Saturday, June 10, 2017

Published 6/10/2017 01:09:00 PM by

SIMU YA MWENZA WAKO YA NINI, UNAJIPA PRESHA YA BURE


KWA wanandoa, uaminifu limekuwa ni jambo la msingi sana ndiyo maana kila siku tunasema, ili udumu na huyo uliyeingia naye kwenye ndoa, mjengee imani kuwa wewe ni wake na haitatokea siku ukamsaliti. Lakini wakati ukweli ukiwa hivyo, kwenye baadhi ya ndoa kuna sarakasi nyingi sana. Katika ulimwengu wa sasa kumekuwa na tatizo kubwa la baadhi ya wanandoa kutibuana kila siku kisa kikiwa
ni kutokuaminiana kupitia simu zao. Kwa hili niseme tu kwamba, ni wanandoa wachache sana ambao wanaamini simu za wenza wao hazina madhambi, wengi wanahisi wanasalitiwa kupitia simu na ndiyo maana unaweza kukuta mke akishika simu ya mumewe tu inakuwa shida. Si hivyo tu, wapo wake za watu nao hawataki kabisa simu zao zishikwe na waume zao, unajiuliza kwa nini iwe hivyo kama kila mtu anajiamini? Lakini sasa, leo naomba niwashauri kitu wale walioingia kwenye ndoa. Kuna mambo ambayo unatakiwa kuyapuuza laa sivyo huwezi kuwa na amani katika maisha yako. Kama kweli unampenda huyo uliyenaye, usimfikirie vibaya! Jenga imani kuwa,
hawezi kukusaliti. Hii tabia kwamba simu ya mwenza wako ikiita tu unachungulia kujua nani kapiga, SMS ikiingia unafungua, ya nini kujipa presha? Hivi unadhani kweli unaweza kumzuia huyo mwenza wako asikusaliti kwa kutompa uhuru wa simu yake? Hili ni gumu hivyo unachotakiwa kufanya ni kumuacha na simu yake. Usijipe presha zisizo na msingi. Unaweza kukurupuka, ukapokea simu ya mumeo, mara unakutana na sauti nyororo ya msichana, presha inakupanda bila kujua aliyepiga ni nani. Na yeye kwa kuwa aliyepokea siye aliyempigia, anakata. Wewe huko uliko unachanganyikiwa, unafikiri aliyepiga ni mchepuko. Kumbe aliyepiga labda ni mfanyakazi mwenzake

au rafiki yake wa kawaida tu. Wewe unakuja juu na kumwambia mumeo anakusaliti, kumbe hamna kitu kama hicho.Au wewe mwanaume unaweza kuchukua simu ya mkeo, ukaenda kwenye sehemu ya meseji ukitaka kujua ni nani huwa anachati nao. Bahati mbaya unakutana na meseji ya kimahaba iliyotumwa na mwanaume ambaye alikosea namba. Wewe bila kuwa na uhakika na kile ulichoona unakimbilia kuhitimisha kuwa, mke si muaminifu. Hili ni tatizo kubwa ndiyo maana leo kupitia safu hii nimeona niwakumbushe tu kwamba, simu ya mwenza wako achana nayo ili kujihakikishia amani ya moyo.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Read More
      edit
Published 6/10/2017 11:24:00 AM by

MAGAZETI YA LEO JUNE 10, 2017









Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

Read More
      edit

Wednesday, June 7, 2017

Published 6/07/2017 01:17:00 PM by

MSANII EBITOKE ASEMA AJAWAI KUKUTANA NA MWANAUME


Mchekeshaji kutoka Timamu African Media, Ebitoke baada ya kutangaza anamuhitaji msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol katika mahusiano ya kimapenzi, leo ameibuka na kioja kingine.


Ebitoke ambaye amekuwa akitoa vichekesho mbali mbali kupitia mitandao ya kijamii, ametoa kauli ambayo imetafsiriwa kuwa hajawahi kufanya mapenzi na mwanaume yeyote.
“Nawashangaa mnaonifananisha na USED, mimi niko SEALED jamani,
"Hatufanani thamani yangu ni kubwa kuliko make up za kichina,” aliandika Ebitoke Instagram.


Baadhi ya mashabiki wake wamechukulia jambo hilo kama utani, wengine wakimpongeza, huku wengine wakibeza kwa kudai amejishusha kusema hivyo.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

CHANZO:BONGO 5
Read More
      edit
Published 6/07/2017 10:57:00 AM by

MAGAZETI YA LEO JUNE 7, 2017





Read More
      edit

Sunday, June 4, 2017

Published 6/04/2017 04:19:00 PM by

MUME AJINYONGA KWA UGOMVI MKE KUUZA MALI ZA FAMILIA ALIPE MIKOPO SHINYANGA


Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Luhende Lusangija(34) mkazi mtaa wa Mwinamila Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga amekutwa amejinyonga nyumbani kwake kutokana na kile kilichotajwa kuwa mke wake alikuwa anauza mali za familia kutokana na mikopo aliyokuwa anadaiwa.

Tukio hilo limetokea Jumamosi June 3,2017 majira ya saa 11 alfajiri ambapo marehemu akiwa na watoto wake watatu nyumbani, aliamka na kisha kuchukua mtandio huku watoto wake wakiwa wamelala, na kuamua kujitundika kitanzi sebuleni, na kusababisha kifo chake papo hapo.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema mwanamme huyo amejiua kutokana na kwa kile kinachodaiwa kuwa na ugomvi wa siku nyingi na mke wake ambaye siku kabla ya tukio alikuwa ameshaukimbia mji wake.



Wakisimuliza tukio hilo majirani zake Safina Javali, alisema marehemu alikuwa na ugomvi na mkewe muda mrefu ambapo walikuwa wakipigana kila siku, kwa kile kinachodaiwa kuwa mwanamke alikuwa akikopa mikopo, na baada ya kushindwa kuirejesha alikuwa akiuza vitu vya ndani wakati mumewe akiwa safarini kwenye majukumu yake ya kikazi.

“Juzi alipokuja mwanaume kutoka safarini akakuta kitanda kimefungwa kwenda kuuzwa, ili mwanamke alipe deni la mikopo aliyokuwa akiichukua, ndipo ugomvi mkubwa ulipozuka hadi kusababisha mwanamke kuukimbia mji wake na kwenda kusiko julikana,”alisema Javali.

Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo kutokea walimsikia mtoto wake mkubwa wa miaka 7 majira ya saa moja asubuhi akilia kwa uchungu na kupiga kelele, kuwa baba yake amekufa kwa kujinyonga na walipofika kwenye mji huo na kuchungulia mlangoni ndipo wakamuona amenin’ginia kwenye paa la sebuleni akiwa ameshafariki.

Naye mwenye nyumba Halma Issa ambapo marehemu alikuwa mpangaji wake, alisema mji huo ulikuwa na ugomvi wa mara kwa mara, na walikuwa wakiwasuluhisha lakini ugomvi wao ulikuwa pale pale, na walipopata taarifa ya kifo chake walifika eneo la tukio kasha kuwasiliana na uongozi wa mtaa ilikufuata taratibu za kisheria.

Aidha mwenyekiti wa mtaa huo wa Mwinamila Ngokolo mjini Shinyanga Yohana Munisa, alikiri kupokea taarifa za marehemu huyo majira ya saa moja asubuhi, na alipofika eneo la tukio alimkuta Lusangija akiwa tayari amejinyonga, ndipo akatoa taarifa polisi ambapo nao wakafika ili kuuchukua mwili wa marehemu.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Elias Mwita alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, huku ndugu wa marehemu wakitafutwa ili kuuchukua mwili huo kwa taratibu za mazishi.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

CHANZO: MALUNDE BLOG
Read More
      edit

Saturday, June 3, 2017

Published 6/03/2017 05:42:00 PM by

JOKATI ASEMA ANATAKA MUME MWENYE HOFU YA MUNGU

Mrembo Jokate Mwegelo ameamua kuweka wazi juu ya mwanaume anayependa kuolewa naye na kuanzisha familia baada ya miaka mitano.

Joketi
Akizungumza na gazeti la Mwanachi Jokate ambaye ametajwa kuwa katika orodha la jarida la Forbes Africa la kuwa miongoni mwa vijana walio na umri chini ya miaka 30 wenye mafanikio mbalimbali kwa mwaka 2017.

 Kusema kweli kitu ninachotamani awe nacho mume wangu ni hofu ya Mungu, pia awe mchapakazi na mwenye malengo ya mbele. Mwanaume wa aina hiyo ni rahisi sana kumthamini mke wake, kutambua mwanaume mwenye upendo wa dhati si ngumu kwani unaangalia maisha yake binafsi anaishije na ndugu ,jamaa na marafiki” amesema Joketi.

Pia mrembo huyo amesisitiza kuwa suala la dini si kikwazo kwake kwani amezungukwa na watu wa imani tofauti.
Kwa takribani mwaka mmoja Jokate amekuwa akihusishwa kuwa na mahusiano na mwanamuziki Alikiba ingawa hakuna kati yao aliyewahi kuthibitisha hilo.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa



CHANZO: BONGO 5 
Read More
      edit
Published 6/03/2017 05:22:00 PM by

UZURI NA MVUTO USIOCHUJA


Upo uzuri ambao hauchuji, haufifii na wala hauna madhara… Upo uzuri ambao hauhitaji kutumia nguvu kubwa kumvuta mtu wa jinsia nyingine au wenzio.
Upo uzuri ambao mpaka kuzeeka kwako bado utakufanya uendelee kuonekana mzuri na kujiona wewe ni mzuri mnooo… uzuri usio na majuto yoyote wala kikomo!
 Hoja mbili tatu za kukukumbusha kuhusu uzuri huo!
1. Elimika!..... Ukielimika utastaarabika mwanamke, utajishughulisha! Utashika chenji zako mwenyewe mkononi… Utakuwa na upeo, utajua dunia inakwenda vipi.
Kuna watu wanasoma ila hawaelimiki. Wewe kuwa tofauti soma uelimike! Ukielimika huwezi kuburuzwa ovyo na mtu au makundi ya watu. Utakuwa na msimamo wako binafsi kwa kuwa utajua nini ni nini. Ukielimika utajishughulisha na utashika pesa yako mwenyewe hata kama ni kidogo kiasi gani, ni ya kwako! 

2. Roho nzuri…. Haijalishi una makalio makubwa kiasi gani au u mweupe kama karatasi… au una sura ya kuvutia namna gani ama umebeba mkoba wa laki ngapi.
Kama roho yako imejaa chuki za chini chini, husda, wivu, vinyongo, misengenyo, vijicho, kufurahia matatizo ya wenzio, kuharibia wengine na unafiki!....Woman you are ugly! Roho nzuri ni uzuri usiochuja hata mbele za Mungu!

3. Tabasamu la upendo… huu ni uzuri ambao wengi wetu tunauchukulia poa sana. Ni uzuri usio na gharama yoyote ile.
Salimia watu kwa tabasamu la upendo bila kujali umri, rangi, hali zao kiuchumi au vyeo vyao kazini. Huwezi jua tabasamu lako la upendo litakurudishia baraka gani mbele ya safari pasipo wewe kujua. Huwezi jua salamu yako yenye tabasamu inampa nani hali ya kujiona anathaminika. Utunze uzuri huu kwa gharama yoyote ile. Ni tiba kwako na wengineo!

4. Kauli safi!... kuna watu wanadhani kutukana ni ujanja, kuongea sana ovyo ovyo ni umjini... kuongea kimipasho kila saa ni ushujaa…. Kujua matusi ya nguoni ndio kwenda na wakati… hata wakati ambao mtu amekukalfisha nafsi vibaya sana, unapoweza kumjibu pasipo tusi hata moja la nguoni wewe ni mzuri! Mzuri sana!
Unapoporomosha matusi kuyajibu matusi, unajivunjia heshima, unapoteza uzuri wako! Na hakika unaweza kumchoma adui yako kwa jibu safi zaidi kuliko jibu kali la matusi kwa kuwa nia ya mtu anayekuumiza ni kuona umeumia na kujibu tusi kunadhihirisha amekuweza!

5. Usafi…. Ni uzuri usiochuja kabisa! Utazeeka nao, utawavutia watu popote na wakati wowote ule. Usafi aina zote ni silaha kubwa sana. Hata wewe unapokutana na mtu nadhifu anayeweka mazingira yake katika hali nadhifu lazima utahisi kuvutiwa naye.
Hii inajumuisha kuikubali ngozi yako na kuiweka nadhifu bila kuikwangua kwangua. Mwanamke mrembo ambaye amejipamba vito ila kasimama kwenye mazingira machafu na mwanamke msafi asiye na vito aliyesimama sehemu safi inayovutia yupi anaweza kuvuta umakini wa watu makini?

6. Ucheshi… haimaanishi uchekecheke kama mwendawazimu na kila mtu, ujirahisi kwa kila mtu... Mtu mcheshi ni msikilizaji mzuri, ni mtu asiyebeza wengine na kudharau, ni mtu asiye na mafumbo mafumbo na minuno ya ajabu ajabu.
Hata watu wakimya huweza kuwa wacheshi… kuna ucheshi na umapepe, ukimya na gubu! Tofautisha tabia hizi uendelee kuwa mzuri miaka kwa miaka!

7. Sauti ya kike…. Uzuri wa mwanamke upo katika sauti yake pia… Mungu alijua hii ni silaha kubwa sana ambayo wanawake wengi hawajui wameibeba. Kuongea kike hakumaanishi uongee kwa madeeeeko…ubane sauti au sijui ujipe kithethe… ipo namna ambayo mwanamke akiongea hata kama panya anatoboa salfeti la unga ataacha kwanza asikilize kazi ya Mungu!
Hujawahi sikia mtu anadata na sauti kabla hajamuona mtu?.... ndiyo ujue hata kama una bezi la home theatre…dada na bezi lako ongea ‘kike’…. sio chichichichichichichichichichiiiiiii anhaaa!

8. Ujasiri…. Ni uzuri ambao hauchuji asilani abadani!... ujasiri utakutoa katika mahusiano mabovu kwa kuwa unajiamini… utakupa roho ya kuyakabili matatizo na si kuyakimbia na kujirahisisha kwa mtu… ujasiri unakupa nguvu ya kusema hapana panapostahili kusema hapana na nguvu ya kujitafakari.
Ujasiri utakufanya wewe single mother usijione una mikosi…wewe ambaye hujabarikiwa ndoa usijione hufai… wewe ambaye umetoka kwa talaka ujione ndiyo basi tena… wewe ambaye mume anacheat ujione dhalili…. wewe ambaye unasita sita kuanza biashara au kutimiza ndoyo yako fulani usijione umechelewa... uzuri wa mwili hauna maana yoyote kama nafsi yako haina ujasiri!!
Hebu jivike uzuri huu kabla hujaenda kununua matako bandia kumvutia mtu! Kuna wakati watu wanadata na wanawake wanaojua nini wanataka pasipo kuyumbishwa ovyo. Anaanguka katika hili anasimama haraka kuendelea na maisha wakati wewe usiye na ujasiri bado unatangatanga hapo hapo.

9. Kujikubali ulivyo…. Ni uzuri ambao wengi hatuna… kujikubali haimaanishi ujiachie tu rafu rafu kisa unajikubali ulivyo … hapana kujikubali haimaanishi ukae na michunusi au usipake hata poda usoni… hulka ya kike ni kujipamba hata vitabu vya imani vimeonyesha hilo… jipambe wewe ni mwanamke bwana!... ila kuna vitu vya kimaumbile unapaswa kujikubali kwanza mfano ulemavu au shepu tu bovu…. Huwa nasikitika nikikutana na meseji za watu wanaomba ushauri wa kujibadili maumbile fulani kisa mume sijui bf anamwambia ajibadili… mpaka unaomba msaada it means mwenyewe hajajikubali!
hii inajumuisha na kuishi maisha yako halisi… maana mjini hapa mabinti wanadhani kushow off kuwa wanazijua pesa… au wanaishi maisha ya juu ni sehemu ya uzuri… trust me! unajiongezea stress utapendwa na utavutia hata ukiishi maisha yako halisi. Hutoyumbishwa na maneno/ mitazamo ya watu/jamii.

10. Hofu ya Mungu!... si jambo la mwisho ila ndio unatakiwa ubaki nalo kichwani. Ukiwa na hofu ya Mungu wewe ni mzuri kwa viwango vya hali ya juu mno. Utajipenda, utajiamini, utajikubali, utajiheshimu, utajisahihisha, utajipongeza, utaanguka utainuka, utasamehe, utajisamehe, utalia, utacheka, utapongeza, utapongezwa, utapata utapoteza, utasadia utasaidiwa na kadhalika ila mwisho wa siku utapata la kujitetea mbele za Muumba sio binadamu wenzio.
Anza kwanza na kujipa uzuri huu usiochuja, usiofubaa, usioisha kisha uone kama nafsi yako haitotulia! mengine mtaongeza wenyewe…neno langu si sheria..

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

Read More
      edit
Published 6/03/2017 04:30:00 PM by

MNYIKA ATOLEWA NJE YA BUNGE


DODOMA: Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika leo alisababisha kuzaazaa Bungeni  Dodoma baada ya kugoma kutoka nje ya Bunge alipoamuriwa na Spika Job Ndugai kutokana na kile kilichodaiwa kukataa kuketi kama alivyoamuriwa na kiongozi huyo wakati mijadala ikiendelea.
Chokochoko hizo ziliibuka baada ya Mbunge wa  Mvumi,  Livingstone Lusinde kudai kwamba wapinzani bungeni humo wanatetea wezi wa mchanga wa dhahabu.

Mnyika ilibidi asimame na kutoa mwongozo kwa kusema wao wapinzani sio wezi isipokuwa walichokuwa wakikisema ni kulalamikia mikataba mibovu ya madini ambayo imeingiwa na serikali na kusababisha kufikia hapa tulipo.
Wakati Mnyika akiendelea kumpa taarifa Lusinde, mbunge ambaye hajajulikana jina alisikika akisema kwa sauti ‘mwizi’, hali iliyomfanya Mnyika kumuomba spika amjuwe aliyemuita mwizi, hata hivyo, Spika Ndugai akawa anamsisitizia akae chini.
Alimuomba kukaa chini mara tatu lakini Mnyika hakutii ndipo Ndugai alipomuamuru atoke nje lakini pia hakutoka, hivyo akawaita askari wa bunge aliowaamuru waingie ndani na kumtoa nje kwa nguvu mbunge huyo kijana.
Kuona hivyo Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na yule wa Bunda, Ester Bulaya, waliingilia kati kuwazuia askari wa bunge kumtoa nje Mnyika, hali iliyoleta tafrani, hata hivyo, alitolewa na kwenye lango la kuingilia bungeni, alisukumwa na ‘kutupwa’ nje ya mjengo.
Spika alitangaza kumsimamisha Mnyika asihudhurie vikao vya bunge kwa wiki moja huku Ester Bulaya na Halima Mdee akisema wataandikiwa barua ili wakahojiwe na Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

CHANZO: GPL

Read More
      edit

Thursday, June 1, 2017

Published 6/01/2017 11:10:00 PM by

JAQUELINE WOLPER ALIMISI PENZI LA ALI KIBA


TAMU wa ubuyu ukae chini na umung’unye taratiiibu! Staa wa filamu za Kibongo asiyepungukiwa mbwembwe kwenye mapenzi, Jacqueline Wolper, amefunguka kuwa ilibaki kidogo tu aolewe na msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba kama wasingekuwa mastaa maishani mwao. lilizungumza na Wolper ambaye alidai kuwa penzi alilolikuta na kulipata kwa Kiba ni penzi ambalo hawezi kulisahau maishani mwake.
ASIMULIA PENZI LA KIBA LILIVYO

“Ni mtu mwenye upendo wa kweli, anajua kujali, anathamini na ninaamini moyo wangu ulimpenda kwa dhati.

WALIVYOKUTANA
“Sikumbuki ilikuwa mwaka gani, ninachokumbuka ilikuwa ni Mtaa wa Lindi uliopo Kariakoo wala sikumbuki nilienda kufanya nini siku hiyo.
MUDA WALIO-DATE
“Ni muda mrefu, maana imekuwa siku nyingi. Kipindi hicho wote hatukuwa na majina makubwa (mastaa) kama tuliyonayo sasa. Tulipendana na tulikuwa na matarajio makubwa mbeleni.
KUTENGANA KWAO

“Baada ya kuwa mastaa, kila mmoja akajiona mkubwa zaidi ya mwenzake, ndoto na matarajio yote yakatoweka, polepole penzi likaanza kuyeyuka na hatimaye kufa kabisa, ingawa hatujakoseana kihivyo kiasi cha kushindwa kusalimiana kama wengineo. Naamini tulipendana lakini usupastaa ukazidi nguvu ya penzi letu.

ANACHOKIKUMBUKA KWA KIBA
“Mengi nakumbuka, kubwa ni upole wake pamoja na unyenyekevu, hii ni tofauti na wanaume wengine ambao nimewahi kukutana nao.
KUHUSU KURUDIANA NAYE

“Swali hilo naomba nisilijibu na ibaki kuwa siri yangu, ingawa ni muda mrefu na kila mtu ana mambo yake mengi zaidi,” anasema Wolper.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

CHANZO: GPL
Read More
      edit
Published 6/01/2017 08:25:00 PM by

ALIYEFUNGWA JELA KWA KUFANYA NGONO NA MWALIMU



Mwanamume amewasilisha kesi mahakamani akitaka atengane na mkewe ambaye ni mwalimu wake wa zamani aliyefungwa kwa kufanya nae ngono akiwa na umri wa miaka 12.

Vili Fualaau, ambaye sasa ana umri wa miaka 33, amewasilisha nyaraka za kesi kwenye mahakama ya jimbo la Washingto, Marekani , akitaka ndoa yake ya miaka 12 na Bi Mary Kay Fualaau (zamani akijulikana kama Letourneau), mwenye umri wa miaka 55 ivunjwe.

Bi Fualaau aliolewa akiwa na umri wa miaka 34- akiwa na watoto wanne alipoanza uhusiano wa kindoa na Vili Fualaau.

Baada ya kutumikia kufungo cha jela , wawili hao walioana kwa siri mnamo mwaka 2005.

Bwana Fualaau aliwasilisha kesi ya kuachana nae mapema mwezi huu bila kuelezea sababu ya uamuzi wake huo, ilibainika.

Katika ombi lake kwa mahakama , aliandika kwamba iwe yeye wala mkewe hakuna aliye na mali wala mkopo, vimeripoti vyombo vya habari vya marekani.

Bwana Fualaau, ambaye ana watoto wawili na mkewe , pia alisema kwa sasa hawamtegemei tena, akiomba wawili hao wagawanywe kile walichoweza kutafuta pamoja kwa haki.

Mkewe hajatoa kauli yoyote kwa umma juu ya uamuzi wa mumewe.

Bwana Fualaau alikuwa darasa la sita alipoanza uhusiano wa kimapenzi mjini Seattle mwaka 1996.

Akiwa mwalimu Bi Fualaau alikamatwa mwaka 1997 alipokuwa na mimba ya mtoto wao wa kwanza ,na baadaye alikiri kufanya kosa la ubakaji wa mtoto.

Huku yake ya kwanza ya miezi sita ilipunguzwa baadae na kuwa ya miezi mitatu chini ya misingi kwamba angelikosa mawasiliano na mwanafunzi wake wa zamani.

Lakini katika kipindi cha wiki kadhaa wawili hao walikamatwa wakifanya ngono, na akafungwa miaka saba.


 Alipata mtoto wao wa pili.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa


CHANZO: KALUNDE BLOG
Read More
      edit