Saturday, June 3, 2017

Published 6/03/2017 05:22:00 PM by

UZURI NA MVUTO USIOCHUJA


Upo uzuri ambao hauchuji, haufifii na wala hauna madhara… Upo uzuri ambao hauhitaji kutumia nguvu kubwa kumvuta mtu wa jinsia nyingine au wenzio.
Upo uzuri ambao mpaka kuzeeka kwako bado utakufanya uendelee kuonekana mzuri na kujiona wewe ni mzuri mnooo… uzuri usio na majuto yoyote wala kikomo!
 Hoja mbili tatu za kukukumbusha kuhusu uzuri huo!
1. Elimika!..... Ukielimika utastaarabika mwanamke, utajishughulisha! Utashika chenji zako mwenyewe mkononi… Utakuwa na upeo, utajua dunia inakwenda vipi.
Kuna watu wanasoma ila hawaelimiki. Wewe kuwa tofauti soma uelimike! Ukielimika huwezi kuburuzwa ovyo na mtu au makundi ya watu. Utakuwa na msimamo wako binafsi kwa kuwa utajua nini ni nini. Ukielimika utajishughulisha na utashika pesa yako mwenyewe hata kama ni kidogo kiasi gani, ni ya kwako! 

2. Roho nzuri…. Haijalishi una makalio makubwa kiasi gani au u mweupe kama karatasi… au una sura ya kuvutia namna gani ama umebeba mkoba wa laki ngapi.
Kama roho yako imejaa chuki za chini chini, husda, wivu, vinyongo, misengenyo, vijicho, kufurahia matatizo ya wenzio, kuharibia wengine na unafiki!....Woman you are ugly! Roho nzuri ni uzuri usiochuja hata mbele za Mungu!

3. Tabasamu la upendo… huu ni uzuri ambao wengi wetu tunauchukulia poa sana. Ni uzuri usio na gharama yoyote ile.
Salimia watu kwa tabasamu la upendo bila kujali umri, rangi, hali zao kiuchumi au vyeo vyao kazini. Huwezi jua tabasamu lako la upendo litakurudishia baraka gani mbele ya safari pasipo wewe kujua. Huwezi jua salamu yako yenye tabasamu inampa nani hali ya kujiona anathaminika. Utunze uzuri huu kwa gharama yoyote ile. Ni tiba kwako na wengineo!

4. Kauli safi!... kuna watu wanadhani kutukana ni ujanja, kuongea sana ovyo ovyo ni umjini... kuongea kimipasho kila saa ni ushujaa…. Kujua matusi ya nguoni ndio kwenda na wakati… hata wakati ambao mtu amekukalfisha nafsi vibaya sana, unapoweza kumjibu pasipo tusi hata moja la nguoni wewe ni mzuri! Mzuri sana!
Unapoporomosha matusi kuyajibu matusi, unajivunjia heshima, unapoteza uzuri wako! Na hakika unaweza kumchoma adui yako kwa jibu safi zaidi kuliko jibu kali la matusi kwa kuwa nia ya mtu anayekuumiza ni kuona umeumia na kujibu tusi kunadhihirisha amekuweza!

5. Usafi…. Ni uzuri usiochuja kabisa! Utazeeka nao, utawavutia watu popote na wakati wowote ule. Usafi aina zote ni silaha kubwa sana. Hata wewe unapokutana na mtu nadhifu anayeweka mazingira yake katika hali nadhifu lazima utahisi kuvutiwa naye.
Hii inajumuisha kuikubali ngozi yako na kuiweka nadhifu bila kuikwangua kwangua. Mwanamke mrembo ambaye amejipamba vito ila kasimama kwenye mazingira machafu na mwanamke msafi asiye na vito aliyesimama sehemu safi inayovutia yupi anaweza kuvuta umakini wa watu makini?

6. Ucheshi… haimaanishi uchekecheke kama mwendawazimu na kila mtu, ujirahisi kwa kila mtu... Mtu mcheshi ni msikilizaji mzuri, ni mtu asiyebeza wengine na kudharau, ni mtu asiye na mafumbo mafumbo na minuno ya ajabu ajabu.
Hata watu wakimya huweza kuwa wacheshi… kuna ucheshi na umapepe, ukimya na gubu! Tofautisha tabia hizi uendelee kuwa mzuri miaka kwa miaka!

7. Sauti ya kike…. Uzuri wa mwanamke upo katika sauti yake pia… Mungu alijua hii ni silaha kubwa sana ambayo wanawake wengi hawajui wameibeba. Kuongea kike hakumaanishi uongee kwa madeeeeko…ubane sauti au sijui ujipe kithethe… ipo namna ambayo mwanamke akiongea hata kama panya anatoboa salfeti la unga ataacha kwanza asikilize kazi ya Mungu!
Hujawahi sikia mtu anadata na sauti kabla hajamuona mtu?.... ndiyo ujue hata kama una bezi la home theatre…dada na bezi lako ongea ‘kike’…. sio chichichichichichichichichichiiiiiii anhaaa!

8. Ujasiri…. Ni uzuri ambao hauchuji asilani abadani!... ujasiri utakutoa katika mahusiano mabovu kwa kuwa unajiamini… utakupa roho ya kuyakabili matatizo na si kuyakimbia na kujirahisisha kwa mtu… ujasiri unakupa nguvu ya kusema hapana panapostahili kusema hapana na nguvu ya kujitafakari.
Ujasiri utakufanya wewe single mother usijione una mikosi…wewe ambaye hujabarikiwa ndoa usijione hufai… wewe ambaye umetoka kwa talaka ujione ndiyo basi tena… wewe ambaye mume anacheat ujione dhalili…. wewe ambaye unasita sita kuanza biashara au kutimiza ndoyo yako fulani usijione umechelewa... uzuri wa mwili hauna maana yoyote kama nafsi yako haina ujasiri!!
Hebu jivike uzuri huu kabla hujaenda kununua matako bandia kumvutia mtu! Kuna wakati watu wanadata na wanawake wanaojua nini wanataka pasipo kuyumbishwa ovyo. Anaanguka katika hili anasimama haraka kuendelea na maisha wakati wewe usiye na ujasiri bado unatangatanga hapo hapo.

9. Kujikubali ulivyo…. Ni uzuri ambao wengi hatuna… kujikubali haimaanishi ujiachie tu rafu rafu kisa unajikubali ulivyo … hapana kujikubali haimaanishi ukae na michunusi au usipake hata poda usoni… hulka ya kike ni kujipamba hata vitabu vya imani vimeonyesha hilo… jipambe wewe ni mwanamke bwana!... ila kuna vitu vya kimaumbile unapaswa kujikubali kwanza mfano ulemavu au shepu tu bovu…. Huwa nasikitika nikikutana na meseji za watu wanaomba ushauri wa kujibadili maumbile fulani kisa mume sijui bf anamwambia ajibadili… mpaka unaomba msaada it means mwenyewe hajajikubali!
hii inajumuisha na kuishi maisha yako halisi… maana mjini hapa mabinti wanadhani kushow off kuwa wanazijua pesa… au wanaishi maisha ya juu ni sehemu ya uzuri… trust me! unajiongezea stress utapendwa na utavutia hata ukiishi maisha yako halisi. Hutoyumbishwa na maneno/ mitazamo ya watu/jamii.

10. Hofu ya Mungu!... si jambo la mwisho ila ndio unatakiwa ubaki nalo kichwani. Ukiwa na hofu ya Mungu wewe ni mzuri kwa viwango vya hali ya juu mno. Utajipenda, utajiamini, utajikubali, utajiheshimu, utajisahihisha, utajipongeza, utaanguka utainuka, utasamehe, utajisamehe, utalia, utacheka, utapongeza, utapongezwa, utapata utapoteza, utasadia utasaidiwa na kadhalika ila mwisho wa siku utapata la kujitetea mbele za Muumba sio binadamu wenzio.
Anza kwanza na kujipa uzuri huu usiochuja, usiofubaa, usioisha kisha uone kama nafsi yako haitotulia! mengine mtaongeza wenyewe…neno langu si sheria..

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

      edit