Thursday, December 15, 2016

Published 12/15/2016 05:26:00 AM by

MAGAZETI YA LEO 15 DEC, 2016























Read More
      edit

Wednesday, December 14, 2016

Published 12/14/2016 11:00:00 PM by

MKASA WA KWELI: NIMEAMUA KUJIUZA!



Nilijitunza sana ili nisiuharibu mwili wangu kwa kurukaruka na wapenzi tofauti.
Niliamua kuishi bila mpenzi kwa muda mrefu sana lakini mwisho niligonga mwamba kwa kaka mmoja ambaye ni mwenyeji wa Arusha, mkazi wa Morogoro.
Ilichukua muda mrefu kumuamini na kumkabithi moyo na mwili wangu. Nilihakikisha najiridhisha kwa kila hatua ili nisije nikaangukia pua.


Nilimwambia naishi na mama pamoja na baba yangu wa kambo, tukiwa tunaishi kwenye kijumba chetu cha tope kwenye kijiji kimoja kilichopo mkoa wa Pwani.

"Kama kweli Maiko unanipenda basi njoo nyumbani japo ujitambulishe ishu ya mahari siyo tatizo, naweza kuongea na familia yangu wakatuelewa." Binti alimwambia Mpenzi wake.
Maiko aliniomba ajifIkirie kwanza kuhusu hilo, je nini kilifuatia baada ya Maiko kufikiria? Usikose sehemu inayofuatia ya mkasa huu kila Jumapili na Alhamisi saa 9 Alasiri.
Read More
      edit
Published 12/14/2016 08:43:00 PM by

FIKIRIA, SOMA, MSOMESHE KUJIAJIRI SI KUAJIRIWA!






Habari mpenzi msomaji, nikualike tena kwa upendo wa dhati kabisa katika somo letu linalojieleza hapo juu. Kupata nafasi hii ya kukupatia somo haimanishi mimi ni bora kuliko wewe, la hasha ila wewe ni bora zaidi kuliko mimi.
Dhamila ya somo tajwa nikukufanya ubadilike katika mtazamo mzima wa kufikiri na kuamua katika maisha yako.
Leo hii wanafunzi yoyote ambaye anasoma ukimuuliza swali, je, unasoma ili iweje? 
Bila shaka majibu ya walio wengi watakwambia, mimi nataka kuwa mwalimu, mimi nataka kufanya kazi benki, mimi nataka kuwa rubani, ni sawa! lakini, je, masomo au elimu anayoisoma moja kwa moja inampeleka kuwa rubani, mwalimu, askari, mwandishi, mwanamuziki na fani zingine? Utakuta hamna.
Watu wengi wanaamini baada ya masomo kuna ajira siyo KUJIAJIRI, wengi wanaamini wakimaliza chuo kwa masomo au mchepuo aliochukua basi atapata kazi fasta lakini kwenye uhalisia wa maisha haiko hivyo.
Somo la leo likubadilishe, uwaze namna ya kujiajiria na siyo kuajiriwa, hata kama una ndugu yako unamsomesha,someshe kujiajiria na si kuajiriwa, kwa kwa wanachuo hao ninaowaona baada ya kuhitimu vyuo mbalimbali sioni ajira zao zinazoweza kukidhi wingi wao.
Bila KUFIKIRIA, KUSOMA AU KUSOMESHA mwanao au mpenzi wako kwa lengo la kuja kujiajiria basi kila siku utaendelea kulalamika kuwa serikali haijatoa ajira mpya.
Serikali haifanyi kazi, kwa sababu wananchi wahitimu wanazurura hovyo mitaani na vyeti vyao wakisaka kazi.
Sina elimu kubwa sana ya kuajiriwa ila ni elimu kubwa zaidi ya kujiajiri.
Kuna wakati nauchulia vibaya mfumo mzima wa elimu yetu kwa sababu tu ni kama unampotezea mtu malengo yake, muda na mambo mengine, kwani mwanafunzi anasoma akijua anakuja kuajiriwa.
Katika uhalisia hizo ajira ambazo unazifikiria hazipo, na ni ujinga kusoma ukiamini utaajiriwa na kupata maisha mazuri.
Kama una mtazamo huo, umeula wa chuya, katika uhalisia wa maisha nje ya shule ni tofauti sana. Kuna kuzunguka na vyeti weeee na kazi hakuna, kuna kuombwa rushwa za pesa na ngono, kuna upungufu wa ajira zenyewe.
Lakini kama mfumo ungekuwa unakuandaa kujiajiri bila shaka kila mtu angekula mazao yake.
Fikiri zaidi kuhusu kujiajiri hata kama uko kwenye ajira, pamoja na kwamba haiwezekani wote tukajiajiri lakini wewe ambaye umebahatika kupata sumu ya kujiajiri basi fanya hivyo.

Msomeshe mwanao kwa kile anachokipenda, mtengenezee mazingira ya kujiajiri, kuwa mzalishaji wa bidhaa ili akimaliza masomo yake ajue anachofanya.
Kama unasoma, soma kwa kujiajiria na siyo kukalia vimbweta kwa kuamini kuwa unasoma ukaajiriwe.
Ninachoamini mabadiliko yanaanza na wewe muhusika kwa kujitambua kisha kufanya yale ambayo unahisi yanastahili kufanywa na wewe au mtu yeyote anayejitambua.
Acha kuifanya akili yako kuwa tegemezi, akili yako kuiegemeza kwenye kuajiriwa. Kwani huwezi kufanya japo jambo dogo la kujiajiria angalau kwa kufungua kibanda cha pipi, machungwa au genge kwa sababu tu una amini una tuzo unayostahili baada yakuhitimu chuo.
Hii siyo nchi ya hivyo, hata huko kwingine ambako unahisi kuna ajira kibao, si kweli, bali hata wao wanaangaika ila kwa kuwa mfumo wao wameufanya kujiajiri kwa mhusika na ndiyo maana leo hii tunatumia vifaa, huduma za wenzetu.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Read More
      edit
Published 12/14/2016 06:53:00 AM by

NDOA ZA UTOTONI ZAWAWEKA PABAYA WALIMU





Walimu wakuu Nzega Tabora wadai kutishiwa maisha na wazazi wanapohimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kukataa ndoa za utotoni
Read More
      edit
Published 12/14/2016 06:35:00 AM by

HABARI ZA MAGAZETI YA LEO 14 DEC,2016



























Read More
      edit

Friday, December 9, 2016

Published 12/09/2016 05:02:00 PM by





MADA YA LEO USIKU:  MAJI HAYASAHAU BARIDI HATA YACHEMKEJE!

Tabia ni kama ngozi, kwa mtu ambaye tabia yake ni ya unafiki hata kama atapewa ukiongozi wa dini fulani tabia yake ya asili ni ngumu kuiacha sanasana atakuwa anaishi maisha ya kuigiza kutokana na ninyi kumsimanga.
Ingawa kwa maombi na msaada wa Mwenyezi Mungu anaweza kubadilika kama kweli ana nia ya dhati ya kubadilika kutoka kwenye tabia hatarishi au mbaya.
Kama Msanii Ray aliamini kuwa maji yanaweza kubadili rangi yake ya zamani na.kuwa nyingine, kwa nini wewe tabia yako isibadilike!

Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI, MACHOMBEZO NA MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI.
Kwa kujiunga na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook
Read More
      edit

Thursday, December 8, 2016

Published 12/08/2016 01:58:00 PM by

NAOMBA USHAURI KAMA SIYO UTAPELI WA MAPENZI NI NINI!




Mimi ni kijana wa miaka kadhaa, kuna binti mtaani ana mtu wake wa muda mrefu lakini cha ajabu amekuwa akining’ang’ania na mimi tuwe na uhusiano hii inakuaje.
Nikweli ana nipenda nafahamu hilo lakini ataweza kutupenda wote kama siyo utapeli wa mapenzi! Nimejaribu kumwambia lakini hanielewi, kiasi kwamba imekuwa kero kwangu. Naombeni ushauri wenu, nifanyeje?

Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI, MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Read More
      edit

Wednesday, December 7, 2016

Published 12/07/2016 06:30:00 PM by





 MUNGU NISAIDIE KUNIVUSHA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU MAISHANI MWANGU


Mbona mapenzi kwangu yamegeuka shubiri, mbona kwangu yamekuwa ni  hatari  kama kisu chenye ncha kali, nimekosa nini, tatizo langu nikukupa moyo wangu uutunze!
Read More
      edit