Inawezekana hapo ulipo ukawa huna kazi ama unakazi
ambayo unaona haikuingizii kipato cha kutosha. Inawezekana pia kutokana na
sababu hizo ukawa una shauku kubwa ya kutaka kuanzisha biashara ambayo
itakulipa. Na inawezekana tena umekuwa ukijiuliza maswali mengi ufanye nini au
ufanye bishara gani ambayo kwako itakuingizia pesa nyingi na kwa muda mfupi.
Hayo ni baadhi ya maswali machache kati ya mengi
ambayo naamini umekuwa ukijiuliza sana kutaka kujua, ni biashara gani ambayo
inaweza kuwa ya manufaa kwako zaidi. Naamini pia kwa maswali hayo umekuwa
ukitafuta kama mwongozo wa kukusaidia kufanikiwa kibiashara pale utakapoanza.
Kama nia na lengo lako ni hilo uko sawa. Nimesema hivyo nikiwa na maana kwamba,
biashara yoyote utakayoianza ili iweze kufanikiwa ni lazima ujue kwanza mambo
ya msingi ya kukusaidia kufanikiwa.
Watu wengi kutokana na kutokujua mambo hayo mapema
au kukosa mwongozo huo sahihi hujikuta kila wanapoanza biashara huwa ni watu wa
kushindwa sana. Leo hii utakuta mtu huyo yupo kwenye biashara hii au kesho ile
ilimradi tu yupo yupo na ukichunguza, hakuna mafanikio makubwa anayokuwa
anayapata. Tatizo kubwa linalopelekea hali hiyo ni kule kwa wao kutokujua mambo
ya msingi yatakayowapa mafanikio, hasa pale unapoanza biashara.
Leo kwa kusoma makala haya, utajifunza mambo haya
muhimu yakukusaidia kuanza bashara yako kwa mafanikio makubwa. Bila shaka
yoyote, kwa kujua mambo haya yatakusiadia kufanya biashara yako kwa ushindi .
Ile hofu ya kusema kwamba naweza nikashindwa kwa namna moja au nyingine naweza
sema utakuwa umeipunguza kwa kiasi kikbwa. Najua unajiuliza tena mambo hayo ni
yepi ya kuyajua kabla ya kuanza kufanya biashara? Toa shaka na twende pamoja sasa
kujifunza.
1. Pata uzoefu.
Kabla hujaanza kufanya biashara unayotaka kufanya
kitu cha kwanza unachotakiwa utambue ni lazima upate au ujenge uzoefu kwenye
biashara hiyo. Nikiwa na maana kwamba biashara unayoiendea kuifanya ni lazima
uijue ndani nje kwa sehemu kubwa sana . Bila kuwa na uzoefu angalau kidogo sio
rahisi sana kuweza kufanikiwa kwa biashara inayotaka kuifanya au kuiendea. Ni
lazima utaanguka tu ikiwa utaingia kichwa kichwa bila kuijua biashara hiyo
vizuri.
Kwa mafano unataka kuanzisha duka la vipodozi, pata
uzoefu kwa kuwatembelea watu wenye maduka yenye vipodozi . Lakini hiyo isiishie
hapo utatakiwa pia uwaulize maswali ya kutosha ili kujijua biashara hiyo
vizuri. Pia kama unataka kufanya kilimo cha aina fulani ni lazima sana
kuwatembelea wataalamu wa kilimo hicho ili kujifunza. Kwa kufanya hivyo utajenga
uzoefu na itakusaidia kuanza biashara yako kwa mafanikio makubwa.
2. Jiwekee
malengo ya kibiashara.
Kabla hujaanza biashara yako ni vyema ukatambua
malengo uliyonayo kwenye hiyo biashara. Ni lazima ujiulize unataka kufika wapi
kwenye hiyo biashara? Unataka kuwa mfanyabiahara mdogo wa kawaida? Au unataka
kuwa mfanyabiashra mkubwa. kwa kujiuliza maswali kama hayo na mengineyo mazito
yatakufanya ufanye biashara yako kwa ukomavu mkubwa.
Kwa kuwa utakuwa umeshajua malengo yako ya
kibiashara ni wapi unapotakiwa kufika, endelea kuwekeza nguvu zako nyingi huko.
Tambua ni baada ya mwaka mmoja au miwili utakuwa wapi. Kwa kujiwekea mahesabu
kama hayo itakusaidia sana kuweza kufanya biashara yako kwa ushindi kwa sababu
ya kuweka juhudi nyingi bila kuchoka. Kwa juhudi hizo utajikuta umekuwa
mshindi.
3. Tengeneza
mtandao wako.
Kabla hujaanza biashara ni lazima ujue mtandao
vizuri utakaoweza kukusaidia kufanikiwa. Ukijijengea ‘netwek’ yako nzuri ya kibiashara itakupa mafanikio makubwa na
itakuwa ni njia bora ya kisasa ambayo umeichagua kuitumia kukuza biashara.
Lakini hata hivyo si njia tu ya kisasa pia wengi hawaitumii, nikiwa na maana
hawana mtandao.
Kwa mfano, unapokuwa na mtandao wako mzuri, mara
nyingi mtandao wako huo unakusaidia kuifanya biashara yako kuwa juu hata katika
kipindi soko linapokuwa limeshuka au baya kabisa. wale watu ambao upo nao
kwenye mtandao mmoja ndio itakuwa chanzo cha kukuza na kutangaza iashara yako
vizuri. Angalia biashara za mitandao au ‘netwek marketing’ nyingi zinafanya
vizuri kwa sababu ya mtandao walioweka waanzilishi wake.
4. Wajue
washindani wako vizuri.
Ni vyema kabla hujaanza biashara yako, weka
mikakati ya kuwajua washindani wako na pia elewa jinsi ya kukabiliana nao.
Kitendo cha kuwajua washindani wako kitakusaidia sana kujipanga vizuri kwa
ajili ya kutoa huduma bora na hata kuweza kumudu soko kwa uhakika. Lakini ikiwa
utaingia kwenye biashara bila kujua wapinzani wako itakusumbua kidogo
kufanikiwa.
Kumbuka kwamba kabla hujaanza biashara yako ni
lazima upate uzoefu, uwe na malengo mazuri ya kibiashara, jiwekee mtandao na
bila kusahau ni lazima kuwajua washindani wako. Kwa kuyajua mambo haya manne
kwa vyovyote ni lazima utakuwa mshindi kwenye biashara yako.
Kwa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali.
Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U
Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U