Kwa mjasiriamali yeyote
mwenye kujua mbinu na siri za mafanikio ni lazima anajua namna ya kutumia fursa
ipasavyo. Anajua namna ya kubadili matatizo yanayomzunguka kuwa mafanikio
makubwa kwenye maisha yake.
Hakuna sababu ya kushangaa,
huo ndiyo ukweli. Kutokana na matatizo yanayokuzunguka au kuizunguka jamii yako,
unaweza kutumia fursa hiyo kutengeneza ajira, kama ulikuwa hujui basi hilo liweke
akilini mwako.
Unawezaje kubadili matatizo
Jaribu kujiuliza jamii
yako inakumbwa na matatizo gani, inakabiliwa na changamoto zipi? Inawezekana
moja ya tatizo lililopo ni upatikanaji wa maji safi, pengine watu wanafuata
maji hayo umbali mrefu na wanachukua muda mrefu katika kutafuta huduma hiyo
muhimu.
Kama wewe ni mjasiriamali,
basi tumia tatizo hilo kuchimba kisima cha maji, kwa kufanya hivyo utakuwa
umebadilisha tatizo linalowakabili wanakijiji. Zipo faida kadhaa ambazo
utazipata. Kwanza, utakuwa umeihudumia jamii yako kwa maana ya kupata huduma ya
maji kwa wepesi na muda muafaka.
Pili, wewe kama mtoa huduma, utapata fedha ambazo
zitasaidia katika kuboresha maisha yako kwa jumla.
Hakikisha kuwa wakati
ukifanya hivyo kusiwe na mtu wa kukukatisha tamaa. Kwa kufanya hivyo utakuwa
umeinusuru jamii yako inayokuzunguka kutumia muda mrefu katika kutafuta huduma
ya maji lakini pia kuepukana na magonjwa yatokanayo na maji kutokuwa safi.
Ninachoamini, kila jamii
ina changamoto zake. Anza sasa kufanya utafiti kuhusu mazingira yanayokuzunguka
kwa kubaini matatizo na changamoto zililizopo kisha anza kufikiria ni namna gani
unaweza kubadili tatizo hilo kuwa mafanikio. Ili kufanya vizuri ni lazima
uangalie ni matatizo yapi unayoyaweza? Kuligana na uwezo wako na mazingira
uliyopo.
Jipime kwa kuanza na
tatizo dogo, huku ukiweka nia ya dhati ya kulitatua tatizo hilo kwa mtazamo wa
kuisaidia jamii na wewe kujipatia kipato.
Hakikisha unafanikiwa
katika kutatua tatizo hilo dogo, ili upate fursa na kutafuta lililokubwa zaidi.
Duniani kote wajasiriamali huwa ni watu wenye kutumia fursa za matatizo na kubadilisha
kuwa mafanikio.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U