Friday, August 26, 2016

Published 8/26/2016 10:30:00 PM by with 0 comment

AKICHEPUKA SINA WIVU NAYE WALA SIFURAHII FARAGHA YAKE


Mimi ni mama wa miaka 30 nina watoto 3 wote wa kiume, niliolewa nikiwa na miaka 18 naweza kusema sikuwa najitambua kihivyo.
 Nilijikuta nikikubali kuolewa  naye kwa sababu alinipata ujauzito kwa kuwa baba yangu alikuwa mkali na alikasirika sana nikaladhimika kuolewa tena kwa harusi kubwa sana yenye kila aina ya amshaamsha.

Mume wangu ana miaka 47 kwa sasa ninahisi alinioa nikiwa sina uhakika kama nilimpenda kwani sijawahi kusikia raha ya mapenzi nikiwa na mume wangu zaidi ya mateso. Kwa mtu ambaye unampenda wivu unakuwepo lakini kwangu wala sina na sijawahi hata kuwa na wivu naye.

Naweza kusema ninaishi naye kwa sababu ya hao watoto wangu niliozaa naye ila sina naye mapenzi ya dhati ingawa yeye ananipenda sana.


Nimefika sehemu nahisi kama hakuwa chaguo langu, kwani anaweza akalala nje  kwa siku kadhaa lakini hata siku moja sijawahi kumuuliza kuhusu hilo kiufupi simpendi tu sina furaha ya ndoa nipo nipo tu hata sijielewi kiukweli. Ninaomba ushauri wenu mimi mwanaM&U mwenzenu.
Read More
      edit
Published 8/26/2016 07:30:00 PM by with 0 comment

MWISHO WA MAJONZI KESHO KWENYE SEMINA

Nimechoka kuwa mtumwa wa kulia na kuteseka kwa mtu ambaye hana mapenzi ya dhati na mimi, na mwisho wa kutoa machoji yangu ni kesho kwenye SEMINA YA MIMI NA UHUSIANO. NAJUA TUKO WENGI TUNAOTESWA BASI UNGANA  NAMI KUHUDHURIA SEMINA HIYO NA UTAIONA MABADILIKO YAKE.


Read More
      edit
Published 8/26/2016 07:24:00 PM by with 0 comment

NAMNA YA KUFIKA KWENYE SEMINA KESHO:

Kwa yeyote anayetaka kufika kwenye semina popote alipo jijini DAR apande gari ambalo litamfikisha KITUO CHA SAYANSI- KIJITONYAMA, DAR akishuka ataona JENGO LA TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA BASI NYUMA YAKE NDIPO SEMINA ITAFANYIKIA. 


Niwashukuru wale wote ambao wamejisajiri au WAMELIPIA TIKETI ZAO kwa ajili ya semina ya KESHO KIJITONYAMA. 
TIKETI BADO ZINAPATIKANA UNAWEZA KULIPIA  KWENYE TIGO PESA AU M-PESA KWA NA. 0767207156 AU 0657486745  KISHA UNAPEWA NAMBA YA SIRI YA TIKETI NA KWA WALE WANAOTAKA KULIPIA GETINI WANAWEZA KUWAHI MAPEMA NA KUJIPATIA TIKETI YAO.

KARIBU NA MTAARIFU NA MWENZIYO

Read More
      edit

Thursday, August 25, 2016

Published 8/25/2016 07:37:00 PM by with 0 comment

KUACHANA NA WEWE SIYO KAMA NIMEKOSEA




Read More
      edit
Published 8/25/2016 03:45:00 PM by with 0 comment

MAREKANI-,MWANAFUNZI ATOZWA MILIONI 600 KWA KUMPACHIKA MIMBA MWALIMU

Mahakama moja ilimtunuku mwanafunzi Sh600 milioni kwa kumtia mimba mwalimu wake akiwa na miaka 16

–Mwalimu huyo alifungwa kwa mwaka mmoja lakini alikaa jela kwa miezi sita pekee. Binti wao ana miaka mitatu

Mwanafunzi mmoja California, Marekani, atatunzwa Sh600 milioni kwa kuhusika kimapenzi na mwalimu wake na kumtia mimba.

Mwalimu huyo Laura Whitehurst, 31, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo akiwa na miaka 16 ambapo alipata mimba na kumzalia binti miezi tisa baadaye.

Hukumu hiyo ilitolewa miaka mitatu baada ya Whitehurst kutambulika kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi wake.

Mahakama iliambiwa kuwa mwalimu huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wengine wawili ambao hawakutambulishwa.

Ilisemekana mwalimu huyo alikuwa akishiriki ngono darasani akiwa na mvulana huyo, na nyumbani kwake kwa mwaka mmoja kabla ya tukio hilo kujulikana.

Mwanafunzi huyo alidai kuwa usimamizi wa shule yake, Redlands Unified School District, ulikuwa ukijua kuhusu uhusiano huo lakini ukakataa kuchukua hatua yoyote.

“Ushahidi unaonyesha kuwa usimamizi ulijua vyema kuhusiana na suala hilo lakini ukakataa kuchukua hatua yoyote,” alisema wakili wa mwanafunzi huyo Vince Finaldi.

Whitehurst alifungwa mwaka mmoja 2013 kuhusiana na kisa hicho lakini alikaa jela kwa miezi sita pekee kwa kuonekana kuwa na tabia njema.
Read More
      edit
Published 8/25/2016 03:34:00 PM by with 0 comment

MARA-UKIBAINIKA KUMPA UJAUZITO MWANAFUNZI KUPEWA KIBANO KIZITO

 Serikali wilayani Serengeti Mkoani Mara imeamua kupambana na wanaume waliowakatishia masomo wanafunzi wa kike zaidi ya 42 wa shule za msingi na sekondari kwa kuwapa ujauzito.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu katika mkutano wake na wakazi wa mji wa Mugumu alimwagiza kamanda wa polisi wilayani humo kuwakamata wanaume wanaodaiwa kuwapa ujauzito wanafunzi hao na kuwafikisha mahakamani.

Pia, aliagiza wazazi wa wanafunzi hao ambao wanawalinda waliowapa ujauzito wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

“OCD kamata wazazi na watoto ambao watajaribu kuficha ukweli na wafikishwe mahakamani kwa kuwa kumeibuka mtindo wa wazazi kushirikiana na watoto na anapoulizwa aliyempa mimba hamjui, wenye majibu kama hayo kamata wote,” alisema Babu.
Read More
      edit
Published 8/25/2016 03:22:00 PM by with 0 comment

MKE AMFUMANIA MUMEWE NA KUMPA ADHABU KALI!

Mwanamke mmoja Nairobi alifika nyumbani na kumpata peupe mumewe akila uroda na kimada katika kitanda chao bila aibu!

–Asimulia katika jukwaa moja mtandaoni alivyowapa adhabu tosha kwa kumpiga picha kimada na kuzituma kwa wanaume wote aliokuwa nao kwenye Whatsapp

Mwanamke huyo alirauka kama ilivyo kawaida yake kutayarisha watoto waende shule. Kisha, akamtengenezea kiamsha kinywa mumewe na kuondoka kuelekea kazini.

Mumewe alikuwa likizo hivyo wakakubaliana ndiye atakayewachukua watoto jioni.
Akichapa kazi alikuwa akihisi ndivyo sivyo lakini akapuuza.

Ilipofika saa za kula akaondoka na wenzake kwenda kutafuta chakula. Kwa bahati mbaya akajikwaa na kupata jeraha lililomzuia kuendelea na kazi.

Baada ya kujaribu kumpigia mumewe bila kufanikiwa, alikimbia nyumbani na kumpata mumewe kitandani na mwanamke mwingine. .

Hakuamini macho yake kumuona mumewe wa miaka mitano amemkunja kimada wanakula uroda katika kitanda chao chao cha ndoa.

Hasira zikampanda akaondoka haraka kwenda kutafuta silaha kali awafunze adabu huku machozi yakimtiririka.

Haraka mke wa nyumba akapata jawabu: akampia picha nyingi kimada huyo na kuzituma mfululizo kwa kila mtu ambaye mumewe alikuwa amemjumuisha katika Whatsapp yake, ikiwemo wafanyakazi wenzake.

Je, unaunga mkono adhabu ambayo mama huyo alimpa mumewe?
Read More
      edit
Published 8/25/2016 03:04:00 PM by with 0 comment

MIMI NINA NGUVU ILA MAPENZI YANA NGUVU ZAIDI YANGU



USIKOSE JUMAMOSI HII KWENYE SEMINA NAWE PIA JITAHIDI UPATE TIKETI YAKO ILI UEPUKANE NA MATESO YASIYO YA LAZIMA KWENYE MAPENZI.
KWANI KUNA MAISHA NJE YA MAUMIVU YA MAPENZI NA JENGA UJASIRI SIMAMA TENA ITANIFANYA NISIMAME TENA IMARA NI KWA SH. 7000/= LIPIA TIKETI YAKO KWA TIGO PESA AU M-PESA NA. 0767207156 AU 0657486745 NA UTAPEWA NAMBA YA SIRI YA TIKETI YAKO.
Read More
      edit

Wednesday, August 24, 2016

Published 8/24/2016 07:11:00 PM by with 0 comment

MADA YA MAHABA YA LEO USIKU





Read More
      edit
Published 8/24/2016 12:54:00 PM by with 0 comment

USHAURI WAKO:MKOSAJI NI YEYE MSAMAHA NIMUOMBE MIMI, INAKUJA KWELI


Kaka nina mpenzi wangu ambaye nimedumu naye kwa miaka mitatu mpaka sasa, katika kipindi chote hicho tumekuwa tukielewana sana lakini hivi karibuni imetokea kutoelewana.
Mpenzi wangu ni kapteni wa feri moja hapa nchini na mimi pia ni karani katika hiyo feri naweza kusema tunafanya kazi wote, yey huwa na zamu ya kulala kazini lakini walalala upande wa pili wan chi kavu kuna siku nilimuomba tukalale ng’ambo wote  akakataa vibaya na kudai kuwa anaumwa.

Nilimwambia ninataka nikalale tu wala sitamsumbua kuhusu ndi ndi ndi lakini bado aliendelea kukataa kabisa nisiende kulala wote  nikamwambia kama hataki basi anipe sababu ya msingi ambayo itanifanya niridhisha lakini hakuwa na sababu nyingine zaidi ya kusema kuwa anaumwa. Niliondoka kwa hasira nikiwa nimenua na hata usiku mwema siku hiyo sikumtakiwa. Kwa kawaida asubuhi huwa tunauliza nini tunywe au tule tukikubaliana tnafanya tulichokubaliana lakini kulivyokucha siku hiyo hatukujadiliana
lakini tangia siku hiyo mawasiliana yetu yakawa ni yakusuasua labda nimtumie ujumbe wa kawaida t.
Baba yake anaumwa huwa ninamtumia ujumbe wa kumuuliza kuhusu maendeleo ya baba ananijibu baada ya hapo kimya siku nzima inaisha bila kutumia ujumbe wala kupigiana simu.

Lakini kutoka moyoni mwangu kaka G naumia kwani nampenda sana mpenzi wangu na sijui ndiyo kusema mapenzi yetu yameisha au inakuaje? Ni kweli mimi nilifanya makossa kumuuomba tukalale wote au nini tatizo langu jamani?

Kuna wakati natamani nimuombe msamaha ingawa najua kabisa kuwa sina makosa basi yeye ndiye mwenye kosa, au natakiwa nimbembeleze wakati nina hisi yeye ndio amenikosea? Naomba ushauri wako.  
Read More
      edit