Monday, February 12, 2018

Published 2/12/2018 01:32:00 AM by with 0 comment

KWA NINI NAWACHUKIA WANAUME-4


Nilipofika nikamkuta ana mtoto mchanga kabeba, akaniambia mshike huyu mtoto twende nyumbani nikaogopa, akanibembeleza nikamshika tukaondoka mpaka nyumbani. Akaniambia kuwa alioa mwanamke mwingine sasa wamegombana na yule mwanamke akamsusi mtoto, alichofanya ni kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na kupewa RB.



Nikaanza kumlea mtoto hadi akafikisha miaka 2 ndiyo mama yake akaja kumchukuwa mtoto wake, mume wangu akaenda kumchumbia mwanamke aliyezaa na kaka yangu akamuoa mimi nikasema sawa lakini nikamwambia kuwa siwezi kuishi naye, nilivyotoka kwa mume wangu. 

Dada yangu mkubwa akawa amefariki dunia na kuacha watoto watano wakati huo mumewe naye alikuwa ameishafariki miaka 3 nyuma.
Mama yangu akachukuwa watoto wawili na mimi nikachukua watoto watatu.Nilirudi Dar, sina mume sina kazi wala biashara yoyote, ninaishi nyumba ya kupanga.

Niliamua kukopa mtaji, nikanza kuuza sokoni  wakati huo nimepanga Chanika.
Pale sokoni akajitokeza shehe mmoja akasema anataka kunisaidia kulea watoto yatima ila anioe ili awe karibu na watoto nikakubali, nikaamini kuwa nimepata ndoa.


Tukafunga ndoa  tarehe mwezi 8, mwaka  2016 akaniambia niache kufanya biashara nikae nihudumie watoto wangu tu.

 Mwaka jana akasema tuhamia  Mkoa wa Pwani ana mashamba mengi ili tukafanye kilimo, nikakubali lakini nilipofika akanitelekeza na watoto wangu.

Sina biashara waka pakushika, huku pia ni mgeni, nimewambia wazazi wake, sijapata msada wowote, nalala njaa na watoto.


Toka mwezi mwezi 8 mwaka jana hajaja wala hajanipa matumizi, nateseka sana na watoto, kiukweli napata shida sana kaka. Hiyo ndiyo historia ya maisha yangu.
Sina pakushika, nimekata tama kabisa na haya maisha, nawachukia sana wanaume kwani wamegeuza maisha yangu kuwa magumu.


Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com
Read More
      edit

Sunday, February 11, 2018

Published 2/11/2018 01:30:00 AM by with 0 comment

KWA NINI NAWACHUKIA WANAUME-3


Ilipofika Jumapili tukaenda Buguruni, nikamuomba yule mtoto wa dada nikae kwake, akakubal ikabidi nianze kuishi hapo, nikafuata nguo zangu, nikaanza kuishi naye.
Nikawa nafuta kazi yakufanya sikupata , kutokuwa na elimu nako kulifanya ikawa ni ngumu sana  kupata kazi lakini sikukata tamaa ya maisha, nikaendelea kutafuta kazi.



Badala yakupata kazi nikapata mchumba mwingine aliyekuwa anaitwa Mudy, akanioa tukawa tunaishi Uwanja wa Ndege, nikapata mtoto wa kike tena, hapo ilikuwa ni mwaka 2008.  Maisha yakaendelea nikiwa na mume wangu,
alinipenda nikampenda, tulipofikisha miaka 4 ya ndoa, mdogo wake na mume wangu wa kiume alikuwa anafanya kazi kwenye malori, alipata ajali akapasuka kichwa na akavunjika mguu, mkono.


Ndugu wakawa bize, kila mtu yupo bize na mambo yake ikabidi mimi nimuguze yule mgonjwa, akawa anajisaidia haja zote hapo hapo kwani hawezi kutembea wala kusimama, alipopona vidonda akapelekwa Kibaha kwa mtaalamu wa kuunga mifupa ya mguu na mkono bila kutumia dawa za hospitali.

Baada ya hapo alirudi nyumbani nikaendelea kumuuguza kwa muda wa mwaka mmoja na nusu akiwa ndani, alioanza kuchechemea akatafutiwa magongo kwa ajili ya kutembelea.


Siku moja nikiwa naumwa, nikaenda kwenye hospital ya Vingunguti, cha ajabu nikaambiwa hakuna huduma kwa sababu siku hiyo ilikuwa ni Siku ya Muungano, hakuna madokta, wakati naondoka mume wangu akanipigia simu niende kazini kwake, alikuwa anafanya kazi pale Sheli Buguruni.

Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com

Read More
      edit

Saturday, February 10, 2018

Published 2/10/2018 12:00:00 PM by with 0 comment

KWA NINI MPENZI WAKO HASHINDI NYUMBANI!



Hakuna kitu kidogo ila kizuri kinachopendwa na wapenzi hasa wa kike kama mpenzi, mchumba au mume wake kushinda nyumbani siku za mapumziko, wanawake wanapenda sana wanapenda, kupita mbele ya wenza wao ili wawaone walivyobarikiwa, wanapenda sana angalau kupata muda wa kuzungumzia maendeleo ya familia yao japo kwa siku moja.


Kwa kufanya hivyo hakika nakuambia utakuwa umeongeza umechachuza sehemu ya penzi lenu kulifanya lionekane angavu tena kwa mar nyingine. Ebu jaribu, tena sio kujaribu badilika na anza kushinda nyumbani na familia yako siku ya mapumziko hata watoto wanakuhitaji kama baba yao, hata mifugo yenu kama ng’ombe nao wanafurahi wakikuona mara moja moja.

Sio kweli kwamba wanaume wote hawapendi kushinda nyumbani, lah hasa wapo wengine wanapenda kabisa ila kutokana na tabia ya mwenza wake inamfanya aamue kutokushinda nyumbani na kwenda kwa rafiki zake ama bar kula masanga ili akirudi nyumbani muda wa marumbano na vijembe uwe angalau umepungua kidogo.

Ushauri wangu angalia na rekebisha mapito yako, jiulize nini ni kero au karaha yako inayomfanya mumeo, mchumba au mpenzi wako asishinde nyumbani, au ni ile tabia yako ya kidomodomo, au ni ile gubu yako
Wakati mwingine mwenza wako anaamua kutokushinda ndani kwasababu tu anajua akishindanawe ndani siku haitaisha bila kuzinguana, bila kutukanana au kushikana singilendi na kadhalika.

Sio kweli kwamba wote wanakuwa na mambo yao wengine wanakimbia kero kerom zenu. Ingawa pia kuna wengine wanatumia fursa hiyo kama njia ya kuchepuka kwa maana ya kuondoa stesi za makelele yako.
Na wewe mwanaumea anza kurekebisha tabia zako pengine ndizo zinamfanya mwenza wako aanza kukukulalamikia nahata kukwidana naye, yawezekana wewe pia ndiyo sababu ndiyo chanzo. Kama utaweza kurekebisha suala hilo utakuwa umitendea haki familia, mkeo, mpenzi na hata nyumba yako.

Mapenzi bhana umiza kichwa. Tukutane kwenye mada nyingine.

Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. +255679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U






Read More
      edit
Published 2/10/2018 05:44:00 AM by with 0 comment

HABARI ZA MAGAZETINI LEO FEB 10, 2018


























Read More
      edit
Published 2/10/2018 01:29:00 AM by with 0 comment

KWA NINI NAWACHUKIA WANAUME-2



Baadaye nikapata mtu anatafuta mfanyakazi wa ndani, nikasafiri hadi Tegeta jijini Dar,  nikaanza kufanya kazi lakini baadaye ile kazi ilinishinda kwa sababu baba mwenye nyumba alikuwa ananitaka kimapenzi tena kwa kukasirika.

Niliacha kazi nikaenda Magomeni Mwembechai kwa kuuliza watu wenye magari hadi nikafika kwa sababu sikuwa  mwenyeji wa jiji.

Wakati natoka nyumbani kuna namba za simu nilikuwa nimeziandika kwenye karatasi. Nikanywa chai kisha nikaanza kuzitafuta zile namba nilizokuwa nimeziweka kwenye mfuko wa nguo niliokuwa nimebeba.

Niliipata ile karatasi ya namba nikaenda kwenye kibanda cha simu na kumpigia mwenye zile namba ambaye ni mtu wa nyumbani,  nikamuomba namba za simu za kaka yangu niliyezaliwa naye tumbo moja.
Siku hiyo nilipata shida sana kwani nililala stendi ilipofika asubuhi, nikatafuta sehemu ya kunywa chai, wakati nakunywa chai nikakumbuka kuna namba za kaka’ngu mtoto wa baba mkubwa.


Nikampigia kaka kumbe hakuwa mbali sana na nilipolala jana usiku pale stendi, akaja kunichukuwa hadi nyumbani kwake, kufika kwake nikakuta amepanga chumba kimoja. Ikabidi aongee na mama mwenye nyumba ambaye hakuwa na mumewe ili niwe nalala kwake.
Yule mama akaanza kunitafutia wanaume, nikamwambia mimi sitaki wanaume, akaanza kunichukia sana, ikabidi
nimulize kaka ndungu zetu wengine wanaishi wapi? Kaka akasema nisubiri Jumapili atanipeleka, akanipeleka kwa mtoto wa dada yetu Zuena ambaye alikuwa anaishi Buguruni Rozana.

Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com

Read More
      edit

Friday, February 9, 2018

Published 2/09/2018 01:26:00 AM by with 0 comment

KWA NINI NAWACHUKIA WANAUME -1



Nina umri wa miaka 32, mimi ni mzaliwa wa mkoa wa Tabora, baba yangu alifariki dunia nikiwa bado niko tumboni mwa mama yangu.


Sikubahatika kusoma japo darasa la kwanza kwani nilipofikisha miaka 10 nilienda kufanya kazi za ndani mkoani Kigoma katika kota za polisi.

Nikiwa pale nafanya kazi kwa mzee mmoja ambaye ni askari baada ya miaka mitano nikapata rafiki wa kiume ambaye alikuwa na umri wa miaka  25 wakati huo mimi nikiwa na miaka 15. Aliniambia kuwa ananipenda na yuko tayari kunioa akaniahidi mambo mengi sana.


Nikamuamini, nikakubali tukaanza urafiki ambao ulifika hadi miezi 6 ndipo akafanikiwa kuutoa usichana wangu. Nikazidisha upendo, nilimpenda sana, aliposema anataka kunioa bosi wangu akasema inabidi nirudi nyumbani ili harusi ikafanyike nyumbani kwetu.
Kweli nilirudi nyumbani kwetu Urambo ambako alikuweko mama yangu mzazi, yule mchumba akanioa baadaye nikarudi kwangu.



Baada ya muda nikapata ujautizo, mimba ilipofikisha miezi 8 mume wangu akanipeleka kwa mama yangu Urambo ili nikajifungue. Mungu akanijalia mwaka 2001 nikabarikiwa kujifungua salama mtoto wa kike.
Maisha yaliendelea kama kawaida nikiendelea kumlea mwanangu.

 Mume wangu akaanza kubadilika, akawa mkorofi sana, akaanza kutokulala nyumbani, nikimuuliza ananipiga, maisha yakaanza kuwa ya shida.
Nilimle mtoto wangu kwa shida sana, mtoto alipofikisha miaka 3 mwanaume akanirudisha nyumbani  kwa mama. Baada ya mwaka mmoja akaja kumchukua mtoto wangu ili aende akamlee mwenyewe.

Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot.com

Read More
      edit
Published 2/09/2018 12:24:00 AM by with 0 comment

JIPE MOYO UTASHINDA

Kuna wakati mateso, maumivu, shida na karaha zinaumiza na kuona kama kila kukicha ni nafuu ya jana.
Usichoke, usikate tamaa kuna mengine unayapitia ili yakufanye uwe imara zaidi-Mi&U
Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Read More
      edit

Monday, February 5, 2018

Published 2/05/2018 06:35:00 AM by with 0 comment

HABARI ZA MAGAZETI LEO FEB 5, 2018























Read More
      edit