Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI,
MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Friday, December 16, 2016
Thursday, December 15, 2016
Published 12/15/2016 11:00:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U'
Mkuu pole sana na kazi,
nafuatilia sana elimu na ushauri wako kuhusu mahusiano. Mimi ni mwanaume wa
miaka 48, nilianza maisha ya kujitegemea nikiwa na miaka 25, katika mishemishe
na maisha yangu yote hasa ya mapenzi sikubahatika kupata mke wa kweli.
Wengi wao walikuwa ni pasua
kichwa tu nilibahatika kupata watoto 2 kwa wanawake wawili tofauti. Mtoto wangu
wa kwanza anasoma kidato cha pili na wa pili anasoma darasa la pili, wote wako
kwa mama zao.
Naweza kusema kwa sasa mimi ni
mtu mzima kutokana na umri wangu (miaka 48)cha ajabu eti ndiyo anatokea kabisa
mwanamke wa ndoto zangu ina yeye ana miaka 32, ni mvumilivu, ananipenda, ana
bidi ya maisha n ahata mimi nampenda sana.
Dukuduku langu ni kuwa kwa mimi
kupishana na mchumba wangu miaka 16 huoni kama nitalaumiwa na jamii kuwa nimeoa
mtoto mdogo, lakini vipi kuhusu suala mapenzi hawezi kufika sehemu akaanza
ujanja ujanja kwa kuwa nitakuwa namzidi umri sana.
Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI,
MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Published 12/15/2016 02:00:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U'
Mimi ni mwanamke ambaye nimezaa watoto wawili na mwanaume mmoja lakini cha ajabu, mwanaume niliyezaa naye hatoi matumizi yoyote kwangu na hata kwa watoto wake, ni kama amenitelekeza, kila kitu nimekuwa nikiwahudumia mimi.
Imefika sehemu nimechoka kutokana na ugumu huu wa maisha nilio nao, wakati mwingine nawaza hata kuwatelekeza na mimi watoto wangu, lakini roho inaniuma sana jinsi ambavyo nimetesekana nao miezi 18 tumboni mwangu.
Naumia sana nikikumbuka namna ambavyo nilivyowazaa kwa uchungu, namba ushauri wako. Maisha kwangu yamekuwa kama gunia la misumari kwenye kichwa cha mtu mwenye kipara.
Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI,
MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Published 12/15/2016 02:00:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U'
Nilijitunza sana ili nisiuharibu mwili wangu kwa kurukaruka na wapenzi tofauti.
Niliamua kuishi bila mpenzi kwa muda mrefu sana lakini mwisho niligonga mwamba kwa kaka mmoja ambaye ni mwenyeji wa Arusha, mkazi wa Morogoro.
Ilichukua muda mrefu kumuamini na kumkabithi moyo na mwili wangu. Nilihakikisha najiridhisha kwa kila hatua ili nisije nikaangukia pua.
Nilimwambia naishi na mama pamoja na baba yangu wa kambo, tukiwa tunaishi kwenye kijumba chetu cha tope kwenye kijiji kimoja kilichopo mkoa wa Pwani.
"Kama kweli Maiko unanipenda basi njoo nyumbani japo ujitambulishe ishu ya mahari siyo tatizo, naweza kuongea na familia yangu wakatuelewa." Binti alimwambia Mpenzi wake.
Maiko aliniomba ajifIkirie kwanza kuhusu hilo, je nini kilifuatia baada ya Maiko kufikiria? Usikose sehemu inayofuatia ya mkasa huu kila Jumapili na Alhamisi saa 9 Alasiri.
Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI,
MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Subscribe to:
Posts (Atom)