Kaka nina mpenzi wangu ambaye nimedumu naye kwa miaka mitatu mpaka sasa, katika
kipindi chote hicho tumekuwa tukielewana sana lakini hivi karibuni imetokea
kutoelewana.
Mpenzi wangu ni kapteni wa feri moja hapa nchini na mimi pia ni karani
katika hiyo feri naweza kusema tunafanya kazi wote, yey huwa na zamu ya kulala
kazini lakini walalala upande wa pili wan chi kavu kuna siku nilimuomba
tukalale ng’ambo wote akakataa vibaya na
kudai kuwa anaumwa.
Nilimwambia ninataka nikalale tu
wala sitamsumbua kuhusu ndi ndi ndi lakini bado aliendelea kukataa kabisa
nisiende kulala wote nikamwambia kama
hataki basi anipe sababu ya msingi ambayo itanifanya niridhisha lakini hakuwa
na sababu nyingine zaidi ya kusema kuwa anaumwa. Niliondoka kwa hasira nikiwa
nimenua na hata usiku mwema siku hiyo sikumtakiwa. Kwa kawaida asubuhi huwa
tunauliza nini tunywe au tule tukikubaliana tnafanya tulichokubaliana lakini
kulivyokucha siku hiyo hatukujadiliana
lakini tangia siku hiyo mawasiliana yetu yakawa ni yakusuasua labda
nimtumie ujumbe wa kawaida t.
Baba yake anaumwa huwa ninamtumia ujumbe wa kumuuliza kuhusu maendeleo ya
baba ananijibu baada ya hapo kimya siku nzima inaisha bila kutumia ujumbe wala
kupigiana simu.
Lakini kutoka moyoni mwangu kaka G naumia kwani nampenda sana mpenzi
wangu na sijui ndiyo kusema mapenzi yetu yameisha au inakuaje? Ni kweli mimi
nilifanya makossa kumuuomba tukalale wote au nini tatizo langu jamani?
Kuna wakati natamani nimuombe msamaha ingawa najua kabisa kuwa sina
makosa basi yeye ndiye mwenye kosa, au natakiwa nimbembeleze wakati nina hisi
yeye ndio amenikosea? Naomba ushauri wako.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.