Monday, October 3, 2016

Published 10/03/2016 09:33:00 PM by with 0 comment

MWANZO MWA UTAMU WA MAPENZI


Nimshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na kuweza kuikamilisha siku salama bila kupata tatizo lolote kubwa, ni jambo la kumshukur nawe mwanaM&U Kwa kukuepusha na balaa mbalimbali kwa siku ya leo.

Mada ya leo inazungumzia MWANZO MWA UTAMU WA MAPENZI AU MAPENZI MATAMU-MWANZO.Najua umeipenda sana hii mada ili kuweza kujua utamu ambao unazungumzwa na M&U ni upi , hapa nazungumzia kuwa mara nyingi mapenzi huwa ni matamu pindi yanapoanza.
 
Huwa matamu kwa sababu ya vitu kadhaa ambavyo vinakua miongoni mwa wahusika yaani wapenzi.
Kwa kuwa mila na tamaduni za Kiafrika mwanaume ndiye ambaye anapaswa kumtongoza mwanamke basi hapo ndipo tunapoanzia, kwani mwanaume anapokuwa anamtongoza mwanamke au binti Fulani kuna mambo kadhaa huyafanya au hufanyika;

MUDA
Kwa mwanaume anayeanza kutongoza, kutumia muda wake kwa ajili ya mwanamke anayemtongoza si tatizo kwake hata kama atakuwa amebanwa na kazi kwa namna gani yuko radhi kudanganya au kumuuguza mtu ilimradi tu akamuone mpenzi wake.

UMBALI WA ENEO
Utamu mwingine utauona pale ambalo pamoja na kuwa  na umbali wa kimakazi kati ya mwanaume na mwanamke lakini bado mwanaume anafunga safari na kwenda kumuona mpenzi wake na pengine inaweza kuwa hata kila siku iendayo kwa MUNGU. Na anfanya hivyo kwa sababu ya NGUVU NA UTAMU WA MAPENZI.

MAWASILIANO
Hata suala la kuwasiliana na mwanamke huyo huwa ni la lazima, mara kwa mara iwe kwa kumpigia simu, kumtumia ujumbe mfupi wa maneno au kuonana naye.


Kitendo hicho cha mawasiliano wapenzi wengi hasa wanawake wanapenda sana kuwa na mawasilianao ya mara kwa mara na mpenzi wake.

Kupitia mawasiliano hayo mwanaume atakuwa anamuuliza mpenzi wake mara kadhaa, “vipi babu umeishakula, unakula nini leo, ratiba yako leo ikoje mpenzi wangu, natamani tuishi wote ili uwe unanichagulia nguo za kuvaa  na kadhalika” vitu ambavyo wanawake wanapenda sana, wanapenda kujuliawa hali mara kwa mara na huo ndiyo utamu wa mapenzi kwa mwanzoni.

ZAWADI
Kwa mwanamke kwake huwa ni matamu sana wakati anatongozwa kwani mwanaume ataonesha kila aina ya kujali, kuwasiliana na hata kutoa zawadi mbalimbali kama maua, kadi, nguo za ndani, vocha, Muvi, sirizi na zinginezo ili mradi tu kuonesha kuwa anajali hata kama hana hulka hiyo.

Hata hivyo kwenye zawadi wapenzi huwa wanatofautiana kuna wengine bila zawadi wanaona kama hawapendwi ila kuna wengine kwao kawaida, umpe, usimpe ni yaleyale.

Mapenzi matamu bhana! Hiki ndicho ambacho unaweza kujibu kama utauliza ni nini kitamu zaidi katika maisha ya mwanadamu.

Mpenzi msomaji usikose muendelezo wa mada hii kila siku.

Usikose pia kusikilia kipengele cha M&U kupitia 90.8 KAHAMA FM ifikampo saa 4 usiku wa leo au unaweza kusikiliza Online kwa kudownload tunein kisha ukasachi KAHAMA FM.


      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.