Saturday, April 1, 2017

Published 4/01/2017 02:00:00 PM by

MASHETANI YA ZIMAYA





Ni simulizi nzuri inayomhusu msichana mdogo anayeitwa Matrida, ambaye alipoteza wazazi wake wote wawili, jambo lililopelekea kuanza kuishi katika mazingira magumu. Maisha aliyoanza kuishi hakuwahi kuyafikiria kabla kwenye akili yake kama kuna siku atakuja kuishi maisha hayo.

Matrida alianza kuishi maisha ya shida sana tofauti na alivyokuwa akiishi na wazazi wake enzi za uhai wao. Kutokana na ugumu wa maisha aliyokuwa anayapitia msichana Matrida alianza kushawishika kwa kutafuta namna ya kuweza kuishi maisha ya furaha kama zamani kiasi cha kufikia hatua ya kushawishika kuabudu MASHETANI ya ZIMAYA.

Ni maswahibu gani yaliyomkuta Matrida tangu alivyo jiunga na MASHETANI YA ZIMAYA basi endelea kufuatilia hadithi hii nzuri na yenye mafunzo makubwa katika maisha yako nay a watoto wako ambao pengine unaweza kuwaacha duniani.

Ilikua ni siku mpya kwa upande wa Matrida, asubuhi na mapema baada ya kuamka mnamo majira ya saa 12:03 alfajiri alifungua mlango nakutoka chumbani kwake kuelekea sebuleni, wakati huohuo baba na mama yake wakiwa usingizini.

Ni kawaida ya Matrida kuwahi kuamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kuanza kufanya usafi wa nje pia kuwasha jiko ili kuandaa kinywa cha siku hiyo kabla ya kuanza kufanya usafi wa ndani.

Ilipofika saa 12:30, Matrida alimaliza usafi wake wa nje na kubakiwa na usafi wa ndani, wakati akijiandaa kuingia ndani, akiwa bado yupo mlangoni amekaa kutokana na uchovu wa kazi ya siku hiyo aliyokuwa amefanya, akiwa anaendelea kufikiria kufanya kazi iliyobaki lakini pale alipokaa kama hatua tatu hivi kuna kitu alikiona mbele yake.

Je, Matrida aliona kitu gani mbele yake na nini kilifuatia? Usikose Jumanne ijayo.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

Read More
      edit
Published 4/01/2017 12:00:00 PM by

MPENZI WAKO KASEMA NI BIKRA KUMBE SI KWELI, UNAFANYAJE?




Mimi ni binti mwenye miaka 21 ninaishi, Tabora, nina  mpenzi wangu ambaye tuna miaka 3 kwa sasa ila hatujawahi kufanya kukutana kimwili.

Kabla hatujaanza uhusiano wetu aliniuliza kama mimi bado niko bikra au ilishatoka, kwa kuwa sikujua kama tutafika hapa tulipofika nilimdanganya kuwa niko bikra

Muda ukapita na tukaendelea kuwa wapenzi hata nyumbani wazazi wangu wanamfahamu vizuri na mimi pia ninajulikana kwao.
Ila kuna siku mpenzi wangu aliniambia kuwa siku akijakugundua kuwa sina bikra na nilimdanganya basi hatoniamini tena maishani mwangu.

Kiukweli hasi sasa hivi ni kama akili yangu imepooza kwani sina bikra nilidanganya kwa kujua ni mpita njia tu. Nampenda sana mpenzi wangu, sijui naanzia wapi kumwambia, tafadhali naomba ushauri wako najua nilifanya kosa.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

Na.M&U
Read More
      edit
Published 4/01/2017 09:53:00 AM by

NAMNA YA KUONDOA HOFU-2




Jana niliishia pale nilipozungumzia mtu kuwa na hofu ya kuhisi kuwa huwezi kufanya jambo fulani kwa sababu wewe ni mdogo, huna pesa, huna elimu, huna ndugu wala jamaa eneo ulilopo, kwenye ukoo wenu hamna mtu mwenye histori ya kufanya jambo kama hilo.


Tuendelee na sehemu ya pili ya mada yetu
Inayohusu namna ya kuondoa au kutoa hofu, kabla ya kujifunza kuondoa hofu nimejaribu kukupitisha kwenye  baadhi ya aina za hofu ili kuweza kujua mantiki ya kile ambacho tunajifunza.


Hii ni hofu ya kipuuzi ambayo kama usipoangalia itakutafuna wewe na kizazi chako kijacho.

HOFU YA KUSHINDWA 

Hofu hii aiko mbali sana na ile ya kutengenezwa kwani unavyotengenezewa hofu au unavyojitengenezea hofu basi hata kwenye kufanya maamuzi ya jambo fulani wewe unakuwa na hofu ya kushindwa. Yaani unaona ni heri kubaki na shilingi 20000 uliyonayo chini yam to kuliko kuanzisha biashara ya maembe kwa kuamini kuwa unaweza kukosa wateja na mwisho wa siku maembe yakaoza. Na mtaji ukakatika papo kwa papo.



Ndugu yangu, watu wote duniani ambao unawaona, unawasikia na kuwasoma au kuhadithiwa kuwa wana mafanikio, hawakuzaliwa na hayo mafanikio bali waliyapata hapa hapa chini ya jua kwenye nchi ambayo wewe pia unaishi, kwenye mtaa ambao nawe unakaa.

 Kilichotokea kwao ni kukubali kujifunza kwa kukubali kushindwa mara kwa mara , naposema kushindwa namaanisha kuishindwa kwa fakti au kushindwa kwa sababu maalumu siyo kushindwa kwa uzembe.

UNAPOSHINDWA mara ya kwanza utakuwa umejifunza ni kwa nini umeshindwa hivyo awamu ya pili huwezi kushindwa na kama utashindwa basi utashindwa kwa sababu na kwa njia nyingine.


Ila kadri unavyozidi kushindwa mara nyingi ndivyo hivyo unavyozidi kuyakaribia mafanikio au kuufikia ushindi kwa sababu madhaifu, matatizo, changamoto zote za kushindwa unazifahamu hivyo hubabaiki na jambo lolote wala hakuna changamoto mpya ambayo itakufuata utashindwa kuitatua na kama ukishindwa basi hiyo hiko juu ya uwezo wako kabisa na hata uwezo wa kibinadamu.


 Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
Read More
      edit
Published 4/01/2017 07:54:00 AM by

Magazeti leo, April 1, 2017


























Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
Read More
      edit