Thursday, December 14, 2017

Published 12/14/2017 09:30:00 PM by with 0 comment

USIKATE TAMAA KWA SABABU YA KUACHWA


Mungu ni mwema na mwenye upendo wa dhati kwetu sote kwa yeye kutuunganisha na kuwa kitu kimoja kupitia #Mi&U. Nikushukuru wewe ambaye umekuwa sehemu ya #Mi&U tangu kuanzisha hadi sasa. Najua kuna mengi ambayo unayapitia katika maisha yako ya kila siku yawe ya mapenzi au kawaida.

Vivyo hivyo hata Mi&U inapitia mambo na changamoto mbalimbali katika kujiimarisha zaidi. Kuna wakati unatokea huduma zetu ambazo zilikufanya ukajiunga nasi zinalegalega kwa sababu maalumu lakini hatuwezi kuanguka hata kama tutayumba kwa myumbo mkubwa na mkali. Hata wewe pia kwenye maisha yako ya kazini, shuleni, ibadani, biasharani na hata mapenzi umekuwa na changamoto, maumivu, mateso na majonzi ya kila aina.

Nimepata nafasi hii kwa kudra za Mwenyezi Mungu sina budi kukusihi kuendelea kupambana pamoja na kila aina ya myumbo ambao umekuwa ukikutana nao. Mapenzi ndiyo hasa yanayoongoza kwa kukuyumbisha kwa kipindi fulani, lakini kama mwanaMi&U ambaye umekuwa ukishiriki nasi katika mada, maoni na ushauri mbalimbali, usikubali kuyumba kwa sababu ya mapenzi. Jipe imani kuwa Mungu yuko upande wako wakati ukijipigania na yeye pia anakupigania.

Usikate tamaa wewe ambaye umeachwa na mpenzi, mchumba au mwenza wako kwa namna yoyote ile, iwe kakutelekeza na familia au lah, iwe kakuacha na ujauziti anahudumia au ahudumii, usikubali kukata tamaa kamwe. Naliona sononeko lako wewe mwanamke ambaye umefikwa na mumeo au mkeo, umelia, sasa imetosha acha maisha yaendelee kwani mapito hayo yaliwekwa katika maisha yako ili uyashinde na uingine katika nchi ya ahadi yenye mito ya maziwa na asali lakini kama utashindwa basi watu watakucheka, watakudharau, hata yule ambaye amekuacha utakuwa umempa kichwa na kujiona kuwa bila yeye huwezi kuishi lakini ukweli ni kwamba unaweza kuishi.

 Nakushuruku wewe mwanamke ambaye umetelekezwa na mumeo lakini umekubaliana na ukweli na unapambana na hali yako kuhakikisha unawasomesha watoto wako kwa uchungu na matesio makali lakini nakwambia Mungu hawezi kukunyima kila kitu.


 Kuna mateso na changamoto ambazo unaweza ukawa unapewa ili kupimwa ni kwa namna gani akili uliyopewa inaweza kufanya kazi katika maisha yako. Unapimwa kungaliwa ni kwa namna gani unaweza kuwa mvumilivu na mwenye kukabiliana changamoto mbalimbali. #USIKUBALI #KUSHINDWA #KUKATAA #TAMAA #KUJIONA #DHAIFU AU #HUWEZI

Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785. Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa Na.M&U

Read More
      edit
Published 12/14/2017 10:00:00 AM by with 0 comment

MWAKA UNAISHA UMEGUNDUA MAKOSA YAKO!


Mwaka ndugu ndiyo unakaribia kuisha, yamkini ulikuwa na majukumu au mipango mingi sana katika maisha ya penzi lako. Je, mipango yako imeenda kama ulivyokuwa umepanga? Kama ilienda aua haijaenda sawa mshukuru Mungu. Kwani bado kakujaliwa pumzi yake.

Kama mipango haikwenda sawa, jiulize kwa nini? Nani chanzo au sababu ya mipango yako kufeli? Je, ni wewe, ndugu, mpenzi, mfanyakazi au mwanafunzi mwenzako, au ni akili yako?

Kama ni wewe, kwa nini na kama ni yule kwa nini? Vipi kuhusu mpango wako wa kuoa au kuolewa, umefikia wapi? Nini na nani chanzo cha migogoro katika penzi lako?
Kwa mwaka 2017 changamoto zipi kubwa na mbaya ambazo umepizipitia? Je, ni jambo lipi lililokukwaza na kukusumbua katika mapenzi kwa mwaka huu?



Katika ugomvi na mwenza wako nani amekuwa chanzo, ni wewe au yeye? Ni kwa kiasi gani umepambana kuepukana na changamoto hizo?


Jifunze changamoto na mambo yote mazuri ambayo umeyapitia kwa mwaka 2017 kisha jirekebishe kwa mwaka 2018. Usikate tamaa kwa sababu ulifeli sana kwenye biashara, masomo, kazini au penzi lako bali mshukuru Mungu kwa kukuonesha upande wa pili wa maisha ya kazi, shule au mapenzi. Kwa mwenye swali au maoni, karibu DM AU #WhatsAPP +255679979785.
 
Jipange kuuanza mwaka kwa mapambano mapya kabisa, jiepushe na kisirani, maamuzi yasiyokuwa na busara. Kuhamaki na kuchukua hatua.
Kama taasisi tunashukuru uwepo wako toka kuanzishwa kwake,  changamoto na hapa tulipo.
Taasisi ya Mimi na Uhusiano "Mi&U" inakutakiwa KHERI YA MWAKA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA 2018.

#ACHAWOGATHUBUTU#MIMINAUHUSIANO#

Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Read More
      edit
Published 12/14/2017 12:00:00 AM by with 0 comment

NITUMIE MBINU ZIPI KUINJOYI KIBAMIA CHA MUME WANGU!


Naomba ushauri wako, mimi ni mwanamke ambaye nimeolewa hivi karibuni, ila kabla ya ndoa sikuwa nimekutana kimwili na mume wangu.


Baada ya kufuata taratibu zote za kwetu alinioa.Siku ya kwanza nakutana naye faragha nilishtuka sana kuona ana #KIBAMIA nikapotezea kwa kujua atakuwa anajua kukitumia vizuri.
 
Kiukweli siku zimekuwa nyingi naona kama siinjoyi chochote kwa kibamia chake. Naipenda sana ndoa yangu. Je. Nifanyeje au nitumie staili ili niinjoyi #KIBAMIACHAMUMEWANGU.

#ACHAWOGATHUBUTU#MIMINAUHUSIANO#


Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Read More
      edit

Friday, October 6, 2017

Published 10/06/2017 06:06:00 AM by with 0 comment

HATA COMPUTER HAIZIDI AKILI ZAKO-2!

Jana nilianza kuzungumzia ni kwa jinsi gani akili yako inaweza kujibu maswali magumu yote ambayo unayo au yanakusumbuka.

Ili kupata majibu au mafanikio ya jambo lolote ni lazima uumize kichwa kwa maana nyingine lazima ufikirie utatokaje, au utafanikiwa kivipi.

Watu wengi sana ni wavivu wa kufikiri na niwasemaji sana huku wanaofikiri ni wachache ni watu wakutenda.

Kama umefikiria sana lakini bado hujapata jibu la swali au changamoto inayokusumbua basi pumzika kufikiri kwa nguvu na akili nyingi. Relax.

Namaani s a ukiona umeshindwa kuendelea kuwaza au kupata majibu achana nayo, kalale, pumzika kisha endelea kujiuliza kwa nini # MIMI NI MASKINI, #KWA NINI MIMI SIJASOMA, #KWA NINI NIMESOMA LAKINI SINA AJIRA WALA #SIJAAJIRIWA, #KWA NINI NAKULA #MLO MMOJA#KWA NINI NAACHWA KILA SIKU#

Endelea kujiuliza kuhusu magumu na mapito yote ambayo unayoyapitia. Kisha jiulize swali au maswali hayo magumu kwa wepesi kwa mfano:
Hivi hakuna watu wanaokula milo mitatu tena milo inayostahili kwa maana ya kujenga mwili-WAPO. Hivi hakuna maskini aliyezaliwa hana kitu lakini leo anatamba au ana miliki pesa kibao-YUPO. Hivi hakuna mtu ambaye hakusoma kama wasomi wengine lakini leo ni tajiri na anaheshimika-YUPO/WAPO.

Hivi hakuna mwanamke ambaye alitelekezwa na mzazi mwenzake na leo anasongesha maisha yake mwenyewe bila huyo mwenza tena wakati mwingine maisha yake ni bora kuliko alivyokuwa na mwenza wake-YUPO.
Hivi hakuna mtu ambaye alikuwa na pesa lakini akafilisika ila hakukataa tamaa na leo hii amefanikiwa tena. Jibu-/YUPO.

Hivi hakuna binti ambaye amekuwa akihitaji kuolewa kwa muda mrefu lakini alipomlilia Mungu akamkutanisha na mume mwema-YUPO.

Hivi hakuna MJANE /MGANE ambaye aliumizwa na kifo cha mwenza wake lakini mwisho wa siku akakubali ukweli na leo hii anasomesha watoto wake  yeye mwenyewe-YUPO TENA JIRANI YAKO. Sasa kama wao wameweza kwa nini wewe ushindwe. Jiulize hapo utakuwa ba shida kubwa sana.

Sasa wewe endelea kusubiri miujiza bila kujishughulisha utaona miujiza ya kufa maskini.

#ACHAWOGATHUBUTU#MIMINAUHUSIANO#

Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com

Read More
      edit

Thursday, October 5, 2017

Published 10/05/2017 06:12:00 AM by with 0 comment

HATA COMPUTER HAIZIDI AKILI ZAKO-1!


Ukimuuliza mtu kitu gani kina akili nyingi na zenye kufanya kazi zaidi ya computer utaambia hakuna zaidi yake.

Kwa sababu computer inaendesha mashine, inatengeneza bunduki, inatengeneza mitambo, makombora, ndege na vitu vingi unavyoviona na kuvitumia kila siku.

Lakini kwa nini nasema hata computer haina akili za kukuzidi ni KWA SABABU COMPUTER IMETENGENEZWA NA MTU, kumbe wewe kwa akili yako unayoiona ni ndogo, haina akili, haina ufumbuzi wa maswali na matatizo yako UNAKUWA UNAIKOSEA, HUJITENDEI HAKI.

AKILI YAKO VYOVYOTE ILIVYO iwe haijaenda shule, iwe ina elimu ndogo, elimu ya kati, chuo na kadhalika  lakini BADO NDANI YAKE INA AKILI ambazo unaweza kuzitumia kuishi mjini, kukifanya uende shule, kukufanye upate maendeleo, kukufanya ufikie maendeleo au ukamilishe MAONO YAKO.
Kila swali au tatizo lako linalilokutatiza lina jibu NDANI YA AKILI YAKO.

Hiyo computer yenyewe imewekewa/imelishwa hayo majibu yote ambayo umekuwa ukiiuliza na kukupa majibu ina maana kuna watu ambao waliumiza kichwa na kupata majibu kisha kuyaweka kwenye computer.

Kwa  nini wewe huwezi hata kidogo kuumiza kichwa kwa jambo fulani ambalo linakutatiza, unaendekeza kulalamika. #ACHAKULALAMIKA#ACHAKULIA#THUBUTU-M&U#

Pikicha kichwa chako, nyanyua juu uso wako kama unaangalia juu kwenye mawingu au kwa imani, unaangalia ANAPOISHI MUNGU kisha endelea kufikiria. Tembea tembea ukitoka pointi A unaenda B unarudi tena A ukiwa kama umechanganyikiwa, gonga ukuta au meza kwa taratibu, au jifyonze sana., fyuuuuuuuu! Kote uko ukiwaza kutafuta majibu ya maswali magumu yanayokusumbua akilini na maishani mwako.

#ACHAWOGATHUBUTU#MIMINAUHUSIANO#

Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com



Read More
      edit

Thursday, September 28, 2017

Published 9/28/2017 09:05:00 PM by with 0 comment

USHAURI WAKO: BOSI ANAMUACHA MKEWE CHUMBANI ANAKUJA KWANGU
Mimi ni binti ambaye ninafanya kazi za ndani.Nilishangaa nimejikuta nampenda bosi wangu wa kiume bila yeye kujua lakini kumbe hata yeye ananipenda. Baadaye tuliamua kuingia kwenye uhusiano wa mapenzi, kila siku usiku bosi anamuacha mkewe kitandani na kuja kwangu kupata raha, ninampenda sana na yeye ananipenda. #Miminauhusiano#Elyenekemilemne# Kwa ushauri wa Uhusiano na Ujasiriamali, jiunge na Mi&u WhatsApp :0679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Read More
      edit

Friday, September 22, 2017

Published 9/22/2017 12:27:00 PM by with 0 comment

MCHUNGAJI ANANITAKA, ETI NIKIZINI NAYE MUNGU ATATENDA!

Habari ndugu, naomba ushauri wenu kuna mchungaji kijana anaisumbua na kunikosesha raha kwa kunisumbua eti niwe naye kimapenzi.

Machungaji huyo anataka tukitane sehemu tulivu tuzungumze nikimwambia tuongelee kanisani anakataa.
Eti ananiambia ana maono na mimi nikimkubali na kuzini naye Mungu atatenda. Nimechoka kwa kweli, mtu ambaye nilimuamini kuwa ni msaada wa kunirudisha kiimani leo anashawishi tuzini.

Ungekuwa wewe ungefanyaje kwa hali hii.

#Miminauhusiano#elynekemilembe#

Kwa ushauri wa UJASIRIAMALI na UHUSIANO jiunge na Mi&u WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano  Tutwitee au tembelea www.miminauhusiano.blogspots.com

Read More
      edit

Thursday, September 21, 2017

Published 9/21/2017 07:17:00 PM by with 0 comment

NATAMANI NITILIMIZE NDOTO ZANGU

Hongera Kwa Kazi Kaka Gabriel,,naomba Nikupongeze Kwa Kazi Nzuri Unayoifanya M&U Hasa Machapisho  Kwa Waliokata Tamaa Kabisa Ya Maisha,,binafsi Nilikata Tamaa Baada Ya Kupitia Mikasa Ya Majaribu Magumu Sana,,naamini Mungu Anakutumia Haswa Kuganga Mioyo Ya Watu,,ombi Langu Nisaidie Niyapate Niwe Nayapitia Mara Kwa Mara,,kiukweli Natamani Sana Nitimize Ndoto Zangu,,ila Nimeumizwa Sana Moyo.Asante.

Read More
      edit

Wednesday, September 20, 2017

Published 9/20/2017 07:10:00 AM by with 0 comment

UNA KILA SABABU YA KUFURAHI BILA KUJALI MATATIZO ULIYONAYO

Wakati wewe unalia huna kazi ya maana basi kuna wengine hawana kabisa.

Wakati wewe unalia kwa sababu mwenza wako kakuacha au mmeachana kuna wengine hata wadawa hawana.

Wakati wewe unashinda kwa kula mlo mmoja  kuna mwingine anakula mlo mmoja kwa siku kadhaa.

Wakati wewe una afya njema na mathubuti kuna wengine wamelazwa hospitalini wakiwa hawajitambui.

Kwa hayo machache huna sababu ya kutokufurahia maisha yako.

Kwa ushauri wa Uhusiano na Ujasiriamali, jiunge na Mi&u WhatsApp :0679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano

Read More
      edit
Published 9/20/2017 06:54:00 AM by with 0 comment

KAMA PENZI LIMEFIKA MWISHO KUBALI UKWELI!

Mwanamke mzuri, tabasamu murua, meno mazuri, meupe yaliyopangwa yakapangika.

Kwa nini ukate tamaa kumalizia safari yako kwa sababu uliyekuwa naye safarini kashindwa kuimaliza safari yenu. Ahadi ni kufika mwisho kama yeye kashindwa Pambana na hali yako.

Maisha yapo, komaa unaweza kuishi na kufanya mambo yako bila huyo uliyedhani ndiyo KILA KITU, NDIYO MAISHA YAKO, NDIYO UHAI WAKO, NDIYO KODI YAKO, NDIYO FURAHA YAKO, NDIYO NDOTO YAKO, NDIYO AMANI YA MOYO. Kama imefika mwisho basi imefika tu hata kaka utalia na kusaga meno.

Kwa maoni na ushauri wa Uhusiano jiunge na Mi&u WhatsApp:0679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano

Read More
      edit