Niliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Koyi, nilidumu na Koyi kwa muda wa mwaka mmoja na nusu ila baadaye niliachana naye kutokana nay eye kuhamia mkoani.
Nilipata mpenzi mwingine ambaye ninampenda na yeye ananipenda sana ingawa jamaa huwa ana wivu sana. Juzi kati nilichukua picha ya Koyi na kuiweka kwenye Status yangu ya WhatsApp kasha nikaandika my friend. Baada ya kumuda kidogo nikapokea ujumbe kutoka kwa mpenzi wangu mpya ambaye akaniuliza kuwa kwa nini nimeweka ile picha ya Koyi ambaye anajua kuwa aliwahi kuwa mpenzi wangu.
Nilikataa kuwa Koyi hakuwahi kuwa mpenzi wangu lakini nilisahau kuwa kumbe niliwahi kumwambia mpenzi wangu mpya kuhusu Koyi.
Nilibishana kwa muda mrefu sana na mpenzi wangu ambaye alikuwa akinilalamikia kuwa mimi ni Malaya, na ninampotezea muda kwa sababu yeye ananipenda na ana malengo na mimi ila mimi niko na wanaume wengine ambao ninawapenda na kuwajali ndiyo maana nikathubutu hata kumuweka kwenye status.
Kwa kifupi penzi langu limeharibika sana kwa sababu ya picha ya x-wangu, ninaomba ushauri kwani jamaa mpya nampenda sana.
Nimejaribu kumuomba msamaha lakini hanielewi, sijui nini nifanye kwani nimeharibu siku yangu bila kupenda.
Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot. com
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.