Hii siyo mara yangu ya kwanza
kumzungumzia Wema katika safu hii na kwa maana hiyo, sitarudia kuzitaja
sifa zake nyingi katika uigizaji wa fi lamu. Na siyo kwamba ninakutana
naye hapa mara nyingi kwa sababu nina chuki naye, hapana, huwezi kuwa na
chuki na mtu kama Wema, ambaye ni mkarimu kwa kila mtu, uongo?
Huyu binti ni role model wa watu wengi
sana, wake kwa waume na katika akaunti yake ya Instagram, ana wafuasi
zaidi ya milioni moja. Hao ni watu wengi mno, ina maana akitaka
kuhamasisha kitu, wanaweza kutoa ushawishi kwa idadi nyingine kama hiyo
na kitu kikasimama.
Kwa maana hiyo, mtu kama huyu ni rahisi
kuweka mwelekeo anaoutaka, ndiyo maana akapata hata jeuri ya kuanzisha
App yake na watu kibao wanaifuatilia. Juzi hapa nimeona kitu Wema
ameandika katika akaunti yake ya Instagram, anawataka mashabikiwake
wakubali ukweli kuwa yeye hivi sasa hana mpenzi, kwani uhusiano wa
kimapenzi aliokuwa nao zamani, hivi sasa umeisha kwani kila mmoja ana
maisha yake.
Lakini aliponikosha ni pale aliposema
anawaomba wamuombee kwa Mungu apate mwanaume mzuri wa kuweza kumuoa,
tena mwanaume huyo awe na mihela miiiingi!
Hapo kwenye mihela mingi ndipo
paliponitatiza. Nimewahi kusema huko nyuma, kuwa Wema kwa kule majuu,
unaweza kumfananisha na binti mmoja anaitwa Kim Kardashian, mtangazaji
wa televisheni ambaye pia ni mke wa rapa mashuhuri duniani, Kanye West.
Kuna watu wanamsema binti huyu wa Kinyaturu kuwa eti ‘ametoka’ na
wanaume wengi.
Kwa taarifa yao ni kuwa Kim, kabla ya
kuangukia mikononi mwa West, alishatoka na mastaa zaidi ya 25, achilia
mbali wale ambao hawaeleweki. Huu ni umri wa Wema kutafuta mume mwenye
busara wa kumuoa na siyo mwenye fedha kwa sababu hawa wenye mkwanja
mbona amesha-hag nao sana tu? Kila mmoja anajua kuwa ili kutoka na
supastaa Wema ni lazima uwe na waleti iliyonona, siyo kwa ajili ya
kumpa, bali kwa sababu ya gharama za kum-handle
Nilidhani angetumia nafasi ile kuwaomba
mashabiki wake, wamuombee kwa Bwana Mungu wake, ampate mume bora wa
kumuoa ambaye ni mwenye hofu ya Mungu, busara, hekima na upendo, maana
ndicho kitu cha msingi zaidi mwanamke anakihitaji kutoka kwa mwanaume
anayempenda.
Mwanamke anayetafuta mwanaume mwenye
hela, hawezi kumpata wa kumuoa, bali wa kumchezea tu kwa sababu wenye
hela hawajui kupenda, atapenda wangapi wakati kila mrembo anamhitaji?
Wanaume wengi wenye hela huoana na wapenzi wao walioanza nao kuhangaika
pamoja, hawa wengine wanaojitokeza huku juu, huwa ni wa kupotezea tu
wakati.
Hivyo nikupe ushauri mdogo wangu,
kwanza umri wako wa kuolewa umeshafi ka, ni vyema na haki sasa ukatafuta
mtu wa kutuliza naye mpira. Pili, usiwaze sana kuhusu hela, zinatafutwa
na wewe unao uwezo wa kuzipata, ukazitumia na mumeo. Umekutana na
wanaume wengi wenye nazo na wewe ukazitumia sana, hukuwekeza ili zikufae
ndiyo utampa wakati huu?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
CHANZO: GPL