Aliporudi usiku akaahidi kesho atanipeleka
hospitalini, usiku nikampa mambo kama kawaida, basi aliendelea na tabia hiyo
kwa siku kadhaa baada ya kuridhika kuwa amenifaidi basi akaamua kunitelekeza
pale gesti.
ENDELEA…
Nakumbuka siku ya kunitelekeza aliamka alfajiri
akaomba naniliiii, nikampa kama mara mbili hivi, baada ya hapo akajiandaa na
kuondoka zake huku akiniaga kama kawaida alivyokuwa ananiaga siku zingine.
Aliniachia kama shilingi elfu ishirini na moja akadai
kuwa ni za matumizi, nikamshukuru ila nilimkumbushia suala la kumpelekea mtoto
hospitalini akasema akirudi tutaenda, kwani hana pesa kwa wakati huo.
Kabla hajaondoka nilimuuliza kama ameishalipia malipo
ya chumba cha gesti ambacho ninakaa, akasema kisha lipia siku tatu zote.
Nilimuelewa na siku na shaka naye zaidi ya kuwa mpole pasipo kujua dhamila
yake. Basi aliondoka na kuniacha nikiwa na mtoto wangu.
Mchana mzima ukapita bila kupokea ujumbe wake mfupi wa
maneno wala simu yake, kila nilipompigia niliambiwa simu yake iko bize,
inatumika.
Nilijaribu kumpigia na kumtumia SMS kwa siku nzima
lakini sikupata majibu, hatimaye jioni ikaingia, mwisho usiku, bila jamaa
kutokea, nikachukulia poa tu, kukacha, wapi, mchana mwingine, jioni tena na
mwisho ukawa ni usiku mwingine bila jamaa kuonekana.
Nilianza kuhisi jambo kichwani mwangu, nikatafakari ni
siku tatu sasa nimekaa pale, na chumba kila siku ni shilingi elfu saba. Nikiwa
bado najiuliza mara ghafla nilisikia mlango ukigongwa, nikaamka na kujifunga
vizuri kisha nikaulekea mlango ili kujua ni nani aliyekuwa anagonga na nini
alichokuwa anakihitaji?
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U