Wednesday, April 26, 2017

Published 4/26/2017 09:24:00 AM by

MAGAZETI YA LEO APRIL 26, 2017

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
Read More
      edit

Tuesday, April 25, 2017

Published 4/25/2017 09:25:00 PM by

NAHISI MPENZI WANGU AMELOGWA.

Habari kaka G. Naomba ushauri nina mchumba ambaye tunaishi pamoja, huyu mpenzi ni Dr katika hospital binafsi jijini hapa, tangu mwaka jana tumeanza kuishi pamoja kwenye nyumba ambayo wazazi wangu walinipatia chumba kimoja kipindi nilipoanza kujitegemea. Siku za hivi karibuni mpenzi wangu huyo kapata majanga na kufukuzwa kazi, nikawa namsaidia Mimi ikiwemo kula na mambo mengine mengi, lakini sikumuacha sababu nampenda sana.Yafikia wiki ya pili sasa amebadilika sana kutwa nzima anashinda na hasira tu, pia nikimuuliza kilichomkasilisha ananitukana sana, ananiita Malaya wakati since i know him sijawahi kucheat na pia ananipiga pale nani ninapomjibu. Ananitukania mpaka ndugu zangu yaani nashindwa kuelewa nifanye nini ili mpenzi wangu arudi kwenye hali yake ya kawaida nahisi amelogwa......?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

Read More
      edit
Published 4/25/2017 09:11:00 AM by

MAGAZETI YA LEO APRIL 25, 2017

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
Read More
      edit

Monday, April 24, 2017

Published 4/24/2017 06:32:00 PM by

Upendo wa Kweli Haupo Kwenye Tendo Pekee

KWANZA kabisa, kwa moyo mkunjufu, shukurani zangu za dhati ziende kwa Mwenyezi Mungu ambaye amenipa nafasi hii adimu ya kuzungumza nawe tena msomaji wa safu hii nzuri ya XXLove inayokupa fursa ya kupata elimu juu ya uhusiano wa kimapenzi na maisha kwa jumla. Watu wengi wamekuwa na mtazamo kuwa, kutendo cha kuwa na mpenzi, mchumba, mke au mume basi ni kwa ajili ya tendo la ndoa pekee.
Utafiti unaonesha kuwa, hali hii ipo zaidi kwa vijana wa sasa ambao tendo la ndoa kwao limekuwa kama sehemu ya maisha yao.
Kila wanapokuwa wanawaza tendo hilo tu, hawana muda wa kujadili mambo mengine ya maendeleo zaidi ya mapenzi. Kibaya zaidi wanasahau kuwa mapenzi wanayoyapenda na kuyajadili muda wote yanahitaji kustawishwa kwa fedha, kwa maana ya kumtunza na kumpendezesha mpenzi wako.

Mada hii inazungumzia upendo wa kweli kwa wapenzi kuwa, haupo kwenye kufanya tendo la ndoa au kwa wanandoa bali upo kwenye mambo mengi sana kama vile;
KUHESHIMIANA
Kwa mtu anayempenda kwa dhati mpenzi au mwandani wake ni lazima atamheshimu, atamtunzia heshima yake popote aendako. Hata kama kuna watu wanamsema kwa mabaya ya kweli lakini yeye atajitahidi kutumia nguvu na ushawishi mwingi ili kumfichia ubaya mpenzi wake.
KUVUMILIANA
Changamoto za maisha kwa wapenzi huwa ni nyingi lakini kwa umpendaye, upendo wa kweli unanakshiwa na uvumilivu.
KUTHAMINIANA
Kuwa tayari kusikiliza shida za mwenza wako na kuzitatua hata kama huna uwezo wa kuzitatua, lakini kauli na maneno yako yanaonesha unaweza. Kauli ambazo zinamridhisha mpenzi wako na kumfanya aamini kuwa kuna siku utatimiza kile ulichokusudia kwake.

KUMPENDEZESHA
Kama kweli unampenda kwa dhati mpenzi wako ni lazima utahakikisha unampendezesha kwa kila namna ili kila siku aendelee kuonekana mzuri na bora machoni pako na kwa wengine.
KUELEWANA
Wenye mapenzi ya kweli muda mwingi huelewana, hata kama watatibuana lakini muda mchache tu wanaelewana na unakuta wanafanya kitu ambacho huwezi kuamini kama waligombana au kutukanana.
KULINDANA
Mpenzi unayempenda utamlinda kwa namna yoyote ile, hauko tayari kuona akionewa, akilia, akitukanwa, akipigwa na mambo mengine kama hayo. Unamlinda hata katika kujali afya yake. Lakini wapenzi wengi wa sasa wamegeuza mapenzi ndiyo kila kitu kwao, vitu vingine havina nafasi katika uhusiano zaidi ya mapenzi.
Ingawa tendo la ndoa ndiyo hasa kiunganishi kikubwa cha wapenzi, lakini mapenzi pekee hayatoshi kukamilisha upendo wa dhati kwa wapendanao.
Somo hili kama utalichukua kwa uzito wake basi utadumu na mpenzi wako kwa muda mrefu. Hata kama kipato cha mpenzi wako ni kidogo basi na wewe unayependwa unapaswa kuishi na kuendana na kipato chake.
Mpenzi msomaji, kwa ushauri na maoni, tembelea ukurasa wetu wa Gazeti la Ijumaa Wikienda kwenye Facebook, Insta:@mimi_na_uhusiano au jiunge na M&U WhatsApp kwa namba  +255 679 979 785

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

 CHANZO: GLP
Read More
      edit
Published 4/24/2017 12:08:00 PM by

KISA KUMPA PESA NUSU AKASILIKA.

Habari za mchana wana Me & U, ninaomba ushauri wenu ndugu zangu. Mimi ni mwanamke nina mpenzi wangu ambaye tuna mwaka moja ndani ya mahusiano yetu, tuna kawaida ya kusaidiana mambo mengi ikiwemo kupeana pesa mmoja wapo anapokuwa na tatizo.

Siku ya sikukuu ya pasaka aliniombakiasi cha sh. laki tatu nikamwambia nina laki mbili basi fasta nikamtumia. Kumbe mwenzangu alipoona ndogo alikasilika na kuniambia mi mchoyo, simpendi na maneno mengine mengi nikavumilia. Toka siku hiyo nisipomtafuta hawezi nitafuta na nikimtafuta ananijibu kwa dharau na kejeli. Sijui nifanyaje nami bado nampenda, nimejaribu kumuuliza nini nimemkosea hanijibu zaid anakata simu,mpaka sasa nipo njia panda.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
Read More
      edit
Published 4/24/2017 08:55:00 AM by

MAGAZETI YA LEO APRIL 24, 2017

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
Read More
      edit

Sunday, April 23, 2017

Published 4/23/2017 02:22:00 PM by

JINSI YA KUGEUZA KIPAJI CHAKO KUWA BIASHARA

Kila mmoja wetu ana vitu ambavyo anapendelea kuvifanya hata kama hakuna mtu anayemsifia au kumlipa. Anapata msukumo kutoka ndani yake kufanya au kufuatilia vitu fulani mpaka wengine wanamtumia kama ndiyo sehemu ya kujifunza au kupata msaada kuhusu kitu hiko. Kitu hiki ambacho mtu anapata msukumo mkubwa wa kukifanya au kukifuatilia ndiyo kipaji chake. Kinaweza kuwa kimoja au vinaweza kuwa vingi, inategemea na mtu mwenyewe.

Watu wengi wamekuwa hawavipi kipaumbele kikubwa vipaji vyao, huwa wanaona ni kama kitu ambacho kipo na hivyo hakuna anayeweza kukilipia. Lakini tumekuwa tunaona watu wachache wakinufaika na vipaji vyao. Watu kama wasanii, wachezaji na wanamuziki wamekuwa wanatumia vizuri vipaji ambavyo vipo ndani yao.
Je unawezaje na wewe kutumia vipaji vilivyopo ndani yako na kuvifanya kuwa biashara ambayo itakutengenezea kipato kikubwa?

Kwanza kabisa, kabla hata hatujaangalia jinsi ya kugeuza kipaji chako kuwa biashara, tukubaliane kitu kimoja, inawezekana kugeuza kipaji chochote kuwa biashara. Siyo tu kwenye sanaa na michezo, bali kitu chochote kile, ambacho kinaweza kuongeza thamani kwa wengine kwa kuwatatulia matatizo au kuwaletea furaha kinafaa kugeuzwa kuwa biashara. Iwe ni uandishi, uzungumzaji, uongozi, upangaji na mengine mengi, kuna namna unaweza kutumia kibiashara.

Yafuatayo ni mambo muhimu katika kugeuza kipaji chako kuwa biashara;

1. Jua kipaji au vipaji vyako ni nini.
Kwanza kabisa ni lazima ujue kipaji au vipaji vilivyopo ndani yako, hili ni zoezi ambalo unahitaji kulifanya wewe mwenyewe. Wewe unajijua kuliko mtu mwingine yeyote, hivyo angalia maisha yako tangu unakua mpaka sasa na angalia ni vitu gani unapenda sana kufuatilia au kufanya. Ukijitathmini kwa umakini utagundua kuna baadhi ya vitu unapendelea kuliko vitu vingine. Hapa usijihukumu kama unachopendelea ni kizuri au kinakubalika na wengine, unachohitaji ni kutambua kile kinachokusukuma, kinachoweza kukuamsha asubuhi ukiwa na hamasa na uhakika wa kwenda kufanya mabadiliko kwenye siku yako.

2. Jua thamani unayoweza kuongeza kwa wengine kupitia kipaji au vipaji vyako.
Biashara ni thamani, unalipwa kulingana na thamani unayotoa kwa wengine. Kadiri unavyotoa thamani kubwa ndivyo unavyopata mapato makubwa na ukitoa thamani ndogo utalipwa kidogo pia. Ukishajua vipaji vyako unachohitaji kujua ni thamani ipi unaweza kuitoa kwa wengine. Na hili pia ni zoezi rahisi kufanya kama utajitathmini maisha yako yote. Angalia ni vitu gani au maeneo gani ambayo watu wamekuwa wanakutegemea sana kwenye kipaji ulichonacho. Ukishayajua maeneo haya na kuona ni vitu gani ambavyo watu wanahitaji sana, unaweza kuboresha zaidi kile unachowapatia na kuanza kutoza gharama. Kama unachotoa ni bora, utapata watu wengi walio tayari kulipia.
Kwa mfano kama wewe unapenda sana kufuatilia mchezo fulani, na watu wakawa wanakuja kwako ili kusikia maoni yako kuhusu mchezo huo, tayari wewe una thamani ambayo wengine wanaihitaji. Unaweza kukusanya taarifa za kutosha kuhusu mchezo huo na kuziweka kwenye mfumo ambao unaweza kuwauzia wengine. Kipaji chochote, hata kama ni upishi, kuna namna nyingi ambazo unaweza kuzitumia na kuongeza thamani kubwa kwa wengine.

3. Usiogope kutoza gharama.
Tatizo kubwa sana kwenye kugeuza kipaji kuwa biashara huwa linaanzia hapa, watu wanaogopa sana kuwatoza watu wengine fedha. Wanaona kama wataonekana ni watu ambao wanajali zaidi fedha kuliko kuwasaidia wengine. Hii inakuwa hivyo kwa sababu hapo awali wengi walishazoea kupata kile unachotoa bure kabisa. Iwe ni kwa ushauri au msaada mwingine wowote, wengi wataanza kukujua kwa kuwa unafanya bure. Usikubali kupotezwa na hili, hakikisha unaandaa kitu chenye thamani bora na usiogope kuwatoza watu gharama. Kama kuna watakaokuambia kwa nini uweke gharama basi jua hao siyo muhimu na hawajali sana kwa kile unachotoa.
Hakuna dhambi kwenye kuwatoza watu gharama kama unawapatia thamani ambayo inafanya maisha yao kuwa bora zaidi. Unachohitaji kusimamia wewe ni thamani bora na inayowafanya watu kuwa na maisha bora.

Kama kila mmoja wetu angeweza kutumia kipaji chake kuwa sehemu kuu ya kipato chake, tungekuwa na jamii zenye furaha na watu wenye mafanikio. Hii ni kwa sababu biashara bora ni ile ambayo mtu anaipenda kutoaka moyoni, biashara hii inapotokana na kipato, mtu anaipenda sana. Hata kama tayari una biashara nyingine, hata kama kwa sasa umeajiriwa, fikiria vipaji vyako ni nini na anza kutoa thamani kwa wengine. Unaweza kuanza bure kwa mwanzoni ili watu wajue una nini, na baadaye ukaanza kuwatoza watu fedha kulingana na thamani unayotoa.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

Read More
      edit
Published 4/23/2017 11:12:00 AM by

MAGAZETI YA LEO APRIL 23, 2017

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
Read More
      edit

Saturday, April 22, 2017

Published 4/22/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-60

NILIPOISHIA…

Nilichojifunza G ni mwanaume ambaye hastahili kupewa nafasi ya kuzungumza kwani anajua sana namna ya kupangilia maneno kiasi kwamba ni ngumu sana kukataa au kutokuamini kile anachokueleza.

ENDELEA…
Nilikuwa naona mchungaji anatikisa tu kichwa kuashiria kuwa amekubaliana naye. Meneno ya mwisho niliyoyasikia kutoka kwa G ni:

“Mchungaji mimi nilifanya nilichostahili kumfanyia mdada huy, sina maslahi yane, nashukuru dada mtangazaji naye alifanya kile alichopaswa kufanya. Kilichobaki ni ninyi pia kutimiza kile ambacho Roho wa Mungu anawaaongoza, kuhusu kutudanganya, kutukana ua chochote kile tumuachie Mungu.”
G alimaliza zungumza na kumuachia mchungaji na viongozi wake, ambao walikubaliana kunipata ile pesa. Walitaka kukabidhi G lakini akawambia wanikabidhi mimi au dada mtangazaji ambaye ndiye hasa anayenilea mimi na mwanangu.

Nilimshukuru sana mchungaji na waumini wa kanisa lile, nikamshukuru sana dada mtangazaji na hata kaka G kwani yeye ndiye hasa aliyenipigania hadi nikafika pale.
 
Tuliondoka na kurudi nyumbani, ambapo dada mtangazaji yeye alienda kwenye mishe zake nikabaki mimi na G njiani tukiwa tunarudi nyumbani.

G aliendelea kunisistiza kuwa muungwa na mwenye hekima katika maisha yangu, pia nisifanya jambo la ajabu ambalo litanidhalilidha mimi na kumuachia lawama yeye kwa watu waliomuamini na kunipa msaada.

Nikimuahidi kuwa sitaweza kufanya hivyo. Nilichomoa shilingi 5000 na kumapa kaka G kama nauli lakini alikataa na kuniambia hizo mpesa si za kutumia matumizi ambayo hayajakusudiwa bali zinatakiwa zitumike kumsaidia mtoto anyooshwe mguu wake.

Niliagana na G akarudi kwenye kazia yake, nilifurahi sana siku hiyo kwani nilikuwa na uhakika wa mwanangu kesho kwenda kunyooshwa mguu wake.

Je, kesho yake alifanikiwa kwenda hospitalini kwa ajili ya kunyoosha mguuu wa mtoto wake?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

Read More
      edit
Published 4/22/2017 12:48:00 PM by

TUKIGOMBANA ANANIAMBIA NITAFUTE MWANAUME MWINGINE!

TUKIGOMBANA ANANIAMBIA NITAFUTE MWANAUME MWINGINE!
Ndugu zangu naombeni ushauri wenu, niko kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume fulani kwa mwaka mmoja sasa.
Mwanaume huyu anaonesha kila aina ya dalili kuwa ananipenda lakini ikitokea tu tukagombana basi ananiambia nitafuta mwanaume mwingine yaani anataka tuachane.
Nikijaribu kumuelewesha ananiambia mawazo yangu ni pumba kwa sababu amenipita miaka mitano hivyo ni mdogo sana siwezi kumuelekeza... Nisaidieni jaman niongee naye kwa lugha ipi? Au nifanye nini?