Saturday, April 1, 2017

Published 4/01/2017 02:00:00 PM by

MASHETANI YA ZIMAYA





Ni simulizi nzuri inayomhusu msichana mdogo anayeitwa Matrida, ambaye alipoteza wazazi wake wote wawili, jambo lililopelekea kuanza kuishi katika mazingira magumu. Maisha aliyoanza kuishi hakuwahi kuyafikiria kabla kwenye akili yake kama kuna siku atakuja kuishi maisha hayo.

Matrida alianza kuishi maisha ya shida sana tofauti na alivyokuwa akiishi na wazazi wake enzi za uhai wao. Kutokana na ugumu wa maisha aliyokuwa anayapitia msichana Matrida alianza kushawishika kwa kutafuta namna ya kuweza kuishi maisha ya furaha kama zamani kiasi cha kufikia hatua ya kushawishika kuabudu MASHETANI ya ZIMAYA.

Ni maswahibu gani yaliyomkuta Matrida tangu alivyo jiunga na MASHETANI YA ZIMAYA basi endelea kufuatilia hadithi hii nzuri na yenye mafunzo makubwa katika maisha yako nay a watoto wako ambao pengine unaweza kuwaacha duniani.

Ilikua ni siku mpya kwa upande wa Matrida, asubuhi na mapema baada ya kuamka mnamo majira ya saa 12:03 alfajiri alifungua mlango nakutoka chumbani kwake kuelekea sebuleni, wakati huohuo baba na mama yake wakiwa usingizini.

Ni kawaida ya Matrida kuwahi kuamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kuanza kufanya usafi wa nje pia kuwasha jiko ili kuandaa kinywa cha siku hiyo kabla ya kuanza kufanya usafi wa ndani.

Ilipofika saa 12:30, Matrida alimaliza usafi wake wa nje na kubakiwa na usafi wa ndani, wakati akijiandaa kuingia ndani, akiwa bado yupo mlangoni amekaa kutokana na uchovu wa kazi ya siku hiyo aliyokuwa amefanya, akiwa anaendelea kufikiria kufanya kazi iliyobaki lakini pale alipokaa kama hatua tatu hivi kuna kitu alikiona mbele yake.

Je, Matrida aliona kitu gani mbele yake na nini kilifuatia? Usikose Jumanne ijayo.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

      edit