Karibu katika muendelezo
wa mada yetu ya namna ya kuondoa hofu katika moyo wako , mwili na hata maisha
yako. Kwani hofu ya moyo ndiyo husababisha hofu ya mwili na hofu hiyo ndiyo
hasa uzalisha hofu kuu kwa muusika.
Hofu ambayo inaonekana kwenye uhalisia wa
maisha. Nilizungumzia baadhi ya hofu na leo naendelea tena na mada yetu.
HOFU YA KIJINGA
Kuhisi kuwa ukifanya jambo
fulani utachekwa, utashangaliwa, utaonekana wa ajabu, utaonekana hufai kama
jambo lenyewe ulilofanya litashindwa kufanikiwa.
Ni kwambie kitu ili uwe
mtu kama maybe wewe unamfikiria, mfano Bakhresa, Bill Gates, Ben Po, Shilole,
Snura, Diamond, Mo, Dk. Mengi, Madam
Ritha, Shigongo na wengine wengi unaowafahamu mwenyewe, ni lazima ujitoe
ufahamu, kwa ajili ya jambo ambalo unataka kulifanya.
Hivi ni mambo mangapi
ambayo umeyasikia yakisemwa yakiandikwa kuhudu Diamond lakini leo si wote
tunamkubali kuwa anaiwakili Tanzania kimataifa kwenye mambo ya muziki.
Anatuwakilisha kwa sababu
alisemwa, aliandikwa sana akasengenywa, akadhihakiwa, akaziba masikio yake na
kuamua kufanya kile alichokifanya na ndiyo maana leo hii kaibuka kuwa mshindi.
Lakini kama angekuwa na
hofu kwa sababu ya maneno ya baba, mama, rafiki
mpenzi, jirani, mwalimu, mchungaji au shehe wake basi asingefika hapo
alipo. Wala asingeitwa kupafomu katika ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika
2017 (AFCON 2017), Januari 14 nchini Gabon.
Ondoa kwanza, hofu ya
kumuogopa fulani, kuogopa kuwa utaoneka mshamba au bado uko nyuma sana, acha
waseme wewe komaa, mwisho wa siku hao hao watakuja kukupongeza hata kama siyo
uso kwa uso lakini mioyoni mwao watakuwa wankukubali kiaina.
Ni lazima uchukue maamuzi
magumu au ya ajabu ili uonekane mtu wa
ajabu. Usihofie kuchekwa, acha wacheke ilimradi wewe umejaribu, umethubutu. Na kwa
kuchekwa iko iko siku utashinda.
NAKUPA MFANO WANGU HAI
Mwaka 2009 nilitamani sana
kuanzisha Ng’os ya kutoa elimu ya Afya
ya Mama na Mtoto, kuna watu walinicheka na kuniambia sitaweza,
nikajiuliza moyoni mwangu hivi ni kweli mimi msiwezi, na kwa nini siwezi ni kwa
sababu damu yangu nay a wale wanaoweza zinatofauti ni kwa sababu wenzangu,
hawali, hawaendi haja, hawaugui, wakifa hawataoza.
Nilipojiuliza maswali hayo
nikapata jibu kuwa mimi na wao tuko sawa, unajua nilifanya nini basi usikose
kesho kwenye soma hili la namna ya kuondoa Hofu.
Kama una swali, maoni au
ushauri unaweza kuuliza moja kwa moja au nitumie inbox kwangu.
Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745 au 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
Asante sana na MUNGU
akubariki wewe maybe umezalia tarehe na mwezi kama niliozaliwa mimi.
Nawapenda sana .