Monday, April 3, 2017

Published 4/03/2017 06:46:00 AM by

MAGAZETI LEO, APRIL 3, 2017


























Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
Read More
      edit

Sunday, April 2, 2017

Published 4/02/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-41



 
Aliporudi usiku akaahidi kesho atanipeleka hospitalini, usiku nikampa mambo kama kawaida, basi aliendelea na tabia hiyo kwa siku kadhaa baada ya kuridhika kuwa amenifaidi basi akaamua kunitelekeza pale gesti.

ENDELEA…

Nakumbuka siku ya kunitelekeza aliamka alfajiri akaomba naniliiii, nikampa kama mara mbili hivi, baada ya hapo akajiandaa na kuondoka zake huku akiniaga kama kawaida alivyokuwa ananiaga siku zingine.

Aliniachia kama shilingi elfu ishirini na moja akadai kuwa ni za matumizi, nikamshukuru ila nilimkumbushia suala la kumpelekea mtoto hospitalini akasema akirudi tutaenda, kwani hana pesa kwa wakati huo.
 
Kabla hajaondoka nilimuuliza kama ameishalipia malipo ya chumba cha gesti ambacho ninakaa, akasema kisha lipia siku tatu zote. Nilimuelewa na siku na shaka naye zaidi ya kuwa mpole pasipo kujua dhamila yake. Basi aliondoka na kuniacha nikiwa na mtoto wangu.
Mchana mzima ukapita bila kupokea ujumbe wake mfupi wa maneno wala simu yake, kila nilipompigia niliambiwa simu yake iko bize, inatumika.

Nilijaribu kumpigia na kumtumia SMS kwa siku nzima lakini sikupata majibu, hatimaye jioni ikaingia, mwisho usiku, bila jamaa kutokea, nikachukulia poa tu, kukacha, wapi, mchana mwingine, jioni tena na mwisho ukawa ni usiku mwingine bila jamaa kuonekana.

Nilianza kuhisi jambo kichwani mwangu, nikatafakari ni siku tatu sasa nimekaa pale, na chumba kila siku ni shilingi elfu saba. Nikiwa bado najiuliza mara ghafla nilisikia mlango ukigongwa, nikaamka na kujifunga vizuri kisha nikaulekea mlango ili kujua ni nani aliyekuwa anagonga na nini alichokuwa anakihitaji?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.  0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U



Read More
      edit
Published 4/02/2017 10:00:00 AM by

NAMNA YA KUONDOA HOFU-3





Karibu katika muendelezo wa mada yetu ya namna ya kuondoa hofu katika moyo wako , mwili na hata maisha yako. Kwani hofu ya moyo ndiyo husababisha hofu ya mwili na hofu hiyo ndiyo hasa uzalisha hofu kuu kwa muusika.
 Hofu ambayo inaonekana kwenye uhalisia wa maisha. Nilizungumzia baadhi ya hofu na leo naendelea tena na  mada yetu.


HOFU YA KIJINGA

Kuhisi kuwa ukifanya jambo fulani utachekwa, utashangaliwa, utaonekana wa ajabu, utaonekana hufai kama jambo lenyewe ulilofanya litashindwa kufanikiwa. 


Ni kwambie kitu ili uwe mtu kama maybe wewe unamfikiria, mfano Bakhresa, Bill Gates, Ben Po, Shilole, Snura, Diamond, Mo, Dk. Mengi, Madam  Ritha, Shigongo na wengine wengi unaowafahamu mwenyewe, ni lazima ujitoe ufahamu, kwa ajili ya jambo ambalo unataka kulifanya.


Hivi ni mambo mangapi ambayo umeyasikia yakisemwa yakiandikwa kuhudu Diamond lakini leo si wote tunamkubali kuwa anaiwakili Tanzania kimataifa kwenye mambo ya muziki.


Anatuwakilisha kwa sababu alisemwa, aliandikwa sana akasengenywa, akadhihakiwa, akaziba masikio yake na kuamua kufanya kile alichokifanya na ndiyo maana leo hii kaibuka kuwa mshindi.


Lakini kama angekuwa na hofu kwa sababu ya maneno ya baba, mama, rafiki  mpenzi, jirani, mwalimu, mchungaji au shehe wake basi asingefika hapo alipo. Wala asingeitwa kupafomu  katika ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 (AFCON 2017), Januari 14 nchini Gabon.


Ondoa kwanza, hofu ya kumuogopa fulani, kuogopa kuwa utaoneka mshamba au bado uko nyuma sana, acha waseme wewe komaa, mwisho wa siku hao hao watakuja kukupongeza hata kama siyo uso kwa uso lakini mioyoni mwao watakuwa wankukubali kiaina.


Ni lazima uchukue maamuzi magumu au ya ajabu  ili uonekane mtu wa ajabu. Usihofie kuchekwa, acha wacheke ilimradi wewe umejaribu, umethubutu. Na kwa kuchekwa iko iko siku utashinda.


NAKUPA MFANO WANGU HAI

Mwaka 2009 nilitamani sana kuanzisha Ng’os ya kutoa elimu ya Afya  ya Mama na Mtoto, kuna watu walinicheka na kuniambia sitaweza, nikajiuliza moyoni mwangu hivi ni kweli mimi msiwezi, na kwa nini siwezi ni kwa sababu damu yangu nay a wale wanaoweza zinatofauti ni kwa sababu wenzangu, hawali, hawaendi haja, hawaugui, wakifa hawataoza. 


Nilipojiuliza maswali hayo nikapata jibu kuwa mimi na wao tuko sawa, unajua nilifanya nini basi usikose kesho kwenye soma hili la namna ya kuondoa Hofu. 

Kama una swali, maoni au ushauri unaweza kuuliza moja kwa moja au nitumie inbox kwangu.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

Asante sana na MUNGU akubariki wewe maybe umezalia tarehe na mwezi kama niliozaliwa mimi.
Nawapenda sana .
Read More
      edit

Saturday, April 1, 2017

Published 4/01/2017 03:30:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-40








NILIPOISHIA...

Nilikaa gesti kwa wiki nzima lakini kila nilipompigia jamaa hakuwa anapokea simu yangu na hata SMS zangu hakuwa anajibu.

ENDELEA...


Niliumia sana na kujiona ni mtu kwenye mikosa mingi katika maisha yangu.

Kutokana na yule jamaa kuniacha pale gesti nilijikuta nikiangukia mikononi mwa msamalia mwema mwingine ambaye alinihakikishia kuwa yuko tayari kunisaidia tatizo la mtoto wangu. Kwa kuwa alikuwa anaishi Jijini Dar aliniombe tuondoke wote, tulianza safari hadi Jijini Dar es Salaam.


Alinipangishia chumba kwenye gesti moja iliyopo Magomeni, Dar na kuniahidi kuwa kesho yake tutaamkia hospitali ya CCBRT kwa ajili ya kumpeleka Gift iki akafanyiwe uchunguzi kuhusu mguu wake.

 
Ilipofika usiku nilishangaa mwanaume yule alirudi kwenye chumba changu na kuombe tufanye mapenzi, nilimwambia kuwa aliahidi kunisaidia na siyo penzi inakuaje. Aliongea sana na kwa kuwa nilikuwa na shida ya kumuona mtoto wangu akipona mguu wake. 


Nilijikuta namkubalia na kumvulia pichu, tukafanya yetu. Kulipokucha akaondoka cha ajabu hakurudi hadi usiku na muda mwingi simu yake haikuwa ikipatikana.

Aliporudi usiku akaahidi kesho atanipeleka hospitalini, usiku nikampa mambo kama kawaida, basi aliendelea na tabia hiyo kwa siku kadhaa baada ya kuridhika kuwa amenifaidi basi akaamua kunitelekeza pale gesti.

Usikose kujua nini kilifuatia baada ya kutelekezwa gesti kwa mara ya pili.



Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U


@@@
Read More
      edit