CHOMBEZO: TARATIBU SHEMEJI
ME&U
SEHEMU YA 1
Inawezekana umekata tamaa na huoni
mtu mwingine wa kumpa nafasi katika moyo wako kwa sababu tu umeishaumizwa na
kulizwa vya kutosha, umeishateseka sana kiasi ambacho umefika sehemu huoni
mwanaume au mwanamke mwingine ambaye unaweza kumpa moyo wako kwa kuamini kuwa
yawezekana na yeye ni wale wale waliozoea kuumiza.
Ama
kweli mapenzi fumbo la ajabu sana katika mafumbo yote yaliyowahi kutokea
duniani, fumbo ambalo kulifumbua kwake ni ngumu. Na kama ni janga basi janga
linalowaumiza vichwa walio wengi ndani na nje ya uhusiano, wasomi na wasio
wasomi, matajiri kwa masikini, wenye akili na wasio na akili, wastaarabu na hata
watukuti kwani wapo wanaotamani kuingia penzini huku wengine wakipigana kufa na
kupona kujinasua katika penzi hilohilo lakini nadhiri ikiwasuta na
kuwakatalia.Najua unaona hakuna mwingine wa kumpa moyo wako kwa sababu tu
uliyempa awali alikuumiza, alikutesa, alikuliza, alikusimanga, alikunyanyasa
kisa kikiwa ni mapenzi, penzi lake ambalo ulilithamini na kulipenda lakini bado
mwisho wa siku kimekuumiza vya kutosha.Yawezekana wewe ni mmoja wa wale ambao
nawazungumzia kwenye simulizi hii ambayo wameumizwa na hawana tena hamu na
mapenzi, hawako tayari kabisa kuwa na mpenzi kwa kuhofia hata huyo atakayempata
ni kama aliyewahi kumuumiza. Tapeli wa mapenzi kama yule ambaye alimwamini
lakini mwisho wa siku akamtapeli kwa kushindwa kujua thamani ya pendo lake kwake.Uliteseka
juu yake, ulimsaidia sana pale alipokwama, ulijitoa alipokuhitaji, ulimpenda na
kumfariji alipohitaji farijiko lako lakini leo hauko naye tena, aidha kwa
kukuacha, kumuacha au kuachana kwa sababu tu umechoshwa na vioja vyake.
Ulimpa
furaha alipokuwa na huzuni, ulisimama pembeni ya ubavu wake mliopoenda dukani
kukununua bidhaa, ulimshika kiunoni mwake mlipokuwa bichi lakini yote hayo ni
kama simulizi iliyowahi kutokea ilihali wewe ukitamani ingekuwa ni tamthilia
inayoendelea.Wewe ni mmoja wa wale ambao wamekuwa wakijiuliza kila siku kuhusu
kukosa mtu wa kumpa moyo wako, au umewahi kusikia rafiki, ndugu au jamaa yako akilalamika
au kusema maneno hayo basi kaa nae chini umwambie jinsi unavyojisia kuumia juu
yake kwa yale aliyofanyiwa.Haya twende sasa kushuudia kisa hiki cha kusisimua.
Jumapili moja baada ya kula chakula
cha usiku, baba mzazi wa kijana Ramadhani ambaye wengi walipenda kukatisha jina
lake na kumwita Rama au Ramso,akiwa ameketi sebuleni na kijana wake huyo
aliyehitimu kidato cha nne, alimweleza kwamba kwa wakati ule hakuwa na fedha za
kuweza kumuendeleza kielimu hivyo atafute kazi mjini ili kujikimu na maisha.Wakati
mzee huyo aliyepewa jina la utani la Kila, akimweleza hivyo, mkewe alikuwa
akimsikiliza ambapo alimuunga mkono mumewe kwani hali yao kiuchumi aliielewa
vizuri.
“Ramso, ni kweli kabisa kwa hivi
sasa baba yako hana fedha na unaona jinsi familia yetu ilivyo kubwa na wote
tunamtegemea yeye, mimi nakubaliana na ushauri wake wa wewe kutafuta kazi mjini au kufanya vibarua ambavyo vitakuwezesha
kupata riziki yako na yetu,” mama huyo alimwambia kijana wake.
Ramso kijana ambaye tangu udogo wake
ni handsome boy kiasi cha kuwavutia wasichana wengi wakiwemo watu wazima,
aliposikia kauli hiyo ya wazazi wake aliinamisha kichwa na kuanza kufikiria
hatima ya maisha yake ingekuwaje.
“Hivi baba, huwezi kuuza lile shamba
la mpiji magoe ili fedha zitakazopatikana niweze kuendelea na masomo nitimize
ndoto zangu za kuwa mhasibu?” Ramso alimuuliza baba yake.
Baba yake alimfahamisha kwamba baada
ya mambo yake kuanza kumwendea kombo, aliuza nusu ya shamba hilo na nusu
iliyobaki asingeweza kuiuza kwani alipanga iwasaidie wadogo zake ambao walikuwa
wadogo wakisoma.
Kwa kuwa Ramso alikuwa akielewa
ukubwa wa familia yao na jinsi mzazi wake alivyokuwa akihangaika kuitunza,
akawa hana jinsi zaidi ya kuingia mitaani kusaka kibarua chochote ambacho
kingemuwezesha kupata fedha.
“Okey baba na mama, kwa kuwa
naielewa hali halisi ya maisha yetu hapa nyumbani, nitazungumza na rafiki yangu
Chidy ili niongozane naye kwenye shughuli zake za kuuza mitumba,” Ramso
aliwaambia wazazi wake.
Alipotoa kauli hiyo, baba yake licha
ya kujiuliza moyoni kama kweli Ramso aliyemlea kimabavu angeweza kufanya kazi
ya kuuza mitumba lakini hakutaka kumuonesha wasiwasi wake, akamwambia sawa.
Baada ya mazungumzo hayo, Ramso
aliwaaga wazazi wake na kwenda kwenye chumba alichokuwa akilala na wadogo zake
wawili kilichokuwa uani, alikuwa mtu mwenye mawazo mengi sana akawa anatafakari
ugumu wa maisha uliokuwa ukiwakabili.
Chumbani kwa wazazi wake, baba na
mama yake walimjadili sana kijana wao kama angeweza kufanya kazi ya kuuza nguo
mnadani lakini baadaye walikubaliana wasubiri kuona matokeo.
Alfajiri na mapema kijana Ramso alikwenda
kumgongea rafiki yake chidy ambaye alikuwa akiuza mitumba buguruni aliyekuwa
akisifika sana kwa umahiri wake wa kumnadi mteja mpaka akanunua nguo kwa pesa
ndogo maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar kwa kazi yake hiyo.
“Niambie Ramso, naona leo umenivamia
alfajiri yote hii, umekwama nini?” Chidy aliyekuwa akimpa fedha Ramso siku moja
moja alipokwama alimwuliza.
“Ukiacha kukwama, leo nataka
tuongozane huko buguruni unakokwenda kuuza nguo japo nikakusaidie kazi yoyote
maana mtoto wa kiume kumtegemea baba kila kitu haipendezi,” Ramso alimwambia
chidy.
“Yaani Ramso na huo usharobaro wako
unataka kwenda kufanya kazi ya kutapanya maneno na kuwavuta wakina dada,
utaweza kweli?” Chidy alimwambia....ITAENDELEA
Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com
Kwa ushauri wa UHUSIANO na UJASIRIAMALI jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tufollow Insta@mimi_na_uhusiano, Facebook Page: Mimi na Uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.