Baadaye nikapata mtu anatafuta mfanyakazi wa ndani, nikasafiri hadi Tegeta jijini Dar, nikaanza kufanya kazi lakini baadaye ile kazi ilinishinda kwa sababu baba mwenye nyumba alikuwa ananitaka kimapenzi tena kwa kukasirika.
Niliacha kazi nikaenda Magomeni Mwembechai kwa kuuliza watu wenye magari hadi nikafika kwa sababu sikuwa mwenyeji wa jiji.
Wakati natoka nyumbani kuna namba za simu nilikuwa nimeziandika kwenye karatasi. Nikanywa chai kisha nikaanza kuzitafuta zile namba nilizokuwa nimeziweka kwenye mfuko wa nguo niliokuwa nimebeba.
Niliipata ile karatasi ya namba nikaenda kwenye kibanda cha simu na kumpigia mwenye zile namba ambaye ni mtu wa nyumbani, nikamuomba namba za simu za kaka yangu niliyezaliwa naye tumbo moja.
Siku hiyo nilipata shida sana kwani nililala stendi ilipofika asubuhi, nikatafuta sehemu ya kunywa chai, wakati nakunywa chai nikakumbuka kuna namba za kaka’ngu mtoto wa baba mkubwa.
Nikampigia kaka kumbe hakuwa mbali sana na nilipolala jana usiku pale stendi, akaja kunichukuwa hadi nyumbani kwake, kufika kwake nikakuta amepanga chumba kimoja. Ikabidi aongee na mama mwenye nyumba ambaye hakuwa na mumewe ili niwe nalala kwake.
Yule mama akaanza kunitafutia wanaume, nikamwambia mimi sitaki wanaume, akaanza kunichukia sana, ikabidi
nimulize kaka ndungu zetu wengine wanaishi wapi? Kaka akasema nisubiri Jumapili atanipeleka, akanipeleka kwa mtoto wa dada yetu Zuena ambaye alikuwa anaishi Buguruni Rozana.
Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembeleawww.miminauhusiano.blogspot. com
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.