Wednesday, December 14, 2016

Published 12/14/2016 08:43:00 PM by

FIKIRIA, SOMA, MSOMESHE KUJIAJIRI SI KUAJIRIWA!






Habari mpenzi msomaji, nikualike tena kwa upendo wa dhati kabisa katika somo letu linalojieleza hapo juu. Kupata nafasi hii ya kukupatia somo haimanishi mimi ni bora kuliko wewe, la hasha ila wewe ni bora zaidi kuliko mimi.
Dhamila ya somo tajwa nikukufanya ubadilike katika mtazamo mzima wa kufikiri na kuamua katika maisha yako.
Leo hii wanafunzi yoyote ambaye anasoma ukimuuliza swali, je, unasoma ili iweje? 
Bila shaka majibu ya walio wengi watakwambia, mimi nataka kuwa mwalimu, mimi nataka kufanya kazi benki, mimi nataka kuwa rubani, ni sawa! lakini, je, masomo au elimu anayoisoma moja kwa moja inampeleka kuwa rubani, mwalimu, askari, mwandishi, mwanamuziki na fani zingine? Utakuta hamna.
Watu wengi wanaamini baada ya masomo kuna ajira siyo KUJIAJIRI, wengi wanaamini wakimaliza chuo kwa masomo au mchepuo aliochukua basi atapata kazi fasta lakini kwenye uhalisia wa maisha haiko hivyo.
Somo la leo likubadilishe, uwaze namna ya kujiajiria na siyo kuajiriwa, hata kama una ndugu yako unamsomesha,someshe kujiajiria na si kuajiriwa, kwa kwa wanachuo hao ninaowaona baada ya kuhitimu vyuo mbalimbali sioni ajira zao zinazoweza kukidhi wingi wao.
Bila KUFIKIRIA, KUSOMA AU KUSOMESHA mwanao au mpenzi wako kwa lengo la kuja kujiajiria basi kila siku utaendelea kulalamika kuwa serikali haijatoa ajira mpya.
Serikali haifanyi kazi, kwa sababu wananchi wahitimu wanazurura hovyo mitaani na vyeti vyao wakisaka kazi.
Sina elimu kubwa sana ya kuajiriwa ila ni elimu kubwa zaidi ya kujiajiri.
Kuna wakati nauchulia vibaya mfumo mzima wa elimu yetu kwa sababu tu ni kama unampotezea mtu malengo yake, muda na mambo mengine, kwani mwanafunzi anasoma akijua anakuja kuajiriwa.
Katika uhalisia hizo ajira ambazo unazifikiria hazipo, na ni ujinga kusoma ukiamini utaajiriwa na kupata maisha mazuri.
Kama una mtazamo huo, umeula wa chuya, katika uhalisia wa maisha nje ya shule ni tofauti sana. Kuna kuzunguka na vyeti weeee na kazi hakuna, kuna kuombwa rushwa za pesa na ngono, kuna upungufu wa ajira zenyewe.
Lakini kama mfumo ungekuwa unakuandaa kujiajiri bila shaka kila mtu angekula mazao yake.
Fikiri zaidi kuhusu kujiajiri hata kama uko kwenye ajira, pamoja na kwamba haiwezekani wote tukajiajiri lakini wewe ambaye umebahatika kupata sumu ya kujiajiri basi fanya hivyo.

Msomeshe mwanao kwa kile anachokipenda, mtengenezee mazingira ya kujiajiri, kuwa mzalishaji wa bidhaa ili akimaliza masomo yake ajue anachofanya.
Kama unasoma, soma kwa kujiajiria na siyo kukalia vimbweta kwa kuamini kuwa unasoma ukaajiriwe.
Ninachoamini mabadiliko yanaanza na wewe muhusika kwa kujitambua kisha kufanya yale ambayo unahisi yanastahili kufanywa na wewe au mtu yeyote anayejitambua.
Acha kuifanya akili yako kuwa tegemezi, akili yako kuiegemeza kwenye kuajiriwa. Kwani huwezi kufanya japo jambo dogo la kujiajiria angalau kwa kufungua kibanda cha pipi, machungwa au genge kwa sababu tu una amini una tuzo unayostahili baada yakuhitimu chuo.
Hii siyo nchi ya hivyo, hata huko kwingine ambako unahisi kuna ajira kibao, si kweli, bali hata wao wanaangaika ila kwa kuwa mfumo wao wameufanya kujiajiri kwa mhusika na ndiyo maana leo hii tunatumia vifaa, huduma za wenzetu.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
      edit