Jana niliishia pale
nilipozungumzia mtu kuwa na hofu ya kuhisi kuwa huwezi kufanya jambo fulani kwa
sababu wewe ni mdogo, huna pesa, huna elimu, huna ndugu wala jamaa eneo
ulilopo, kwenye ukoo wenu hamna mtu mwenye histori ya kufanya jambo kama hilo.
Tuendelee na sehemu ya
pili ya mada yetu
Inayohusu namna ya kuondoa
au kutoa hofu, kabla ya kujifunza kuondoa hofu nimejaribu kukupitisha
kwenye baadhi ya aina za hofu ili kuweza
kujua mantiki ya kile ambacho tunajifunza.
Hii ni hofu ya kipuuzi
ambayo kama usipoangalia itakutafuna wewe na kizazi chako kijacho.
HOFU YA KUSHINDWA
Hofu hii aiko mbali sana
na ile ya kutengenezwa kwani unavyotengenezewa hofu au unavyojitengenezea hofu
basi hata kwenye kufanya maamuzi ya jambo fulani wewe unakuwa na hofu ya
kushindwa. Yaani unaona ni heri kubaki na shilingi 20000 uliyonayo chini yam to
kuliko kuanzisha biashara ya maembe kwa kuamini kuwa unaweza kukosa wateja na
mwisho wa siku maembe yakaoza. Na mtaji ukakatika papo kwa papo.
Ndugu yangu, watu wote
duniani ambao unawaona, unawasikia na kuwasoma au kuhadithiwa kuwa wana
mafanikio, hawakuzaliwa na hayo mafanikio bali waliyapata hapa hapa chini ya
jua kwenye nchi ambayo wewe pia unaishi, kwenye mtaa ambao nawe unakaa.
Kilichotokea kwao ni kukubali kujifunza kwa
kukubali kushindwa mara kwa mara , naposema kushindwa namaanisha kuishindwa kwa
fakti au kushindwa kwa sababu maalumu siyo kushindwa kwa uzembe.
UNAPOSHINDWA mara ya
kwanza utakuwa umejifunza ni kwa nini umeshindwa hivyo awamu ya pili huwezi
kushindwa na kama utashindwa basi utashindwa kwa sababu na kwa njia nyingine.
Ila kadri unavyozidi
kushindwa mara nyingi ndivyo hivyo unavyozidi kuyakaribia mafanikio au kuufikia
ushindi kwa sababu madhaifu, matatizo, changamoto zote za kushindwa unazifahamu
hivyo hubabaiki na jambo lolote wala hakuna changamoto mpya ambayo itakufuata
utashindwa kuitatua na kama ukishindwa basi hiyo hiko juu ya uwezo wako kabisa
na hata uwezo wa kibinadamu.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U