Nimshukuru Mungu kwa wema
wake alionitendea leo katika mzunguko mzima wa shughuli zangu za kila siku,
ikiwemo kuninuthuru na mambo mbalimbali ya kiovu. Bila shaka na wewe unaposoma makala
haya huna budi kusema asante Mwenyezi Mungu kwa kunisimamia katika kuimaliza
vyema siku ya leo.
Katika somo la leo
tutajifunza kuhusu tabia za baadhi ya
wapenzi kutokuwa na tabia ya kukubali pindi wanapokosea na badala yake
wanang’ang’ana na kusababisha mtafaruku mkubwa katika uhusiano wake.
Baba au mama bora ni yule
ambaye anajifunza kutokana na makosa pindi anapokosea, hata mpenzi, mchumba
anayefaa au unayefaa ni yule mwenye tabia ya kukubali unapokuwa umekosea.
Kitu kinachosikitisha ni
baadhi ya wapenzi kukataa katakata kuwa hawajakosea hata kama wamekosea, kiasi
kwamba mtu yeyote akija na kusimuliwa namna ilivyokuwa anabaini kuwa wewe ni mkosaji
lakini hutakikukubali ukweli, hivu kwa
nini hutaki?
Unajihisi wewe ni malaika
ambaye huwezi kukosea, au unahisi wewe ni mkamilifu sana kuliko penzi, mchumba
au mwenza wako. Jifunze kutokana na makosa. Lakini unapokosea na kukataa kwa
kusudi unamfanya hata mwenza wako kujiona yeye ndiyo mkosaji na mnyonge kila
siku. Wakati mwingine unaweza kummwathiri kisaikolojia, kwani muda mwingi
atakuwa anakaa na kuona unamuone mara nyingi hata kosa linapokuwa lako
unalazimisha liwe lake.
Katika maisha ya kila siku
kuna mambo mengi ambayo unakutanana nayo, kuna vishawishi mbalimbali ambavyo
vinakusakama kila upitapo kwa lengo la kumaliza, kuvunja uhusiano au
kukugombanisha na mpenzi wako.
Kaa ukijua hakuna mtu
ambaye anaweza kufurahia wewe na mpenzi, mchumba, mume au mke wako mnavyoishi
kwa furaha wakati yeye kila siku ni ngumi na minyukano ya hali ya juu, ni
dhahili mtu mwingine atafanya juu chini kuhakikisha anakugombanisha au kukuona
na wewe ukipata karaha kama ambavyo anazipata yeye.
Hiyo ndiyo hila kubwa ya
shetani kwa mwanadamu, anaweza kumtumia jirani, ndugu, rafiki, mfanyakazi, mwanachuo mwenzako
ilimradi tu kuuharibu wako.
Basi unapoteleza, kaa
chini na jitathimini kwa kujikagua toka mwanzo wa siku kwa maana ya asubuhi,
mapito yako nahata kurudi kwako nyumbani, kwa kufanya hivyo utaweza kubaini ni
wapi umemkwaza kipenzi chako. Na kama ukigundua sehemu ulipomkwaza basi
kubaliana na kosa kwa kumuomba radhi na kisha jiepushe, jichunge kurudia kosa
lile lile kwani kufanya hivyo ni kama dharau, ni kama unalitumia vibaya neno
msamaha.
Kwa leo naomba kuishia
hapa nawashukuru wale wote ambao wanaendelea kuchangia gharama za uendeshaji wa
M&U na nitaoa mrejesho wa mchango wa Taasisi ya M&U kuhusu mkakati wa
kuanzisha chuo cha ushonaji.
Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. +255679979785
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa
Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.