Huyu kaka kijijini huko alinipenda tokea nikiwa form one
na yeye form 3 kiukweli mimi sikuwahi kujua kupenda na wala hiyo maana
nilikuwa sina ila kijana inaonyesha alikuwa na real love kwangu barua
nikiwa shule ananitumia na hela kwenye barua nakula hela zake lakini
akitaka kunikiss namwambia ni dhambi na mama amenikataza.
Hili
alikubali sababu anajua mama yangu ni mlokole na ni mkali nikimsemea
ataenda washa moto pale kwao namnyima vyote ila pesa yake nachukua na
tunapiga story sana tu ila hakuna kugusana ni dhambi na hapo mimi
nimesoma girls japo fom two kuna mambo yalitokea lakini yeye siyo sababu
nikachukia wanaume wote pamoja na yeye ila pesa yake sikuacha
niliipenda.
Form four akaomba mchezo nikachomoa kwa kigezo kile
kile cha dhambi na kwamba hanipendi mpaka ndoa kaka wa watu akakubali
tukawa wapenzi wa mdomo tu nimeingia advance huku Dar shule ya dei
nikapata kaboyfriend (h ahaha huyu sitasahahu tulikimbizwa na wanajeshi)
story ndefu hapa basi jamaa yangu huyu wa kusubiri nikawa nampotezea
ila nikiwa na shida ya hela namwambia ananipa kwa kigezo me ni mke wake
kiukweli siwezi sema kama nilikuwa namchukia hapana.
Nikaingia
chuo khee ndiyo majanga zaidi nikaamua kumla kibuti akajaribu kujiua
kaka yake akamuokoa aisee nilisutwa na wachaga wale sitasahau na
kuambiwa akifa ni juu yangu mmh any way sipendi kukumbuka.
Kwa
sasa ana mke na watoto wawili na anaishi Mwanza juzi kanitafuta anakuja
kuniambia kuwa anakosa amani hana furaha sababu anaamini mimi ndiyo mke
wake na mbaya zaidi kamwambia mkewe kuwa ananipenda mimi sioni tabu yeye
kunipenda ila tatizo lipo kwangu nimemueleza haya naona haelewi
1. Huyu kaka ni mtu mzuri mno mno yani hastahili mwanamke kama mimi na
ningekuwa naye ningekuwa nimeokota embu kwenye mwarubaini lakini siwezi
kuwa naye naona nitamtesa hata kama angekuwa hajaoa mmmh hapana
nimejichekecha wee siku ya tano leo bado najiona sistahili hata chembe
kuwa na kijana huyu he is so nice to have a person like me naomba wakuu
muelewe na mumshauri.
2, Nimemwambia siwezi penda wanao kama mama
yao anavyowapenda ila yeye anasema hakuna shida atawapeleka boarding
naogopa kumpa za uso asijejaribu tena kujitoa duniani aache viumbe hawa
wateseke.
3. Anasema yupo tayari kunipa chochote ni kweli anaweza
sababu nakumbuka shamba la baba yake alilompa jina langu na lake lipo,
mimi ni mlaghai jamani na sijui kama kabadilisha umiliki haikuwa ni hati
ila makabidhiano naona kabisa njia ile ya kumchuna huyu kiumbe ila
watoto watateseka na hii familia machozi yao hayataniacha salama mmmh
sipo tayari.
4. Nitamtesa najua unanipenda sana ooh no sideserve.
Mwisho wa kunukuu
TUIACHE STORI... TUIWEKE KANDO
NINA HAYA MASWALI
1. Wanaume wanaopenda hivi wapo kweli? Wanapatikana wapi?
2. Mke ukigundua mumeo kitaaambo tu amedata na mtu namna hii utajisikiaje? Utaendelea kuwepo? Utafanyaje?
3. Nini kinafanya mtu anampenda binadamu mwenzake kiasi hiki?
4. Yawezekana anakuwa anajua alipendewa pesa au anapendewa pesa nk ila bado tu anataka kuwa na wewe no matter what! Kweli???
5. Je ina maana kuna wanaume wanaoa huku mioyo yao iko kwingine????
ETI?
Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com
Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com
Read More