Sunday, October 30, 2016

Published 10/30/2016 08:36:00 PM by with 0 comment

USHAURI WAKO:NAOMBA KUJIFUNZA KUISHI NA MWANAUME MKALI!




Habari yako kaka G, mimi ni mwanamke mwenye mtoto mmoja, nimezaa na mwanaume ambaye ni mchumba wangu.
 Kiukweli nahitaji ushauri wako sana kwani, mwanaume huyu ni mkali sana, naomba kujua ni namna gani ninaweza kuishi na mwanaume mkali. Muda wote yeye ni kuongea kwa ukali tu, kiukweli nafika sehemu naogopa hata kama kunatatizo Napata wakati mgumu kumwambia.

Nimejaribu kumwambia mara kadhaa kuhusu tabia hiyo anasema yeye ndivyo alivyo hawezi kuongea kiupole, nahisi kama nateseka sana kwa sababu mimi najua mwanamke  anahitaji kubembelezwa, kama uchumba tu iko hivi vipi nikiwa mke wake si itakuwa balaa.

Nahisi kama nitaishi maisha yasiyo na raha, nitakuwa  mwanamke ambaye nimejaa woga sina machango wowote katika familia yangu kwa kuhofia kukalipiwa.
Hivyo atakachokuwa anaamua yeye ndiyo hichohicho sasa hii ni tatizo. Nahitaji msaada wenu wadau.
JIUNGE NA M&U WHAT'SAPP KWA NA.0657486745 KUPATA MADA MBALIMBALI ZA MAPENZI.
      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.