Thursday, December 15, 2016

Published 12/15/2016 11:00:00 PM by

USHAURI WAKO NAOGOPA KUSEMWA KWA KUOA MWANAMKE NINAYEMZIDI MIAKA 16





Mkuu pole sana na kazi, nafuatilia sana elimu na ushauri wako kuhusu mahusiano. Mimi ni mwanaume wa miaka 48, nilianza maisha ya kujitegemea nikiwa na miaka 25, katika mishemishe na maisha yangu yote hasa ya mapenzi sikubahatika kupata mke wa kweli.

Wengi wao walikuwa ni pasua kichwa tu nilibahatika kupata watoto 2 kwa wanawake wawili tofauti. Mtoto wangu wa kwanza anasoma kidato cha pili na wa pili anasoma darasa la pili, wote wako kwa mama zao.

Naweza kusema kwa sasa mimi ni mtu mzima kutokana na umri wangu (miaka 48)cha ajabu eti ndiyo anatokea kabisa mwanamke wa ndoto zangu ina yeye ana miaka 32, ni mvumilivu, ananipenda, ana bidi ya maisha n ahata mimi nampenda sana.

Dukuduku langu ni kuwa kwa mimi kupishana na mchumba wangu miaka 16 huoni kama nitalaumiwa na jamii kuwa nimeoa mtoto mdogo, lakini vipi kuhusu suala mapenzi hawezi kufika sehemu akaanza ujanja ujanja kwa kuwa nitakuwa namzidi umri sana.


Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI, MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa



      edit