Thursday, May 4, 2017

Published 5/04/2017 11:21:00 AM by

MAMBO YATAKAYOKUSAIDIA KUANZA BIASHARA YAKO KWA MAFANIKIO

Inawezekana hapo ulipo ukawa huna kazi ama unakazi ambayo unaona haikuingizii kipato cha kutosha. Inawezekana pia kutokana na sababu hizo ukawa una shauku kubwa ya kutaka kuanzisha biashara ambayo itakulipa. Na inawezekana tena umekuwa ukijiuliza maswali mengi ufanye nini au ufanye bishara gani ambayo kwako itakuingizia pesa nyingi na kwa muda mfupi.

Hayo ni baadhi ya maswali machache kati ya mengi ambayo naamini umekuwa ukijiuliza sana kutaka kujua, ni biashara gani ambayo inaweza kuwa ya manufaa kwako zaidi. Naamini pia kwa maswali hayo umekuwa ukitafuta kama mwongozo wa kukusaidia kufanikiwa kibiashara pale utakapoanza. Kama nia na lengo lako ni hilo uko sawa. Nimesema hivyo nikiwa na maana kwamba, biashara yoyote utakayoianza ili iweze kufanikiwa ni lazima ujue kwanza mambo ya msingi ya kukusaidia kufanikiwa.
Watu wengi kutokana na kutokujua mambo hayo mapema au kukosa mwongozo huo sahihi hujikuta kila wanapoanza biashara huwa ni watu wa kushindwa sana. Leo hii utakuta mtu huyo yupo kwenye biashara hii au kesho ile ilimradi tu yupo yupo na ukichunguza, hakuna mafanikio makubwa anayokuwa anayapata. Tatizo kubwa linalopelekea hali hiyo ni kule kwa wao kutokujua mambo ya msingi yatakayowapa mafanikio, hasa pale unapoanza biashara.
Leo kwa kusoma makala haya, utajifunza mambo haya muhimu yakukusaidia kuanza bashara yako kwa mafanikio makubwa. Bila shaka yoyote, kwa kujua mambo haya yatakusiadia kufanya biashara yako kwa ushindi . Ile hofu ya kusema kwamba naweza nikashindwa kwa namna moja au nyingine naweza sema utakuwa umeipunguza kwa kiasi kikbwa. Najua unajiuliza tena mambo hayo ni yepi ya kuyajua kabla ya kuanza kufanya biashara? Toa shaka na twende pamoja sasa kujifunza.
1. Pata uzoefu.
Kabla hujaanza kufanya biashara unayotaka kufanya kitu cha kwanza unachotakiwa utambue ni lazima upate au ujenge uzoefu kwenye biashara hiyo. Nikiwa na maana kwamba biashara unayoiendea kuifanya ni lazima uijue ndani nje kwa sehemu kubwa sana . Bila kuwa na uzoefu angalau kidogo sio rahisi sana kuweza kufanikiwa kwa biashara inayotaka kuifanya au kuiendea. Ni lazima utaanguka tu ikiwa utaingia kichwa kichwa bila kuijua biashara hiyo vizuri.
Kwa mafano unataka kuanzisha duka la vipodozi, pata uzoefu kwa kuwatembelea watu wenye maduka yenye vipodozi . Lakini hiyo isiishie hapo utatakiwa pia uwaulize maswali ya kutosha ili kujijua biashara hiyo vizuri. Pia kama unataka kufanya kilimo cha aina fulani ni lazima sana kuwatembelea wataalamu wa kilimo hicho ili kujifunza. Kwa kufanya hivyo utajenga uzoefu na itakusaidia kuanza biashara yako kwa mafanikio makubwa.
2. Jiwekee malengo ya kibiashara.
Kabla hujaanza biashara yako ni vyema ukatambua malengo uliyonayo kwenye hiyo biashara. Ni lazima ujiulize unataka kufika wapi kwenye hiyo biashara? Unataka kuwa mfanyabiahara mdogo wa kawaida? Au unataka kuwa mfanyabiashra mkubwa. kwa kujiuliza maswali kama hayo na mengineyo mazito yatakufanya ufanye biashara yako kwa ukomavu mkubwa.
Kwa kuwa utakuwa umeshajua malengo yako ya kibiashara ni wapi unapotakiwa kufika, endelea kuwekeza nguvu zako nyingi huko. Tambua ni baada ya mwaka mmoja au miwili utakuwa wapi. Kwa kujiwekea mahesabu kama hayo itakusaidia sana kuweza kufanya biashara yako kwa ushindi kwa sababu ya kuweka juhudi nyingi bila kuchoka. Kwa juhudi hizo utajikuta umekuwa mshindi.
3. Tengeneza mtandao wako.
Kabla hujaanza biashara ni lazima ujue mtandao vizuri utakaoweza kukusaidia kufanikiwa. Ukijijengea ‘netwek’ yako nzuri ya kibiashara itakupa mafanikio makubwa na itakuwa ni njia bora ya kisasa ambayo umeichagua kuitumia kukuza biashara. Lakini hata hivyo si njia tu ya kisasa pia wengi hawaitumii, nikiwa na maana hawana mtandao.
Kwa mfano, unapokuwa na mtandao wako mzuri, mara nyingi mtandao wako huo unakusaidia kuifanya biashara yako kuwa juu hata katika kipindi soko linapokuwa limeshuka au baya kabisa. wale watu ambao upo nao kwenye mtandao mmoja ndio itakuwa chanzo cha kukuza na kutangaza iashara yako vizuri. Angalia biashara za mitandao au ‘netwek marketing’ nyingi zinafanya vizuri kwa sababu ya mtandao walioweka waanzilishi wake.

4. Wajue washindani wako vizuri.
Ni vyema kabla hujaanza biashara yako, weka mikakati ya kuwajua washindani wako na pia elewa jinsi ya kukabiliana nao. Kitendo cha kuwajua washindani wako kitakusaidia sana kujipanga vizuri kwa ajili ya kutoa huduma bora na hata kuweza kumudu soko kwa uhakika. Lakini ikiwa utaingia kwenye biashara bila kujua wapinzani wako itakusumbua kidogo kufanikiwa.
Kumbuka kwamba kabla hujaanza biashara yako ni lazima upate uzoefu, uwe na malengo mazuri ya kibiashara, jiwekee mtandao na bila kusahau ni lazima kuwajua washindani wako. Kwa kuyajua mambo haya manne kwa vyovyote ni lazima utakuwa mshindi kwenye biashara yako.
Kwa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali.

Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U     
Read More
      edit
Published 5/04/2017 10:32:00 AM by

AMANDA AWASHANGAA WANAUME KUONGA





SEXY lady kunako tasnia ya Bongo Muvi, Tamrinah Poshi ameshangazwa na tabia ya baadhi ya wanaume kuhonga wanawake wakati pesa wanazitafuta katika mazingira magumu na ya kusikitisha.

Amanda alidai kuwa, anashangazwa na tabia hiyo ilihali wakijua kwamba hivi sasa pesa imekuwa ngumu kupatikana. “Mi’ nawashangaa sana wanaume wahongaji, mtu ana mke, lakini bado anahangaika na kuhonga michepuko, kama mimi ningekuwa mwanaume, nisingekuwa ninahonga aisee,” alisema Amanda.

wa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali.

Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U     
Read More
      edit
Published 5/04/2017 10:17:00 AM by

SCANE ZA MAPENZI ZAMTESA MWANAHERI

MWIGIZAJI wa Bongo Muvi, Mwanaheri Ahmed, amefunguka kuwa, suala la kucheza ‘sini’ (scene) za kimapenzi kwenye filamu huwa linamtesa hasa linapokuja suala la kumlaghai mwanaume.


Akipiga stori na Showbiz Xtra , Mwanaheri alisema kuwa, pamoja na mwigizaji kupaswa kuvaa uhusika wa scene yoyote ile unayopangiwa, lakini kwake uhusika wa mapenzi huwa unamtesa na kumnyima usingizi.
“Scene za malavidavi kwangu huwa ni mtihani na sizipendi, huwa zinaninyima amani hasa ninapotakiwa kumlaghai mwanaume, wakati mwingine nahisi nikijibebisha sana, naweza kumkwaza baby wangu. Ila uhusika wa kukasirika hata kama utanikurupusha usingizini, nitakuwa huru nao,” alisema.

wa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali.

Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U     

CHANZO: GPL
Read More
      edit
Published 5/04/2017 09:57:00 AM by

MAGAZETI YA LEO MAY 4, 2017











Kwa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali.

Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U     
Read More
      edit

Wednesday, May 3, 2017

Published 5/03/2017 03:46:00 PM by

TABIA AMBAZO UNAWEZA KUZITUMIA KATIKA KUNUFAIKA KIBIASHARA

Moja ya vitu ambavyo kila mfanyabiashara anapaswa kujifunza , ni tabia za binadamu. Hii ni kwa sababu mahusiano ya kibiashara, kati ya mfanyabiashara na mteja wake, yanategemea sana uelewa ambao mfanyabiashara anao juu ya tabia za asili za binadamu. Na kama unavyojua, biashara za zama hizi ni biashara za mahusiano, mtu hanunui kwako kwa sababu unauza, ila ananunua kwako kwa sababu anakujua wewe na biashara yako.
 

Leo nataka nikushirikishe tabia moja ya asili ya binadamu ambayo unaweza kuitumia kunufaika kibiashara. Kwa kujua tabia hii na kuitumia vizuri, utaweza kuikuza biashara yako mara dufu na kupata wateja wengi watakaodumu kwenye biashara yako.  Kabla hatujaanza kuangalia tabia hii, niseme wazi kwamba tabia utakayoenda kujifunza hapa siyo ya kuwalaghai watu, bali kuwapa watu kile wanachotaka na wao wanakupa unachotaka.Sheria moja ya dunia ni nipe nikupe, yaani watu ni rahisi sana kutoa pale ambapo unakuwa umeshawapa. 

Kuna tabia moja ya asili ya binadamu ambayo kila mfanyabiashara anatakiwa kuijua na kuweza kuitumia vizuri. Tabia hii ni UBINAFSI. Kila binadamu ni mbinafsi, ndiyo namaanisha hata wewe na mimi ni wabinafsi. Tunachotofautiana ni viwango vya kuonesha ubinafsi wetu. Lakini mara zote huwa tunajifikiria sisi. Na ubinafsi siyo jambo baya, kwa sababu ndiyo unatuwezesha kujijali na hatimaye kuweza kuishi. Tatizo ni pale ubinafsi wako unapoingilia maslahi ya wengine, ndipo matatizo huanza.



Sasa turudi kwenye matumizi ya ubinafsi wa watu kwenye biashara yako. Iko hivi, kila mtu anapenda kupata vitu bora kwa kutumia fedha kidogo. Ndiyo maana mara nyingi watu wanapopewa bei, huwa wanataka kupata punguzo. Ukipewa vitu viwili vyenye ubora sawa, kimoja kikawa ghali, na kingine kikawa rahisi, utachukua kile cha bei rahisi. Au kama unapewa mikate miwili kwa bei sawa, ila mmoja ni mkubwa na mwingine ni mdogo, utachukua ule mkubwa, labda kama mdogo una vitu vya ziada.
Unaona sasa rafiki, tunapenda kujipendelea, tunapenda kupata kilicho bora kwa gharama kidogo. Tunapenda kupata zaidi ya tunavyopata.


Kwanza tuangalie njia ambayo siyo sahihi kutumia njia hii.
Kuna wafanyabiashara wengi ambao wamekuwa wanatumia tabia hii, iwe kwa kujua au kwa kutokujua, ila wanaitumia kimakosa na inawagharimu baadaye. Wanachokifanya wafanyabiashara hawa ni kuweka bei kubwa ya vitu vyao kuliko uhalisia, ili mtu anapoomba kupunguziwa, basi wakipunguza ifike kwenye ile bei ambayo ni halisi.

Huku ni kudanganya na hakuna kitu ambacho watu hawapendi kama kudanganywa. Kadiri unavyofanya hivi watu watajenga tabia ya tofauti ambayo haitakuwa nzuri kwa biashara yako. Watajizoesha kwamba kila kitu kwako kinauzwa kwa bei ambayo siyo halisi, hivyo yule anayeweza kupambana akapunguziwa basi ndiyo anafaidi.

Wakati mwingine inajenga picha mbaya kabisa, kwa mfano mtu mmoja kanunua kitu kwako, na yeye hakujua kama unapunguza bei, hivyo ulipomwambia bei yeye akalipa na kupata alichotaka. Sasa atakaposikia mwingine kanunua kwa bei ya chini kuliko yeye, ataona umemwibia fedha. Mteja kama huyu anaweza sirudi tena kwenye biashara yako. Na kama atarudi basi hatakuwa na imani kwako.

Njia sahihi ya kutumia tabia hii.
Ipo njia sahihi ya kutumia tabia hii ya ubinafsi ambayo kila mmoja wetu anayo. Njia hii ni kutoa thamani kubwa sana kuliko fedha ambayo mtu analipa. Hapa mtu lazima atakuja kwako na ataendelea kuwa mteja mzuri kama kweli atapata thamani hiyo mara zote.

Unachofanya ni kutoa thamani kubwa sana kwa bei ambayo haiendani na thamani hiyo, kiasi kwamba mteja anaona kama anakuibia hivi. Unatoa thamani ambayo mteja hawezi kuipata sehemu nyingine yoyote, hii inamfanya akutegemee wewe na awe mteja wako wa kudumu. Kwa kutoa thamani kubwa, mteja atakuja yeye na pia atawaambia wengine. Tabia nyingine ya binadamu ni kwamba kizuri hawawezi kula wenyewe, hivyo watawaambia na wengine pia.

Kitu muhimu nataka ujue ni kwamba kutoa thamani kubwa haimaanishi uuze vitu kwa bei rahisi, unaweza kuuza bei ile ile ambayo imezoeleka lakini unaongeza thamani kubwa mno. Au wakati mwingine hata ukauza kwa bei ya juu lakini bado thamani ikawa kubwa sana kiasi kwamba watu wakawa tayari kulipia thamani hiyo.


Njia hii ya kuongeza thamani inafaa sana kwa wale ambao wanatoa huduma au wanatengeneza bidhaa zao wenyewe. Lakini pia inawafaa mno wale wanaofanya biashara ya rejareja. Japokuwa kwenye biashara ya reja reja bidhaa ni ile ile na bei ni zile zile, bado unaweza kuongeza thamani kubwa kwa namna unavyowauzia wateja wako bidhaa zile. Kauli zako kwa wateja wako zinaweza kuwafanya wajisikie vizuri na wapende kuja kwenye biashara yako mara zote. Wewe mwenyewe unajua, kuna biashara ukienda unajisikia vizuri na nyingine unajisikia vibaya jinsi unavyopokelewa na kuhudumiwa. Sasa wewe wafanye wateja wako wajisikie vizuri kuwa kwenye biashara yako.

Ni asili ya binadamu kuwa wabinafsi, tunapenda kupata zaidi kwa kutoa kidogo. Angalia biashara yako, ona ni namna gani unaweza kuwapa wateja thamani zaidi na wao watakuwa tayari kununua kutoka kwako.

Kwa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali.

Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U     
Read More
      edit
Published 5/03/2017 10:29:00 AM by

MAGAZETI YA LEO MAY 3, 2017














Kwa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali.

Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U     
Read More
      edit

Tuesday, May 2, 2017

Published 5/02/2017 10:26:00 PM by

CHUNGA SANA NDOA HAITAJI MAZOEA

VIPO vitu vingi ambavyo kadiri unavyovifanya sana, ukavizoea, vinaleta tija lakini asikwambie mtu ndoa haihitaji mazoea. Ndoa inatakiwa kuwa mpya kila siku. Kama ni kujifunza, kwenye ndoa unapaswa kujifunza kila wakati. Kila siku umuone mwenzi wako kama mpya vile.
Kama ndiyo kwanza mmeonana. Chukulia kama vile ndiyo umemuona kwa mara ya kwanza, unavyokuwa na kile ‘kiraruraru’ cha kumhitaji.
Nasema hivyo marafi ki zangu kwa sababu mimi na wewe ni mashahidi katika hili. Tunashuhudia namna ambavyo matatizo yanavyotokea. Watu wanagombana, watu wanashitakiana kila kukicha, watu wanaachana.
Ukichunguza kwa makini, chanzo kikubwa cha watu kufi kia hatua hiyo ni mazoea. Wameishi miaka mingi, wamezaa, wamezoeana kupita kiasi. Mke hana habari tena na mume. Mume naye ndiyo usiseme, hana muda na mke.



Wanachukuliana poapoa tu. Kinachotokea, kama zamani walikuwa wana tabia ya kujaliana kila wakati, inafi ka wakati wanaacha. Walikuwa wanapigiana simu kila wakati, inafi ka wakati hawapigiani hata siku mbili tatu. Wanapigiana pale panapokuwa na jambo la msingi tu. Mtoto anaumwa, ada inahitajika haraka na mambo mengine yanayofanana na hayo. Zile za kuulizana ‘baby unakula nini leo’, ‘mpenzi nikuletee zawadi gani’ zinakoma kabisa.
Mke anakuwa bize na marafi ki zake. Mume naye anakuwa bize na marafi ki zake. Ndoa itawakutanisha jioni au usiku. Usiku wenyewe kila mtu akifi ka anakuwa na hamsini zake. Wanalala kama vile mtu na kaka dada yake. Hiyo yote yanaletwa na mazoea.
Mke anamzoea mume wake hadi inafi ka wakati anapoteza hamu naye. Anamuona wa kawaida. Awepo sawa, asiwepo hewala. Vivyo hivyo mume. Naye anamuona mke kama vile mtoto wa ba mkubwa. Nyumbani mke hana muda na mume.
Akirudi mambo yote anamuachia dada wa kazi. Aandae maji ya kuoga, chakula na hata usafi wa chumbani kwao.






NI RAHISI KUTAMANI MTU MWINGINE
Kadiri mazoea yanavyozidi kushika hatamu, ni rahisi sana mke kumtamani kijana sharobaro kutokana na namna ambavyo anajua kujali hata kwa kuuliza vipi umeamkaje?
Vipi unaendeleaje?
Mtoto hajakusumbua sana leo usiku?
Acha nikusaidie kubeba hii ndoo ya maji na mambo mengine yanayofanana na hayo. Hii haina tofauti na yule fundi ambaye anamwita na kutokea kwa wakati pale gari lake linapokuwa limeharibika barabarani. Gari kanunuliwa na mumewe lakini fundi anakuwa mwepesi sana kufi ka au kutoa msaada eneo la tukio kuliko mume.
Fundi anajali adha anayoipata mke wa mtu barabarani kuliko mwenye mke, ana bidii ile mbaya. Mwenye mke akipigiwa simu na mkewe kuambiwa kwamba gari imeharibika, anachukulia poa. Majibu ni yale ya ‘sasa mimi nifanyeje?
Si umuite fundi?’
Hayo ndiyo mazoea yenyewe!

Mume anasahau kwamba mke anafahamu kwamba yeye si fundi lakini amempa taarifa kama mtu wake wa karibu.
Mtu ambaye anaamini atampa jibu lenye msaada. La kumpa matumaini, la kumtia moyo lakini matokeo yake anaambulia maneno ya shombo. Mazoea yanasukuma hata suala la faragha liwe la kawaida tu. Liwepo lisiwepo yote heri.
Wanaishi pamoja hata miezi miwili, hakuna anayemgusa mwenzake. Matokeo yake, atazidiwa na matamanio na akapata mtu wa kumtamani, anampa nafasi. Akimpata mtu anayejua kujali, anayejua ‘vurugu za mapenzi’ anashawishika. Anajikuta huko sababu tu ya mazoea mliyoyaweka. Usaliti unakua na hata kuhatarisha ndoa, achilia mbali uwezekano wa kupata magonjwa.
ACHA MAZOEA
Kama vile mlivyoonana, mnapaswa kuishi hivyo miaka yote. Chukulia kama ni jukumu. Usiufanye uhusiano wako uchache. Kila siku uamshe kwa staili tofauti. Kama ulikuwa una tabia ya kumtoa ‘out’, zidisha kasi.
Kama ulikuwa unamthamini kwa shida na raha basi hayo ndiyo yawe maisha yako. Mpende, mdekeze ikibidi maana huyo ndiye wako. Hakuna mwingine. Dekezaneni kila inapobidi maana hakuna namna. Kila mmoja awe na hamu na mwenzake kila wakati.

Usichukulie poa, thamani ya mke au mume inapaswa kuwa vilevile kila siku. Kila mmoja aguswe na maumivu ya mwenzake. Mkianguka kwenye shida muwe pamoja na mkiwa kwenye raha basi mfurahi pamoja. Heshimuni ndoa, iwekeni mbele na muipe thamani kila uchwao! Mkiishi kwa staili hiyo, maisha mtayaona matamu na hakuna kitakachowayumbisha!

Kwa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali.

Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U     

CHANZO: GPL                  

Read More
      edit
Published 5/02/2017 08:45:00 PM by

JINSI YA KUKAMILISHA MIPANGO YAKO JAPO KUNA CHANGAMOTO NYINGI

Namna gani ya kuweza kutatua changamoto, ili uweze kutekeleza majukumu yako kwa wale wanaokutegemea, na pia uweze kutekeleza mipango yako mikubwa ya maisha.

Kwanza; pitia majukumu yako yote, na chagua yale ambayo utawajibika moja kwa moja.

Haijalishi una mizigo mingi kiasi gani kwenye maisha yako, kama ikitokea unakufa leo, hakuna mzigo hata mmoja ambao utaondoka nao. Na hata wale wanaokutegemea wewe moja kwa moja, hawatakufa na wewe. Hii ni kutaka kukuonesha ya kwamba, unahitaji kuwajibika na mizigo yako na wale wanaokutegemea pia, lakini isiwe kikwazo chako kuwa na maisha.

Hivyo hatua ya kwanza kabisa kwako kuchukua ni kupitia majukumu yako yote, pitia mahitaji ya wale wote ambao wanakutegemea wewe moja kwa moja. Kwa kila jukumu na hitaji, angalia lipi ni muhimu kabisa ambalo linakuhitaji wewe moja kwa moja ulifanyie kazi. 

Angalia yapi ambayo yanaweza kufanywa na wengine, na angalia yapi ambayo yanaweza kusubiri kwa kuwa siyo dharura na wala siyo haraka.

Kama ni wazazi na ndugu wanaokutegemea, kama wapo ambao wana uwezo wa kujishughulisha, wape njia wanazoweza kujishughulisha nao pia, ili kupunguza utegemezi usio wa lazima. Kwa zoezi hili, utabaki na yale majukumu muhimu sana, ambayo siyo nje ya chakula, afya na elimu. Usije ukaniambia moja ya majukumu yanayokusubiri ni michango ya harusi au kuandaa sherehe sijui za nini. Hayo futa kabisa, kama uwezo wako hauruhusu usilazimishe, muhimu ni kuhakikisha mahitaji ya msingi kabisa ya kuwawezesha watu waendelee kuishi yanafikiwa.

Kwa zoezi hili utapunguza mzigo mkubwa sana, nakuambia hilo kwa sababu kwa jamii zetu, watu wakishajua fulani anaweza kutusaidia, basi kila aina ya shida watakayopata hawatafikiria mara mbili, bali wataileta moja kwa moja kwako. Sasa unapoweka vigezo vya mambo gani unaweza kusaidia kwa kipindi ambacho bado wewe mwenyewe hujakaa vizuri, watu watajifunza kuja kwako kwa yale ambayo ni muhimu zaidi.

Pili; kabla hujaanza kufanya jambo, lijue mpaka mwisho, na gawa majukumu madogo madogo ya kukamilisha.

Tabia ya kuanza mambo na kuachia njiani, kuanza mengine na kuachia njiani pia inatokana na kuanza mambo bila ya kujipanga vizuri. Wala haihusiani na kuwa na majukumu mengi au kipato. Kwa sababu kabla hujaanza jambo lolote, lazima uwe umeshaliona mpaka mwisho wake, umeshajua utafikaje pale, na pia kujipanga kwa tahadhari zozote. Usipate tu wazo, au kuambiwa tu kitu na kukimbilia kufanya, lazima ufanye tathmini, wewe mwenyewe unajijua hivyo lazima ujiangalie kwanza.

Kingine muhimu ni kutokuanza mambo mengi kwa wakati mmoja. Anza jambo moja kwa wakati, na nenda nalo mpaka mwisho wake, kabla ya kuanza jambo jingine. Ni bora kufanya mambo mawili na kuyakamilisha, kuliko kufanya mambo kumi na yote ukaishia njiani.

Anza yale ambayo unaona unaweza kumaliza, na kama huwezi subiri. Anza jambo moja kwa wakati, weka juhudi zako mpaka uone matokeo yake.

Tatu; weka fedha zako kwenye eneo ambalo huwezi kuzipata kwa haraka.

Ukisema unakusanya mtaji kwa kuweka fedha benki, niamini, hutafikisha huo mtaji, kwa sababu utakapopata shida kidogo, ni rahisi kwenda benki na kutoa fedha ili kutatua shida ile. 

Lakini inapotokea tatizo na huna fedha benki, inakulazimisha wewe kufikiria njia nyingine za kulitatua. Kwa sababu hii, hakikisha hukai na fedha za mipango ya baadaye benki, badala yake ziweke kwenye maeneo ambayo huwezi kuzipata haraka.

Unaweza kuwekeza fedha yako kwenye maeneo ambayo siyo rahisi kuzitoa lakini pia haitakuchukua muda mrefu sana kuzitoa. Hivyo unaweza kuweka kwenye akaunti ya muda maalumu, yaani fixed deposit ambapo huwezi kutoa kwa kipindi fulani ambacho utaeleza, labda miezi mitatu, sita, tisa au mwaka. Pia unaweza kuwekeza kwa kununua hisa na vipande, ambapo uuzaji wake hauchukui muda mrefu sana kama uwekezaji wa maeneo kama ya majengo na ardhi.

Fedha unayopaswa kubaki nayo wewe ni ile ya matumizi yako, na ile ya dharura, iwapo lolote litatokea. Akiba nyingine, ziweke kwenye maeneo hayo.


 Nne; jilipe wewe kwanza, kabla hata hujaanza kutumia kipato chako.

Huenda hatua hiyo ya tatu ikakushinda kwa sababu labda hufanikiwi hata kufikisha kiasi cha kuweza kuwekeza, kutokana na matatizo yanayokuwa yanakuandama mara kwa mara. Sasa hapo cha kufanya ni hichi, kila unapopata kipato chako, ondoa sehemu fulani ya kipato hicho, labda asilimia 10, au hata chini ya hapo, na iweke mbali kabisa. Chukulia kama ulinunua kitu na hivyo huwezi kuipata tena. Tumia ile iliyobaki kwenye matumizi yako na wategemezi wako. Usikubali kabisa kipato chako chote kitumike kwenye matumizi, hata kama una matatizo kiasi gani, weka pembeni hata elfu kumi, haitakuwa sawa na bure.

Tano; pambana zaidi, weka juhudi zaidi, teseka zaidi kwa muda mfupi kupunguza hayo ya sasa.

Pamoja na kufanya hayo hapo juu, kwa kuwa unajua matatizo yako ni yapi, unahitaji kuongeza kipato chako mara dufu. Kwa sababu hata kama utapunguza matumizi na yale ya wategemezi, itafika hatua huwezi kupunguza zaidi, watu lazima wale, na afya lazima zilindwe iwapo magonjwa yanatokea. Hivyo kilichobaki hapo ni wewe kutafuta njia zaidi za kuongeza kipato chako. Kama umeajiriwa anza biashara ya pembeni. Kama huwezi kuanza biashara kwa sababu yoyote, tafuta kitu unachoweza kufanya kwa muda wako wa ziada ili ulipwe zaidi.

Usiniambie una matatizo yote hayo halafu unaenda kazini asubuhi, unarudi jioni na kusubiri tena mpaka kesho, na jumamosi na jumapili na wewe unajiambia una weekend. Wewe unahitaji kupambana hasa, unahitaji ukitoka kazini upite sehemu nyingine ya kukuwezesha kuongeza kipato zaidi. Jumamosi na jumapili zinapaswa kuwa siku nzuri sana kwako. 

Pambana, fanya kile ambacho unaweza kufanya, halali lakini, ili uweze kuongeza kipato chako, hata kama ni kwa kiasi kidogo sana. Wewe huna anasa ya kupumzika na kustarehe kwa sasa, unahitaji kuweka juhudi ili kuweza kutoka hapo ulipo.



Kwa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali.

Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U                       
Read More
      edit

Monday, May 1, 2017

Published 5/01/2017 11:28:00 AM by

NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUTIBULIWA UNA CHETI FEKI




Najua familia za watu  zaidi ya elfu tisa ziko kwenye wakati mgumu sana kutokana na kutumbuliwa kwa kuajiriwa wakiwa na vyeti feki.

Kama wewe, baba, mama au ndugu yako ni miongoni mwao. Kipi cha kumshauri au achukue hatua zipi?

Kwa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali.

Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U                      

Read More
      edit
Published 5/01/2017 09:45:00 AM by

MAGAZETI YA LEO MAY 1, 2017













Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na:M&U
Read More
      edit