Thursday, February 2, 2017

Published 2/02/2017 06:37:00 AM by

MAGAZETI LEO, FEB 2, 2017

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na.M&U
Read More
      edit

Wednesday, February 1, 2017

Published 2/01/2017 04:00:00 PM by

BADILI MATATIZO KUWA MAFANIKIO!

Kwa mjasiriamali yeyote mwenye kujua mbinu na siri za mafanikio ni lazima anajua namna ya kutumia fursa ipasavyo. Anajua namna ya kubadili matatizo yanayomzunguka kuwa mafanikio makubwa kwenye maisha yake.

Hakuna sababu ya kushangaa, huo ndiyo ukweli. Kutokana na matatizo yanayokuzunguka au kuizunguka jamii yako, unaweza kutumia fursa hiyo kutengeneza ajira, kama ulikuwa hujui basi hilo liweke akilini mwako.
Unawezaje kubadili matatizo

Jaribu kujiuliza jamii yako inakumbwa na matatizo gani, inakabiliwa na changamoto zipi? Inawezekana moja ya tatizo lililopo ni upatikanaji wa maji safi, pengine watu wanafuata maji hayo umbali mrefu na wanachukua muda mrefu katika kutafuta huduma hiyo muhimu.
Kama wewe ni mjasiriamali, basi tumia tatizo hilo kuchimba kisima cha maji, kwa kufanya hivyo utakuwa umebadilisha tatizo linalowakabili wanakijiji. Zipo faida kadhaa ambazo utazipata. Kwanza, utakuwa umeihudumia jamii yako kwa maana ya kupata huduma ya maji kwa wepesi na muda muafaka.

 Pili, wewe kama mtoa huduma, utapata fedha ambazo zitasaidia katika kuboresha maisha yako kwa jumla.
Hakikisha kuwa wakati ukifanya hivyo kusiwe na mtu wa kukukatisha tamaa. Kwa kufanya hivyo utakuwa umeinusuru jamii yako inayokuzunguka kutumia muda mrefu katika kutafuta huduma ya maji lakini pia kuepukana na magonjwa yatokanayo na maji kutokuwa safi.
Ninachoamini, kila jamii ina changamoto zake. Anza sasa kufanya utafiti kuhusu mazingira yanayokuzunguka kwa kubaini matatizo na changamoto zililizopo kisha anza kufikiria ni namna gani unaweza kubadili tatizo hilo kuwa mafanikio. Ili kufanya vizuri ni lazima uangalie ni matatizo yapi unayoyaweza? Kuligana na uwezo wako na mazingira uliyopo.

Jipime kwa kuanza na tatizo dogo, huku ukiweka nia ya dhati ya kulitatua tatizo hilo kwa mtazamo wa kuisaidia jamii na wewe kujipatia kipato.

Hakikisha unafanikiwa katika kutatua tatizo hilo dogo, ili upate fursa na kutafuta lililokubwa zaidi. Duniani kote wajasiriamali huwa ni watu wenye kutumia fursa za matatizo na kubadilisha kuwa mafanikio.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U

Read More
      edit
Published 2/01/2017 02:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-26

Mwezi wa pili ulikatika nikiwa Kwa Mfipa lakini akili yangu kubwa ikiwa kwenye mguu wa mtoto wangu, nilitamani sana mtoto wangu apone mguu wake. Niatafanyaje sasa. Kwa kawaida pale nyumbani kuna kiredio kidogo ambacho huwa tunasikiliza, sasa siku hiyo nikawa nimeweka moja ya kipindi cha kinachohusu mambo ya mikasa ya mapenzi.

Nilimsikiliza sana mtangazaji kwa makini sana wakati akitambulisha  mkasa wa binti ambaye alitoroka kwao kwa sababu alitakiwa kuozeshwa kwa nguvu na baba yake,  na mbaya zaidi mwanaume ambaye alitakiwa kumuoa anamzidi umri hata baba yake mzazi na alikuwa anaolewa mke wa pili wakat huo binti alikuwa na miaka 17.

Yule mtangazaji baada ya kumaliza kipindi alitaja namba hivyo nikaona nichukue kwa sababu alisema kama kuna wasikilizaji watakuwa wanataka kutoa mikasa na hata wale wa kuwasaidia wahanga wa mikasa ile, niliona ni vyema na mimi nikiwa nayo ile namba kwa dharura.
 
 Baadaye nilijiuliza hivi kweli nikajitangaze kwa watu wanisikilize, si hata wa kijijini kweu na wao watasikia, sikuwa na namna maji yalikuwa yamenifika shingoni, nilichofanya baada ya wiki moja kupita nilimtafuta mtangazaji huyo na kumuelezea kile nilichokuwa nahitaji.

Nilimwambia mimi hitaji langu kubwa ni mwanangu kunyooshwa tu mguu wake hichi ndicho ambacho nilikuwa naomba. Yule mtangazaji akaniamba nipe dakika mbili nitakwambia. Baada ya muda akanitumia namba 0657486745 na kuniambia kuwa wasiliana na huyo mtu atakusaidia na nimeisha wasiliana naye, nilifurahi sana kwani niliamini tatizo la mwanangu kuwa na ulemavu limetatulika.
 
Nilianza kuisumbua ile namba kwa kubipu mata tafadhali nipigie nika mat ambaye amekutana na zali sasa anaona ni kama linachelewa, ilipofika jioni majira ya saa 12   jioni ile namba ilinipigia nikajikuta nashusha pumzi ndefu kidogo. 

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta@:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U

Read More
      edit
Published 2/01/2017 12:00:00 PM by

HAMTAKI MTOTO WANGU!

Mimi ni binti wa miaka 20 nilipata ujauzito nikiwa shuleni na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike, baada ya muda nilipata mtu wa kunioa, nikamueleza ukweli kuwa nina mtoto akakubali na akaenda nyumbani kwetu kujitambulisha cha ajabu kwa sasa anamchukia mtoto wangu.

Anadai kuwa hawezi kulea mtoto wa mwanaume mwenzake, wakati baba yake yupo, imegeuka masimango katika ndoa yangu, siwezi kumtupa wala kumpelekea mtu mwingine anilele mtoto wangu.
Ungekuwa ni wewe ungefanyaje? Naomba ushauri wako.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
Read More
      edit
Published 2/01/2017 07:14:00 AM by

MAGAZETI LEO, FEB MOSI, 2017