Thursday, January 14, 2016

Published 1/14/2016 07:46:00 PM by with 0 comment

ILA KWELI AISEEE! AU?


Read More
      edit
Published 1/14/2016 07:42:00 PM by with 0 comment

MTUMBUA MAJIPU WA KITAA -2




WIKI iliyopita tuliishia pale Maliamu alipoambiwa na mama yake abadilishe nguo ili waende sehemu ambayo Maliamu hakufahamu ni wapi na anapelekwa kufanya nini.
Sasa songa nalo…

Maliamu alitangulizwa na mama yake kuelekea kwa akina Mery, njia yote waliyopita ilitawaliwa na kilio cha kwikwi na majonzi. Maliamu aliamini mama yake alimuonewa kwani ni kweli barua ile ilikuwa haimuhusu yeye bali rafiki yake kipenzi Mery na hiyo yote ilichangiwa na majina yao kuanza na herufi ‘M.’
Baada ya mama Maliamu na mwanaye kufika kwa akina Mery, mama Maliamu alianza kutukana kwa nguvu na sauti kubwa iliyojaa hasira ndani yake jambo lililomshangaza mama Mery.
“Kwani mama Maliamu kuna nini mwenzangu?” Aliuliza mama Mery.

“Mwambie mwanao akome kumfundisha mwanangu umalaya wake, tena haishie hapo hapo”
Mama Mery alibaki akishaanga asijue la kufanya! Kwani yeye na mama Maliamu ni maswahiba wa muda mrefu ingawa walikuwa anakaa mbalimbali kidogo.


Mama Mery aliamua kutumia busara na kumwambia mama Maliamu kwa upole. “Sasa shoga yangu mbona umekuja umepaniki hivyo, hayo ni mambo ya watoto, tukae chini tuzungumze.”

Maneno ya mama Mery yalipita polepole ndani ya masikio ya mama Maliamu na kuanza kushusha mapigo yake ya moyo yaliyokuwa juu zaidi.

Kama watoto wamekosea zungumza taratibu kwani hatugombani, nafikiri ni suala la kuongea na kuangalia namna gani tutalimaliza jambo hili, mama Mery alikuwa akimwambia mama Maliamu kwa unyenyekevu, kwani alijua kama na yeye angekuja juu kusingekuwa na maelewano zaidi ya malumbano na hata ugomvi ikiwezekana.
Walikaa chini wakahadithiana kile kilichotokea na mwisho mama Maliamu alimwambia shoga yake mama Mery kuwa suala hilo alilifikisha kwa kwangu (mwalimu Mtanange), walikubaliana wanapaswa kuwa makini sasa na watoto wao na kuhakikisha wanadhibiwa pia shuleni ili iwe fundisho.
Kwa upende wa mama Mery alichukia sana kitendo cha mwanaye Mery kumsababishia atukanwe kama mtoto tena mbele ya wapangaji wenzake, tena matusi makubwa makubwa na ya aibu, kitendo hicho
Kilimuuma sana, kwa hasira alizokuwa nazo aliachana na shughuli alizokuwa anazifanya na kuingia ndani akaketi kwenye kitanda akiwa na hasira na kuanza kuwaza kuhusu yale yaliyotokea. “Nakusubiri kwa hamu uje mwanahizaya mkubwa wewe, siwezi kudhalilishwa kwa sababu ya tabia yako chafu, mama Mery alijisemea mwenye.


Mery alirudi kutoka alikokuwa ameagizwa alipofika akakutana na kipigo cha hali ya juu sana kiasi kwamba akakuta analopoka hovyo.
“Mimi kila siku Kangasu ananitongoza hata hivyo sijamkubaliana, akiyanani mama nakwambia ukweli wa Mwenyezi Mungu,” alisema Mery uku akijiapiza shingoni.


“Humefanya uchafu weny mara ngapi?”
“Hapana mama sijawahi huwa ananilazimisha ila mimi nakataa.” Kutokana na kipigo sambamba na maswali ya mama yake, Mery alijikuta akiongea ukweli wote na kisha kumtaja kijana mwingine ambaye na yeye aliwahi kumtongoza.


Nini kilifuatia, usikose Jumanne ijayo

Read More
      edit

Monday, January 11, 2016

Published 1/11/2016 04:23:00 PM by with 0 comment

MWENZA WAKO KUTOSHINDA NYUMBANI NI TATIZO




Ni Jumatatu nyingine tunakutana wanajamvi wa XXLove katika kujifunza namna ya kukabiliana, kuzielewa na kuziishi changamoto mbalimbali tunazokutana nazo kwenye uhusiano, lengo likiwa ni kuboresha uhusiano huo na kuufanya uwe bora na wa kuigwa kwa mwaka huu wa 2016 na miaka mingine mingi tutakayojaliwa na Mwenyezi Mungu.

Wanawake wengi wamekuwa wakiwalalamikia wapenzi wao kutokushinda nyumbani hasa siku za mapumziko, binafsi ninaamini kutokushinda huko kwa wanaume majumbani mwao kunachangiwa na vitu vingi sana ambavyo vinaweza kuwa ni vidogovidogo ila vyenye kukwaza.






Hakuna kitu kidogo, ila kizuri kinachopendwa na wapenzi wengi, hasa wa kike kama mpenzi, mchumba au mume wake kushinda nyumbani siku za mapumziko, wanawake wanapenda sana ‘kupetiwapetiwa,‘ wanapenda kupita mbele ya wenza wao wakijitingisha walivyojaliwa ili wenza wao waone. Wanapenda kupata muda wa kuzungumza na wenza wao kuhusu maendeleo ya familia yao japo kwa wiki mara moja na kuendelea.

Tatizo linaloonekana ni kwamba wanaume wengi huwa hawako tayari kubaki nyumbani kwa muda mrefu, siku ya/za mapumziko kwa kuhofia malumbano ya hapa na pale.


Wengine ni kwa sababu ya tabia za mwenza wake (wewe mwanamke), anaamini kwa jinsi ulivyo akisema ashinde tu ndani basi siku haiwezi kuisha bila kushikana shati au kutukanana, hivyo anaona bora kwenda zake kwa washkaji au baa kula masanga ili akirudi nyumbani muda wa migongoro na malumbano uwe angalau umepungua kidogo.


Ushauri wangu, angalia na rekebisha mapito yako, jiulize ni nini? Tabia ipi? kero au karaha zipi kwa mwenza wako zinazomfanya asishinde nyumbani au pengine ni tabia yako ya kidomodomo, gubu au kisirani?
Ukiweza kujua vyanzo vinavyomfanya mwenza wako asishinde nyumbani, itakuwa ni vizuri sana na kama utavifanyia kazi basi naamini mapenzi yako kwa mwaka 2016 yatakuwa matamu mno na yenye furaha.

Ingawa siyo wote wanakimbia kero za wenza wao, wanaume wengine ndiyo wanapopatia sababu ya kufanya mambo yao kama kula masanga, kukutana na marafiki, kufanya dili zao za nje ya ofisi na hata kuchepuka kwa wenye tabia hiyo.

Hebu fanya mwaka 2016 kuwa wa neema kwako, kama ni mwanamke jirekebishe, nawe mwanaume badilisha baadhi ya tabia zako, pengine ndizo chanzo kikubwa cha malumbano yenu yanayosababisha ninyi kukwidana, kutengana nakadhalika.

Kwa kuzingatia na kuufanyia kazi upungufu wenu ni hakika mtakuwa kama mnalipevusha upya penzi lenu, mwanamke badilisha vijitabia vyako vya ajabu, mwanaume pia fanya utaratibu wa kupumzika nyumbani siku ya mapumziko, watoto, mwenza wako wanakuhitaji, hata mifugo yako kama ng’ombe na mbwa nayo inakuhitaji ndiyo maana siku ukitaka kuipa chakula huwa inafurahi sana kwa sababu inahitaji uwepo wako.

Mpenzi msomaji kama umewahi kukumbana na tatizo nililolieleza hapo juu, tafadhali tuma maoni yako na yatatoka wiki ijayo kwenye kona hii. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook, Instagram na kundi la WhatsApp kujua mengi kuhusu mapenzi.
Read More
      edit

Wednesday, January 6, 2016

Published 1/06/2016 03:57:00 PM by with 0 comment

NAHISI KAMA NINA MKOSI WA MAPENZI


Mimi ni msichana mzuri mwenye miaka 23, najikubali kwa figa nzuri niliyojaliwa na Mungu, kwa kifupi ni msichana mrembo kabisa, kama ungepata nafasi ya kukutana na mimi ungekubaliana dhahiri na maneno nayoyesa. Tatizo langu  sijui ni nini ? Mpaka sasa nimekwisha achwa  na wanaume 4 tofauti. Najaribu Kujiuliza nini kasoro yangu? au NINA NUKSI? naomba ushauri wako WANAM&U
Usikose kutembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Na Thimothe Mjuni:M&U
Read More
      edit

Tuesday, January 5, 2016

Published 1/05/2016 10:35:00 PM by with 0 comment

KIBULI CHA MAPENZI



Ungekuwa wewe ndiyo huyo polisi ungekapa adhabu gani  haka kajamaa kanakokuharibia  binti yako?
Read More
      edit
Published 1/05/2016 12:08:00 PM by with 0 comment

CHOMBEZO: MTUMBUA MAJIPU WA KITAA



“Walimu leo ni siku ya Skuli Baraza, nina wanafunzi wawili nimepokea malalamiko yao na ninataka niwatumbue mbele ya wanafunzi wote na ninyi walimu  ili kukemea kabisa tabia zao chafu waliozianzisha hapa shuleni,” Mwalimu mkuu msaidizi, Dustan Mtanange wa Shule ya Msingi Kilima, wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga alikuwa akiwaeleza walimu wenzake ofisini.

Mara tu baada ya yeye kupata taarifa za msichana Maliamu kukutwa na barua yenye ujumbe wa mzito wa mapenzi ambao alidai ametumiwa mwanafunzi mwenzake wa kiume aliyejulikana kwa jina la Kangasu.
‘’ Nikiwa naenda zangu kunywa chai, mara nasikia sauti ya kitoto ikiniita ‘mwalimu, mwalimu’ ile nageuka hivi namuona mtoto ananikimbilia aliponikaribia akaniambia mama Maliamu anakuita, nilimweleza akamwambie nitapita nikiwa narudi. 

“Kweli nilipita na kumkuta mama yule kapandwa na jazba na kudaia sisi walimu hatutimizi majukumu yetu kwa kuwaangalia wanafunzi wawapo shuleni, kwani amekutana na barua chumbani kwa mwanaye ikiwa imewekwa kwenye bahasha nzuri ya maua na kwa juu imeandikwa kwa mwandiko mzuri sana maneno yanayosomeka ‘Kwako M,’ akimaanisha Kwako Maliamu.’ 

Na hata  alipoifungua  kuisoma alikutana na ujumbe mzito, mzuri mtamu sana wa kimapenzi uliomshangaza kwani ulionekana kuandikwa na mwanaume mwenye kumzidi umri Maliamu lakini pia ni mzoefu wa mambo hayo.
Kitendo cha kuisoma barua ile kilimuumiza sana mama yule na kuamua kumsubiri kwa hamu mwanaye atoke shule ili amuhoji.
Ilikuwa ni majira ya 10 jioni ambapo Maliamu alirudi kutoka shule na kuingia ndani kama kawaida hupenda kujitupa katika kitanda chake cha chuma chenye godoro la pamba lililotengenezwa na fundi mmoja maarufu sana wilayani hapo.

Ghafla alisikia mlango ukisukumwa kwa nguvu sana na kumfanya ashituke.
“Hivi Maliamu siku hizi umekuwa si ndiyo?” Mama yake aliuliza.
“Kwani mama, mimi nimefanyaje!?
Mama alimjibu “Hujui ulichokifanya, si ndiyo, haya niambie haraka sana hii barua imetoka kwa nani?” 
Mama aliuliza huku akiitoa barua ile aliyokuwa ameificha kwa nyumba kisha alimuonesha Maliamu. “Nataka uniambie haraka sana, nani kakutumia hii barua ya ujingaujinga, umeanza michezo ya ajabu si ndiyo.”
Maliamu aling’ata vidole vyake na kupindisha shingo upande wa kushoto, hamna mama sio ya…
Sio yako si mbona imeandikwa Kifupi cha jina lako ‘M’
Kweli mama sio yangu ni ya … kabla hajamaliza tena kujibu fyaaaa! Akapata kiboko cha begani, ile anajishika akachapwa kingine, ajakaa sawa akaanza kuchapwa viboko vingivingi.
“Hiiii hiii hiiiii! Mama unanionea barua hiyo kanipa Kangasu nimpelekee Mery sio yangu mama, mama sio yangu, kweli mama nakwambia sio yangu,” Maliamu alilia kwa uchungu sana.

Mama Maliamu baada ya kusikia maneo yale kidogo yaliingia akilini mwake na kuacha kuendelea kumchapa kisha akashika kiunoni mkono mmoja haya niambie “Mery gani, huyu rafiki yako.
“Ndiyo mama.’’
‘’Wewe ndiyo umekuwa mshenga si ndiyo?’’
‘’Hapana mama, mimi kangasu alinipa tu akasema nimpe Mery hata sijaisoa.’’
Haja badilisha haraka hizo nguo zako za shule twende huko, fanya haraka, pumbavu sana wewe, mama  Maliamu alisema kwa jazba huku kifua chake kikipanda na kushuka kwa hasira.
Je, mama Maliamu anataka kumpeleka wapi mwanaye? Usikose Jumanne ijayo sehemu inayofuatia.
Read More
      edit
Published 1/05/2016 06:51:00 AM by with 0 comment

MAUMIVU YA SIRI



 USIBISHE TU! Mbona kama kuna ukweli hivi, au wewe unasemaje?
Read More
      edit
Published 1/05/2016 06:48:00 AM by with 0 comment

UNATAFUTA MCHUMBA, USICHOKE KUOMBA



MUNGU ANAJIBU; Nimekuwa nikiomba mara kwa mara ili nipate mpenzi atakayenifaa, nimeomba sana na mwisho nilianza kukata tamaa kuwa siwezi kuolewa/ kuoa mwanamke ninayempenda na yeye kunipenda lakini  leo Mungu ametenda miujiza kwangu ni baada ya kunionesha mpenzi mwema.ASANTE MUNGU KWA WEMA WAKO.
Read More
      edit
Published 1/05/2016 06:43:00 AM by with 0 comment

MWANZO WA MAPENZI

HAYA ndiyo mapenzi, hakika mapenzi hayachagui elimu, hulka, rangi, dini kabila, aina na kadhalika kama picha inavyojieleza.
Read More
      edit
Published 1/05/2016 06:38:00 AM by with 0 comment

MWAKA 2016, MALKIA/ MFALME WANGU NI WEWE





 Msanii Kala Jeremiah akiwa na Malkia wake



Nina kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuuona Mwaka 2016, ikiwa ni siku ya nne tangu mwaka huu mpya uanze.

Wapo waliotamani kuuona lakini imeshindikana kwa mapenzi ya Mungu, wapo waliouona wakiwa na majanga tele, wengine wakiwa wamelazwa, wengine wakiwa ni walemavu kwa sababu mbalimbali.
Safu hii pendwa ya XXLove iko nawe bega kwa bega kwa shida na raha bila kujali kilichokufika, tunaamini sote tu waja wa Mungu.

Mada ya leo inazungumzia zaidi kuhusu wapenzi waliogombana, waliotengana, walioumizwa, kuachwa na kadhalika, kuuanza Mwaka 2016 kwa kufikia na kuwaza mazuri.
Msogelee mwenzio kwa karibu kama uko naye, mtumie SMS au mpigie simu na umwabie ‘mwaka 2016, malkia/mfalme wangu ni wewe’, inawezekana mliishi na mwenzako, yaani mchumba, mumeo, mkeo au wapenzi kwa bifu zito, kwa kununiana, kutukanana, kupigana, kusalitiana na mengineyo.

Sasa mwaka mpya umeanza, sema basi, nahitaji kutengeneza na kuanza uhusiano wagu upya. Ahidi familia, ndoa, uhusiano au mapenzi yako kuwa bora na ya kuigwa kwa Mwaka 2016. Achana na yote uliyotendewa na mpenzi wako, mumeo, mkeo, rafiki, ndugu na kadhalika, sasa songa mbele.


Naamini utakuwa unaukumbuka msemo huu; mwaka mpya na mambo mpya, basi msogelee mpenzi wako huko aliko na umwambie kuwa yeye ndiye malkia au mfalme wa moyo wako.
Mwambie mpenzi wako, mumy, baby nakupenda, napenda umbo lako, sura, rangi, nywele, macho, midomo na tabasamu lako.

Wewe ndiye faraja ya moyo wangu, wewe ndiye tiba ya maradhi yangu sugu yanayonisumbua, wewe ndiye mchumba, mpenzi, mke au mume bora.

Hakika kwangu wewe ni malkia, wewe ni mfalme katika ulimwengu wangu wa mahaba, kwako nimetulia.
Sina maua, sina kadi, sina fedha, nyumba wala gari, zaidi ya upendo na kukuthamini siku zote za maisha yangu.Wengi walisubiri tuachane tangu mwaka jana, kuna wakati tunakwazana, tunagombana na kadhalika lakini mwaka huu naomba tumalize tofauti zetu.

Pamoja na maumivu ya kuumizwa, basi nami najipa tumaini jipya la kumpata yule atakayenipenda kwa dhati mwenye penzi la kweli.Dunia ina watu na viatu, wapo waliosambaza umbeya kutugombanisha lakini wameshindwa, wewe ni yuleyule, michepuko tupa kule.

Tukutane wiki ijayo kwenye mada nyingine nzuri na tamu. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram kujua mengi kuhusu mapenzi.

Read More
      edit