rafiki zake wenye jinsia yake, ndiyo hiyohiyo anaiweka anapokuwa na mpenzi wake. Anaishi ‘kikakamavu’ kama vile askari. Akiwa kazini, akiwa mtaani na wenzake, akiwa chumbani lugha yake ni moja.

Anaongea kwa ukali. Hakuna muda wa kuchekacheka. Yeye ni mtu wa amri tu na kusubiri utekelezaji. Amri anazozitoa kwa wafanyakazi wenzake ofisini ndizo hizohizo anazitoa kwa mkewe. Kila muda yupo serious, ni mtu wa kutoa maagizo. Neno lake ni kama sheria. Inafika mahali hata watoto wanamuogopa.

NI TATIZO
Unapokuwa kwenye uhusiano halafu muda wote unakuwa serious, inaondoa uzuri wa uhusiano. Unatengeneza mipaka kati yako na mwenzi wako.

HUPUNGUZA URAFIKI

Ukiwa serious sana, mwenzi wako anapunguza urafiki. Anakuhofia, matokeo yake analazimika kuzungumza utani na mtu mwingine ambaye anapenda utani kwelikweli.

HUONGEZA USHAWISHI WA USALITI

Iko wazi, mwenzi wako anapokosa raha ya uhusiano kwako, akiwa na moyo mdhaifu anaweza kushawishika kusaliti endapo tu atakutana na mtu atakayempa kile ambacho wewe humpi.

KUWENI ROMANTIC

Mwanaume unapaswa kuwa mlaini kidogo kwa mwanamke vivyo hivyo mwanamke. Kweli kuna wakati mkubwa zaidi wa kuutumia mkiwa serious lakini msisahau kuwa na utani, kuchekeshana kwa hapa na pale na mambo mengine kwani yanaongeza utamu au maana ya penzi. 

VUMILIANENI


Wakati mwingine unaweza kuona kwamba utani au vitu vya mzaha anavyokueleza mwenzako havina maana lakini hakuna namna, msikilize na umuunge mkono. Mtaniane kwa kiasi, mcheke kwa kiasi kwani ndiyo chachu ya kuufanya uhusiano wenu uwe hai. Mkizingatia hayo, mtaishi vizuri na mtafurahia uhusiano.

Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com


Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com

CHANZO: GPL
Read More
      edit
Published 8/12/2017 01:32:00 PM by with 0 comment

KADJA NITO AMBADILI DINI MTOTO WAKE


BAADA ya kubadili dini kutoka kwenye Uislam na kuolewa na mwanaume Mkristo, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Natasha Lisimo ‘Kadja Nito’ hatimaye amembadili dini mtoto wake, Nito ambaye naye alikuwa Muislam.
Chanzo kiliimbia Mikito Nusunusu kuwa, bishosti huyo ameamua kumbadili dini mwanaye Nito ambaye alizaa na mumewe wa awali kabla ya huyu wa sasa, Lisimo, jambo lililomkera baba wa mtoto huyo.
Kadja alipotafutwa kuhusu suala hilo aligeuka mbogo na kujibu kwa hasira:

“Sasa cha ajabu hapo kiko wapi ikiwa mtoto ni wangu na mimi ndiyo minaishi naye tangu akiwa mdogo nilivyoachana na baba yake? Mwanangu kwa sasa ni Mkristo kama mimi na tunakwenda wote kanisani.”

Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com


Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com

CHANZO: GPL
Read More
      edit
Published 8/12/2017 06:20:00 AM by with 0 comment

MAGAZETI LEO, AGOSTI 12, 2017
































Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com


Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com


Read More
      edit

Wednesday, August 9, 2017

Published 8/09/2017 05:53:00 PM by with 0 comment

LULU DIVA AJISIFU KWA UZURI


Msanii wa Bongo Flava, Lulu Diva amejimwagia sifa jinsi anavyoamini kuwa yeye ni mzuri.
 Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Uhondo cha E Fm kuwa alitambua kuwa yeye ni mzuri kutokana na sifa alizokuwa akipewa na mama yake mzazi kitu ambacho  kilimfanya kutolaghaika na watu waliokuwa wakimsifia.
“Mimi ni msichana ambaye nipo sex ambaye nina mvuto, mama yangu alikuwa akiniambia Lulu mwanangu mashallah, yaani hapa sidhani kama kuna mtu nitamwambia idadi ya ng’ombe ninazozitaka halafu akapindua,” amesema na kuongeza.
“Na mimi mwenyewe nikawa najiona ndio maana hata sikuweza kurubunika, yaani ile mtu kuniambia wewe mzuri akanidanganya kwa vichipsi mayai, mwenyewe nilishajijua ni mzuri,” amesema Lulu Diva.
Hitmaker huyo wa Usimwache kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake inayokwenda kwa jina la Utamu.


CHANZO: BONGO 5 
Read More
      edit
Published 8/09/2017 05:25:00 PM by with 0 comment

MUIGIZAJI MAMA ASHURA ASEMA HATOKI NA MENEJA WAKE BALI NI MUME WAKE KABISA

Muigizaji wa Timamu Entertement, Mama Ashura amepinga vikali tetesi zilizozagaa kuwa amesababisha kuondoka kwa muigizaji Mkali Wenu katika kampuni ya Timamu kwa kuwa anamahusiano yasio rasmi na bosi wa kampuni hiyo.


Akiongea na Bongo5, mrembo huyu ambaye ni mahiri awapo katika kazi yake amedai hatembei na Meneja wake bali Meneja wake ni mume kabasa wa ndoa.
“Watu wanashindwa kuelewa mimi sitoki na meneja wangu, meneja wangu ni mume angu kabisa, watu wanatakiwa wajue, nina miaka naye sita kabla watu hawajanijua kama Mama Ashura na nina mtoto naye kwa hiyo familia zetu zinajua kabisa huyu ni mke na mume,” amesema Mama Ashura.

Alisisitiza kuwa “Baada ya watu kuona nimetoka kama Mama Ashura mwaka juzi, wakati mimi nipo muda mrefu kwa hiyo watu wasinichukulie mimi namna gani, watu wasinichukulie kisa natoka na fulani ndiyo maana amepewa nafsi hapana, mimi nimeanza sanaa kabla sijamjua Timos ,Mume wangu.”

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa


 CHANZO:BONGO5
Read More
      edit