Ilipofika Jumapili tukaenda Buguruni, nikamuomba yule mtoto wa dada nikae kwake, akakubal ikabidi nianze kuishi hapo, nikafuata nguo zangu, nikaanza kuishi naye.
Nikawa nafuta kazi yakufanya sikupata , kutokuwa na elimu nako kulifanya ikawa ni ngumu sana kupata kazi lakini sikukata tamaa ya maisha, nikaendelea kutafuta kazi.
Badala yakupata kazi nikapata mchumba mwingine aliyekuwa anaitwa Mudy, akanioa tukawa tunaishi Uwanja wa Ndege, nikapata mtoto wa kike tena, hapo ilikuwa ni mwaka 2008. Maisha yakaendelea nikiwa na mume wangu,
alinipenda nikampenda, tulipofikisha miaka 4 ya ndoa, mdogo wake na mume wangu wa kiume alikuwa anafanya kazi kwenye malori, alipata ajali akapasuka kichwa na akavunjika mguu, mkono.
Ndugu wakawa bize, kila mtu yupo bize na mambo yake ikabidi mimi nimuguze yule mgonjwa, akawa anajisaidia haja zote hapo hapo kwani hawezi kutembea wala kusimama, alipopona vidonda akapelekwa Kibaha kwa mtaalamu wa kuunga mifupa ya mguu na mkono bila kutumia dawa za hospitali.
Baada ya hapo alirudi nyumbani nikaendelea kumuuguza kwa muda wa mwaka mmoja na nusu akiwa ndani, alioanza kuchechemea akatafutiwa magongo kwa ajili ya kutembelea.
Siku moja nikiwa naumwa, nikaenda kwenye hospital ya Vingunguti, cha ajabu nikaambiwa hakuna huduma kwa sababu siku hiyo ilikuwa ni Siku ya Muungano, hakuna madokta, wakati naondoka mume wangu akanipigia simu niende kazini kwake, alikuwa anafanya kazi pale Sheli Buguruni.
Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot. com
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.