Imetolewa na Mwanzilishi wa M&U Foundation, Gabriel Ng'osha.
Sunday, December 24, 2017
Published 12/24/2017 09:57:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Tuesday, December 19, 2017
Published 12/19/2017 04:00:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Ni siku moja imesalia ili
Wakristo na wasiyo Wakristo duniani kote kuweza kusherehekea Sikukuu ya Krismas
(kuzaliwa kwa Yesu Kristo).
Wiki kadhaa ndugu zetu
waislamu walisherehekea pia Sikukuu ya Maulidi au kuzaliwa kwa Mtume Muhammad
(S.A.W), walimaliza salama na Mungu awaongoze Wakristo nao wamalize salama
sherehe hiyo.
Msimu wa sikukuu huwa kuna
mambo mengi sana ambayo hutokea katika jamii yetu, kuna watu wanageuza sherehe
hizi kuwa za kulewa, kuzini, kugombana, kufumania, kuchinjana, kutukana na
mambo mengine mengi yenye uovu ndani yake.
Kama huu miongoni wa watu
hao achana na mambo haya, jipange kwa ajili ya mwaka mpya wa 2018. Jiulize
umelumbana mara ngapi na mpenzi wako au mumeo, umepigana na walevi au wahudumu
wa baa mara ngapi, jitathimini umetukana na majirani zako mara ngapi?
Jiulize, umekoswakoswa
kuuwawa kwa tuhuma za wizi mara ngapi? Umedundwa na kusutwa kazini na mtaani
mara ngapi? Umefumaniwa na mpenzi, mchumba, mkeo au mumeo mara ngapi na kwa
nini?
Kama ni mtu ambaye
unapenda maendeleo ya familia au mpenzi wako basi ukishapata majibu ya maswali
hayo anza kujifanyia tathimini ili kupunguza au kuachana kabisa na tabia za
kishenzi shenzi ulizonazo, ili ujipange kwa ajili ya mwaka 2018 ili uwe wa
mafanikio kwako.
Jiulize ni kwa kiasi gani
umerudi nyuma kwa sababu ya mambo yasiyokuwa na maana kwako, mara ngapi familia
yako imelala njaa kwa sababu tu ya uzembe wako wewe mzazi, iwe wa kike au wa
kiume.
Yawezekana umefeli sana
katika mitihani yako, maisha au biashara zako, pengine umefeli na sana katika
mahusiano yako, kila mwanaume au mwanamke unayempata hamfiki naye mbali aidha
kwa sababu yako au yake.
Bado haupaswi kujilaumu,
kiukubwa ni kujifunza, kukubali ukweli kuwa umeachwa au umeachika kisha anza
maisha mapya, jipange namna ya kuweza kutoboa.
Aijalishi kama mchana au
usiku wa leo hauna uhakika wa kula , jiamini unaweza kubadili maisha yako
kutoka hapo ulipo hadi kufikia huwa mtu mashuhuri, maarufu au staa.
Kama ni mfanyabiashara jiulize
ni kwa nini umeshindwa kupiga hatua, nawe msanii basi jipange kwa ajili ya
kujitangaza kitaifa na kimataifa,(M&U tutakusaidia kukupa ushauri na
chaneli zingine)kama ni mkulima hakikisha unalima kilimo chenye tija, kama ni
mwandishi basi hakikisha unaandika makala zenye kuwajenga Watanzania
wanaokusoma, kama ni mwalimu hakikisha unatimiza wajibu wako vizuri ili mwisho
wa siku upate kula matunda.
Mwaka 2018 ni mwaka wa
mabadiliko kwako, rekebisha mapito yako mabaya uliyoyapitia, usijilaumu kwa
kile kilichotokea katika maisha yako. Usijione kama umechemka au umekosea sana,
hapana ulikuwa mafunzoni, sasa umeiva anza kufanya yaliyo mema.
Ebu jaribu kutafakari ni
kwa nini watoto wako tu wamekuwa wakirudishwa nyumbani kwa sababu ya wewe
kukosa ada wakati watoto wa jirani yako wanaenda shuleni kama kawaida. Siajabu
hata mshahara na cheo unamzidi huyo jirani.
Funguka ndugu yangu, mwaka
2017 fanya kama ulikuwa wa mwaka wa mwisho kwa wewe kufanya mambo yakipuuzi,
fanya kama ulikuwa kwenye mapito na sasa umegundua zuri na baya.
Piga goti chini na mlilie
Mungu akufanye kuwa mtu mpya kwa mwaka ujao, akuepushe na migogoro ya kila siku
kwenye ndoa au penzi lako akuepushe na mabalaa ambayo umekuwa ukikuitana nayo
kazini na kwenye biashara zako.
Mwambie ALLAH umechoka kuitwa
mgumba wakati kwenye vitabu vitakatifu aliweze kumpa ujauzito mama mzee ambaye
alionekana ni tasa. Mwambie Yehova umechoka kusumbuliwa na magonjwa sugu wakati
yeye ni mti wa uzima.Mwaka 2018 jitahidi kujirekebisha na kukaa karibu na
MUUMBA WAKO. Kwa naishi hapa.
Uongozi wa M&U
FOUNDATION unapenda kukutakiwa Krismasi na Mwaka Mpya mwema.
#ACHAWOGATHUBUTU#MIMINAUHUSIANO#
Kwa
ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U
WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Na.M&U
Published 12/19/2017 03:00:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Mambo
wanaM&U, nimshukuru Mungu kwa kunipa nafasi ya kukutana nayi kwa siku
nyingine tena, karibuni katika kujifunza kuhusu uhusiano katika maisha yetu ya
kila siku.
Mada
yangu ya leo nitazungumzia watu ambao wanadhani wakitambulishwa basi inakuwa
nikifungo kwa mtu aliyemtambulisha kwa maana ya kuolewa au kuoa, wakati ukweli
unaweza usiwe hivyo.
Swala
la wapenzi kutambulishana katika familia za pande zote mbili kwa maana ya
mwanamke na mwanaume ni sehemu ya utamaduni wa jamii kubwa ya Kiafrika na ni
jambo jema sana. Ila kuna kitu kikubwa sana cha kujifunza kwa baadhi ya wanaume
na hata wanawake, nianza na wanawake.
Unaweza
ukapata mchumba ambaye akapanga mipango yote kwa kuanza kukutambulisha kwa
baadhi ya ndugu zake ambao yeye anaivana nao au anaelewana nao sana na wewe
mwanamke ukaona kama umeishamkamata kwa kila kitu, kwani baadhi ya dada aua
kaka zake wanakufahamu na kukuita wifi au shemeji na wakati mwingine hata
shangazi. Wakati huo mwanaume mwingine anaweza kufanya taratibu zote za kuja
kwenu kujitambulisha kwa utambulisho feki ili kukuaminisha lakini mwisho wa
siku akawa hana dhamila ya dhati ya kutaka kukuoa zaidi ya kula tunda.
Wanaume
Mara
nyingi baadhi ya wanaume wengi wamekuwa wakilalamikiwa kuwa ni sehemu ya
kuzalisha matatizo yanayosababishwa na uhusiano.
Kuna
watu wamewahi kuumizwa vibaya kwa kutambulishwa na wapenzi wao lakini mwisho wa
siku wakaachwa solemba kama waswahili wasemavyo.
Mrembo
mmoja aliwahi kupata bwana na akaonesha msimamo mzuri wa kumwambia jamaa kama
ana mpenda kwa dhati na ana malengo naye kwa maana ya kuwa mke na mume basi
wakatambulishane, kijana alikubali wakapanga siku na muda wa kufanya huo
utambulisho, siku ilipowadia mwanadada akatambulishwa lakini mwisho wa siku
aliyeolewa ni mtu mwingine.
Inaumiza
na ilimuuma sana binti yule kwanza ukiangalia umri wake alikuwa bado binti
mdogo lakini hicho ndicho kilichotokea.
Kila
mtu anapaswa kuwa na hofu ya Mungu anapaswa pia amuonee huruma mwenziye ni kwa
namna gani ataumia pindi atakapomdanganya kuwa anamuoa aua kuolewa naye wakati
moyoni mwaka anajua kabisa kuwa hana mpango wa kumuoa.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
Published 12/19/2017 12:00:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Poleni na majukumu ya siku nzima. Nimekuwa
nikifuatukia ushauri na maoni yenu mbalimbali kuhusu UHUSIANO WA MAPENZI.
Mimi ni binti wa miaka 20 nina mwaka mmoja nikiwa
nimeolewa mke mdogo na mwanaume mwenye miaka zaidi ya 40.
Nilipoolewa nimemkuta mke mwenzangu mkubwa yeye ana
miaka 40. Lakini nimejaribu kumpenda mke mwenzangu (Bi mkubwa), lakini yeye
haoneshi kunipenda zaidi ya chuki dhidi yangu. Naomba ushauri nifanyeje ili
anipende au niishi naye kivipi?
#ACHAWOGATHUBUTU#MIMINAUHUSIANO#
Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali
jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au
tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Saturday, December 16, 2017
Published 12/16/2017 03:30:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Nimshukuru Mungu kwa wema
wake alionitendea leo katika mzunguko mzima wa shughuli zangu za kila siku,
ikiwemo kuninuthuru na mambo mbalimbali ya kiovu. Bila shaka na wewe unaposoma makala
haya huna budi kusema asante Mwenyezi Mungu kwa kunisimamia katika kuimaliza
vyema siku ya leo.
Katika somo la leo
tutajifunza kuhusu tabia za baadhi ya
wapenzi kutokuwa na tabia ya kukubali pindi wanapokosea na badala yake
wanang’ang’ana na kusababisha mtafaruku mkubwa katika uhusiano wake.
Baba au mama bora ni yule
ambaye anajifunza kutokana na makosa pindi anapokosea, hata mpenzi, mchumba
anayefaa au unayefaa ni yule mwenye tabia ya kukubali unapokuwa umekosea.
Kitu kinachosikitisha ni
baadhi ya wapenzi kukataa katakata kuwa hawajakosea hata kama wamekosea, kiasi
kwamba mtu yeyote akija na kusimuliwa namna ilivyokuwa anabaini kuwa wewe ni mkosaji
lakini hutakikukubali ukweli, hivu kwa
nini hutaki?
Unajihisi wewe ni malaika
ambaye huwezi kukosea, au unahisi wewe ni mkamilifu sana kuliko penzi, mchumba
au mwenza wako. Jifunze kutokana na makosa. Lakini unapokosea na kukataa kwa
kusudi unamfanya hata mwenza wako kujiona yeye ndiyo mkosaji na mnyonge kila
siku. Wakati mwingine unaweza kummwathiri kisaikolojia, kwani muda mwingi
atakuwa anakaa na kuona unamuone mara nyingi hata kosa linapokuwa lako
unalazimisha liwe lake.
Katika maisha ya kila siku
kuna mambo mengi ambayo unakutanana nayo, kuna vishawishi mbalimbali ambavyo
vinakusakama kila upitapo kwa lengo la kumaliza, kuvunja uhusiano au
kukugombanisha na mpenzi wako.
Kaa ukijua hakuna mtu
ambaye anaweza kufurahia wewe na mpenzi, mchumba, mume au mke wako mnavyoishi
kwa furaha wakati yeye kila siku ni ngumi na minyukano ya hali ya juu, ni
dhahili mtu mwingine atafanya juu chini kuhakikisha anakugombanisha au kukuona
na wewe ukipata karaha kama ambavyo anazipata yeye.
Hiyo ndiyo hila kubwa ya
shetani kwa mwanadamu, anaweza kumtumia jirani, ndugu, rafiki, mfanyakazi, mwanachuo mwenzako
ilimradi tu kuuharibu wako.
Basi unapoteleza, kaa
chini na jitathimini kwa kujikagua toka mwanzo wa siku kwa maana ya asubuhi,
mapito yako nahata kurudi kwako nyumbani, kwa kufanya hivyo utaweza kubaini ni
wapi umemkwaza kipenzi chako. Na kama ukigundua sehemu ulipomkwaza basi
kubaliana na kosa kwa kumuomba radhi na kisha jiepushe, jichunge kurudia kosa
lile lile kwani kufanya hivyo ni kama dharau, ni kama unalitumia vibaya neno
msamaha.
Kwa leo naomba kuishia
hapa nawashukuru wale wote ambao wanaendelea kuchangia gharama za uendeshaji wa
M&U na nitaoa mrejesho wa mchango wa Taasisi ya M&U kuhusu mkakati wa
kuanzisha chuo cha ushonaji.
Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. +255679979785
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa
Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
Published 12/16/2017 12:00:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Habari za kazi ndugu, swali langu ni sahihi kwa wapenzi au wana ndoa kuwa wanakaguaka kila wanapotoka kazini?
Kwa mfano mwanamke akama hajaenda kazini basi mumewe
akirudi anamkaguwa na mwanaume naye akiwa hajaenda kazini, mkewe akirudi kabla
ya kuoga aua kupumzika anamkagua kama kachepuka!
Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. +255679979785
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa
Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
Friday, December 15, 2017
Published 12/15/2017 03:00:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Hakuna aliyeijua leo, lakini ni Mungu pekee ambaye ametupa
kibali cha kutumia pumzi yake na ndiyo maana tuko wote.
Waswahili wanasema kazi mbaya ukiwa nayo na wengine
wanasema kazi nzuri ukiwa hauko nayo
kama wewe ni mmoja wa wale ambao ulishwawahi
kujilaumu kwa kum,uacha au kufanyia
vimbwanga mpenzi wako na baada ya kuacvhana naye kwa muda ukaanza kujiulia na
kujilaumu ningejuaaa,….. basi nitumie maoni yako na yatatoka wiki ijayo kwenye safu
hii.
Unajuata kuwa naye kwa sababu unaye.
Wengi wamekuwa akijilamumu sana kwa kuwa na wapenzi
flani kwa sababu ya changamoto za hapa na pale, si wanaume wala wanawake ambao
wamejikuta wakiingia kwenye manung’uniko hayo.
Alki wengi wanasahau wanajuata kwa sababu tu yuko
naye, kuna wenzako wanatamni hata
wampate huyo wa kumjutisha anamkosa, kuna mwingine anatamni ampate mpenzi
yeyote atakaye kuwa ana msumbua mara kumuuliza hiki na kile, hauna sababu ya
kujuta hayo ndiyo maisha hata kwa huyo
unayedhani ni bora naye ukipa nafasi ni yale yale tu.
Falsaha hii naifananisha na mtu ambaye anafanya kazi
matra nyingi kazi mbaya ni ile ambayo unakuwa nayo ila ukiwa hauna kazi unaona
kazi yoyote ni nzuri sana.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
Published 12/15/2017 12:00:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Mimi ni mwanamke ambaye nimebahatika kuolewa. Hivi
karibuni nimegundua kuwa mume wangu amezini na binamu yangu. Je, nani wa
kumlaumu kati ya mume wangu na ndugu yangu?
Nini nifanye kwa kitendo alinichonifanyia mume wangu
na binamu yangu?
#ACHAWOGATHUBUTU#MIMINAUHUSIANO#
Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali
jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au
tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Published 12/15/2017 12:00:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Usiogope kukutana au kupatwa na shida, hautakufa kwa sababu ya shida, hautadhorika kwa sababu ya shida ulizonazo ila kama ukizitumia vizuri shida zako zitakufanya upate uvumbuzi wa matatizi na changamoto zako.
Maisha yoyote yale, duniani kote kazima ukutane na shida mbalimbali na hata waliofanikiwa wote walikutana na shida ambazo mwisho wa siku zikawafanya wapate njia yakutokea.
Nitakupa mfano mmoja:
Mama watatu walikuwa wanaenda hospitalini kumpelekea chakula lakini walipofika mwisho wa gari wakawa hawana nauli ya kuendelea kuweza kufika hospitalini.
Mwanamke mmoja kati ya wale aliuliza tunafikaje wakati hatuna nauli, mwanamke mwingine akasema palipo na nia pana njia. Waliamua kutafuta njia ya mkato lakini walipokata kona ya kwanza yule mwanamke aliyeuliza swali la kwanza akauliza tena. Je, tunaielewa kweli njia ya mkato ya kutufikisha hospitalini? Mwanamke mwingine alimjibu kuwa #MATATIZO HUZALISHA UVUMBUZI# Hivyo tutafika kwa njia yoyote ile. Kweli walipambana na kufanikiwa kumuona mgonjwa wao ingawa kuna sehemu walijikwaa, walipotea na kuzunguka lakini waliweza kufanikiwa.
Jifunze kwa wanawake hawa watatu, jifunze kwa changamoto mbalimbali za maisha ambazo unakutana nazo bila kujali ni za #MASOMO#KIKAZI#KIMAPENZI#FAMILIA#BIASHARA.
#ACHAWOGATHUBUTU#MIMINAUHUSIANO#
Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge
na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au
tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Thursday, December 14, 2017
Published 12/14/2017 09:30:00 PM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Mungu ni mwema na mwenye upendo wa dhati kwetu sote kwa yeye kutuunganisha na kuwa kitu kimoja kupitia #Mi&U. Nikushukuru wewe ambaye umekuwa sehemu ya #Mi&U tangu kuanzisha hadi sasa. Najua kuna mengi ambayo unayapitia katika maisha yako ya kila siku yawe ya mapenzi au kawaida.
Vivyo hivyo hata Mi&U inapitia mambo na changamoto mbalimbali katika kujiimarisha zaidi. Kuna wakati unatokea huduma zetu ambazo zilikufanya ukajiunga nasi zinalegalega kwa sababu maalumu lakini hatuwezi kuanguka hata kama tutayumba kwa myumbo mkubwa na mkali. Hata wewe pia kwenye maisha yako ya kazini, shuleni, ibadani, biasharani na hata mapenzi umekuwa na changamoto, maumivu, mateso na majonzi ya kila aina.
Nimepata nafasi hii kwa kudra za Mwenyezi Mungu sina budi kukusihi kuendelea kupambana pamoja na kila aina ya myumbo ambao umekuwa ukikutana nao. Mapenzi ndiyo hasa yanayoongoza kwa kukuyumbisha kwa kipindi fulani, lakini kama mwanaMi&U ambaye umekuwa ukishiriki nasi katika mada, maoni na ushauri mbalimbali, usikubali kuyumba kwa sababu ya mapenzi. Jipe imani kuwa Mungu yuko upande wako wakati ukijipigania na yeye pia anakupigania.
Usikate tamaa wewe ambaye umeachwa na mpenzi, mchumba au mwenza wako kwa namna yoyote ile, iwe kakutelekeza na familia au lah, iwe kakuacha na ujauziti anahudumia au ahudumii, usikubali kukata tamaa kamwe. Naliona sononeko lako wewe mwanamke ambaye umefikwa na mumeo au mkeo, umelia, sasa imetosha acha maisha yaendelee kwani mapito hayo yaliwekwa katika maisha yako ili uyashinde na uingine katika nchi ya ahadi yenye mito ya maziwa na asali lakini kama utashindwa basi watu watakucheka, watakudharau, hata yule ambaye amekuacha utakuwa umempa kichwa na kujiona kuwa bila yeye huwezi kuishi lakini ukweli ni kwamba unaweza kuishi.
Nakushuruku wewe mwanamke ambaye umetelekezwa na mumeo lakini umekubaliana na ukweli na unapambana na hali yako kuhakikisha unawasomesha watoto wako kwa uchungu na matesio makali lakini nakwambia Mungu hawezi kukunyima kila kitu.
Kuna mateso na changamoto ambazo unaweza ukawa unapewa ili kupimwa ni kwa namna gani akili uliyopewa inaweza kufanya kazi katika maisha yako. Unapimwa kungaliwa ni kwa namna gani unaweza kuwa mvumilivu na mwenye kukabiliana changamoto mbalimbali. #USIKUBALI #KUSHINDWA #KUKATAA #TAMAA #KUJIONA #DHAIFU AU #HUWEZI
Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785. Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa Na.M&U
Published 12/14/2017 10:00:00 AM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Mwaka ndugu ndiyo unakaribia kuisha, yamkini ulikuwa na
majukumu au mipango mingi sana katika maisha ya penzi lako. Je, mipango yako
imeenda kama ulivyokuwa umepanga? Kama ilienda aua haijaenda sawa mshukuru
Mungu. Kwani bado kakujaliwa pumzi yake.
Kama mipango haikwenda sawa, jiulize kwa nini? Nani
chanzo au sababu ya mipango yako kufeli? Je, ni wewe, ndugu, mpenzi, mfanyakazi
au mwanafunzi mwenzako, au ni akili yako?
Kama ni wewe, kwa nini na kama ni yule kwa nini? Vipi
kuhusu mpango wako wa kuoa au kuolewa, umefikia wapi? Nini na nani chanzo cha
migogoro katika penzi lako?
Kwa mwaka 2017 changamoto zipi kubwa na mbaya ambazo
umepizipitia? Je, ni jambo lipi lililokukwaza na kukusumbua katika mapenzi kwa
mwaka huu?
Katika ugomvi na mwenza wako nani amekuwa chanzo, ni
wewe au yeye? Ni kwa kiasi gani umepambana kuepukana na changamoto hizo?
Jifunze changamoto na mambo yote mazuri ambayo
umeyapitia kwa mwaka 2017 kisha jirekebishe kwa mwaka 2018. Usikate tamaa kwa
sababu ulifeli sana kwenye biashara, masomo, kazini au penzi lako bali mshukuru
Mungu kwa kukuonesha upande wa pili wa maisha ya kazi, shule au mapenzi. Kwa mwenye
swali au maoni, karibu DM AU #WhatsAPP +255679979785.
Jipange kuuanza mwaka kwa mapambano mapya kabisa,
jiepushe na kisirani, maamuzi yasiyokuwa na busara. Kuhamaki na kuchukua hatua.
Kama taasisi tunashukuru uwepo wako toka kuanzishwa
kwake, changamoto na hapa tulipo.
Taasisi ya Mimi na Uhusiano "Mi&U"
inakutakiwa KHERI YA MWAKA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA 2018.
#ACHAWOGATHUBUTU#MIMINAUHUSIANO#
Kwa ushauri wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge
na M&U WhatsApp:+255679979785 au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au
tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Published 12/14/2017 12:00:00 AM by Mimi na Uhusiano 'M&U' with 0 comment
Naomba
ushauri wako, mimi ni mwanamke ambaye nimeolewa hivi karibuni, ila kabla ya
ndoa sikuwa nimekutana kimwili na mume wangu.
Baada ya
kufuata taratibu zote za kwetu alinioa.Siku ya kwanza nakutana naye faragha
nilishtuka sana kuona ana #KIBAMIA nikapotezea kwa kujua atakuwa anajua kukitumia
vizuri.
Kiukweli
siku zimekuwa nyingi naona kama siinjoyi chochote kwa kibamia chake. Naipenda
sana ndoa yangu. Je. Nifanyeje au nitumie staili ili niinjoyi
#KIBAMIACHAMUMEWANGU.
#ACHAWOGATHUBUTU#MIMINAUHUSIANO#
Kwa ushauri
wa Uhusiano wa Mahaba na Ujasiriamali jiunge na M&U WhatsApp:+255679979785
au tuffolow Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Subscribe to:
Posts (Atom)