Thursday, February 15, 2018
Monday, February 12, 2018
Published 2/12/2018 01:32:00 AM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Nilipofika nikamkuta ana mtoto mchanga kabeba, akaniambia mshike huyu mtoto twende nyumbani nikaogopa, akanibembeleza nikamshika tukaondoka mpaka nyumbani. Akaniambia kuwa alioa mwanamke mwingine sasa wamegombana na yule mwanamke akamsusi mtoto, alichofanya ni kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na kupewa RB.
Nikaanza kumlea mtoto hadi akafikisha miaka 2 ndiyo mama yake akaja kumchukuwa mtoto wake, mume wangu akaenda kumchumbia mwanamke aliyezaa na kaka yangu akamuoa mimi nikasema sawa lakini nikamwambia kuwa siwezi kuishi naye, nilivyotoka kwa mume wangu.
Dada yangu mkubwa akawa amefariki dunia na kuacha watoto watano wakati huo mumewe naye alikuwa ameishafariki miaka 3 nyuma.
Mama yangu akachukuwa watoto wawili na mimi nikachukua watoto watatu.Nilirudi Dar, sina mume sina kazi wala biashara yoyote, ninaishi nyumba ya kupanga.
Niliamua kukopa mtaji, nikanza kuuza sokoni wakati huo nimepanga Chanika.
Pale sokoni akajitokeza shehe mmoja akasema anataka kunisaidia kulea watoto yatima ila anioe ili awe karibu na watoto nikakubali, nikaamini kuwa nimepata ndoa.
Tukafunga ndoa tarehe mwezi 8, mwaka 2016 akaniambia niache kufanya biashara nikae nihudumie watoto wangu tu.
Mwaka jana akasema tuhamia Mkoa wa Pwani ana mashamba mengi ili tukafanye kilimo, nikakubali lakini nilipofika akanitelekeza na watoto wangu.
Sina biashara waka pakushika, huku pia ni mgeni, nimewambia wazazi wake, sijapata msada wowote, nalala njaa na watoto.
Toka mwezi mwezi 8 mwaka jana hajaja wala hajanipa matumizi, nateseka sana na watoto, kiukweli napata shida sana kaka. Hiyo ndiyo historia ya maisha yangu.
Sina pakushika, nimekata tama kabisa na haya maisha, nawachukia sana wanaume kwani wamegeuza maisha yangu kuwa magumu.
Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot. com
Sunday, February 11, 2018
Published 2/11/2018 01:30:00 AM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Ilipofika Jumapili tukaenda Buguruni, nikamuomba yule mtoto wa dada nikae kwake, akakubal ikabidi nianze kuishi hapo, nikafuata nguo zangu, nikaanza kuishi naye.
Nikawa nafuta kazi yakufanya sikupata , kutokuwa na elimu nako kulifanya ikawa ni ngumu sana kupata kazi lakini sikukata tamaa ya maisha, nikaendelea kutafuta kazi.
Badala yakupata kazi nikapata mchumba mwingine aliyekuwa anaitwa Mudy, akanioa tukawa tunaishi Uwanja wa Ndege, nikapata mtoto wa kike tena, hapo ilikuwa ni mwaka 2008. Maisha yakaendelea nikiwa na mume wangu,
alinipenda nikampenda, tulipofikisha miaka 4 ya ndoa, mdogo wake na mume wangu wa kiume alikuwa anafanya kazi kwenye malori, alipata ajali akapasuka kichwa na akavunjika mguu, mkono.
Ndugu wakawa bize, kila mtu yupo bize na mambo yake ikabidi mimi nimuguze yule mgonjwa, akawa anajisaidia haja zote hapo hapo kwani hawezi kutembea wala kusimama, alipopona vidonda akapelekwa Kibaha kwa mtaalamu wa kuunga mifupa ya mguu na mkono bila kutumia dawa za hospitali.
Baada ya hapo alirudi nyumbani nikaendelea kumuuguza kwa muda wa mwaka mmoja na nusu akiwa ndani, alioanza kuchechemea akatafutiwa magongo kwa ajili ya kutembelea.
Siku moja nikiwa naumwa, nikaenda kwenye hospital ya Vingunguti, cha ajabu nikaambiwa hakuna huduma kwa sababu siku hiyo ilikuwa ni Siku ya Muungano, hakuna madokta, wakati naondoka mume wangu akanipigia simu niende kazini kwake, alikuwa anafanya kazi pale Sheli Buguruni.
Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot. com
Saturday, February 10, 2018
Published 2/10/2018 12:00:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Hakuna kitu kidogo ila kizuri kinachopendwa na wapenzi
hasa wa kike kama mpenzi, mchumba au mume wake kushinda nyumbani siku za
mapumziko, wanawake wanapenda sana wanapenda, kupita mbele ya wenza wao ili
wawaone walivyobarikiwa, wanapenda sana angalau kupata muda wa kuzungumzia
maendeleo ya familia yao japo kwa siku moja.
Kwa kufanya hivyo hakika nakuambia utakuwa umeongeza
umechachuza sehemu ya penzi lenu kulifanya lionekane angavu tena kwa mar
nyingine. Ebu jaribu, tena sio kujaribu badilika na anza kushinda nyumbani na
familia yako siku ya mapumziko hata watoto wanakuhitaji kama baba yao, hata
mifugo yenu kama ng’ombe nao wanafurahi wakikuona mara moja moja.
Sio kweli kwamba wanaume wote hawapendi kushinda nyumbani,
lah hasa wapo wengine wanapenda kabisa ila kutokana na tabia ya mwenza wake
inamfanya aamue kutokushinda nyumbani na kwenda kwa rafiki zake ama bar kula
masanga ili akirudi nyumbani muda wa marumbano na vijembe uwe angalau umepungua
kidogo.
Ushauri wangu angalia na rekebisha mapito yako, jiulize
nini ni kero au karaha yako inayomfanya mumeo, mchumba au mpenzi wako asishinde
nyumbani, au ni ile tabia yako ya kidomodomo, au ni ile gubu yako
Wakati mwingine mwenza wako anaamua kutokushinda ndani
kwasababu tu anajua akishindanawe ndani siku haitaisha bila kuzinguana, bila
kutukanana au kushikana singilendi na kadhalika.
Sio kweli kwamba wote wanakuwa na mambo yao wengine
wanakimbia kero kerom zenu. Ingawa pia kuna wengine wanatumia fursa hiyo kama
njia ya kuchepuka kwa maana ya kuondoa stesi za makelele yako.
Na wewe mwanaumea anza kurekebisha tabia zako pengine
ndizo zinamfanya mwenza wako aanza kukukulalamikia nahata kukwidana naye,
yawezekana wewe pia ndiyo sababu ndiyo chanzo. Kama utaweza kurekebisha suala
hilo utakuwa umitendea haki familia, mkeo, mpenzi na hata nyumba yako.
Mapenzi bhana umiza kichwa. Tukutane kwenye mada nyingine.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Subscribe to:
Posts (Atom)






















































