Wednesday, November 30, 2016

Published 11/30/2016 04:46:00 PM by

USHAURI WAKO: MTANDIO ULIVYOVURUGA NDOA YANGU!


Naitwa Ata ni mwanaume mwenye mke na watoto 3, nikiwa kwenye daladala natokea Msasani naenda Chanika nilikutana na dada mmoja ambaye nilikaa naye siti moja.
Kutokana na foleni ilivyokuwa kubwa ikafika sehemu tukaanza kuongea na yule dada ambaye alisema ameokoka.
Daladala uliendelea kwenda mazungumzo yakanoga, hatimaye tukabadilishana namba za simu. Baada ya vituo kama viwili yule dada aliniaga akashuka.
Daladala iliendelea na safari, nilipokuja kuangalia kwenye siti aliyokuwa amekaa alikuwa amesahau mtandio wake.
Nikampigia simu na kumwambi kuhusu mtandio, nikamuuliza niuache tu kwenye daladala au inakuaje. Akaniomba niuchukue afu nitamtafuta ili nimpatie, niliuweka kwenye begi langu.
Nilishuka nakuendelea na mishe zangu kama kawaida, muda wa kufika nyumbani ukawadia, kama kawaida yangu nikafika na kuweka begi kama siku zingine wakati huo akili yangu imesahau kama kuna mtandio ndani ya begi.

Nilienda kuoga, niliporudi chumbani kikakuta mke wangu kanuna vibaya, kashika kiuno mkononi kashika ule mtandio na kuniuliza "kwa hiyo umalaya wako umefanya huko nje, umechoka na sasa umeamua kubeba na mtandio wa mchepuko wako, si ndiyo."

Nilijaribu kumuelewesha mke wangu hanielewi, ila nikawa nimefahamu pia kuwa kumbe mke wangu huwa ananikagua kwenye begi langu.
Nampenda mke wangu, naombeni ushauri wenu, nifanyeje ili anielewe.

Kwa USHAURI, MADA ZA MAPENZI, HADITHI, MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook, Insta: mimi_na_uhusiano
      edit