NILIPOISHIA...
Nilikaa gesti kwa wiki nzima lakini kila nilipompigia
jamaa hakuwa anapokea simu yangu na hata SMS zangu hakuwa anajibu.
ENDELEA...
Niliumia sana na kujiona ni mtu kwenye mikosa mingi
katika maisha yangu.
Kutokana na yule jamaa kuniacha pale gesti nilijikuta
nikiangukia mikononi mwa msamalia mwema mwingine ambaye alinihakikishia kuwa
yuko tayari kunisaidia tatizo la mtoto wangu. Kwa kuwa alikuwa anaishi Jijini
Dar aliniombe tuondoke wote, tulianza safari hadi Jijini Dar es Salaam.
Alinipangishia chumba kwenye gesti moja iliyopo
Magomeni, Dar na kuniahidi kuwa kesho yake tutaamkia hospitali ya CCBRT kwa
ajili ya kumpeleka Gift iki akafanyiwe uchunguzi kuhusu mguu wake.
Ilipofika usiku nilishangaa mwanaume yule alirudi
kwenye chumba changu na kuombe tufanye mapenzi, nilimwambia kuwa aliahidi
kunisaidia na siyo penzi inakuaje. Aliongea sana na kwa kuwa nilikuwa na shida
ya kumuona mtoto wangu akipona mguu wake.
Nilijikuta namkubalia na kumvulia pichu, tukafanya
yetu. Kulipokucha akaondoka cha ajabu hakurudi hadi usiku na muda mwingi simu
yake haikuwa ikipatikana.
Aliporudi usiku akaahidi kesho atanipeleka
hospitalini, usiku nikampa mambo kama kawaida, basi aliendelea na tabia hiyo
kwa siku kadhaa baada ya kuridhika kuwa amenifaidi basi akaamua kunitelekeza
pale gesti.
Usikose kujua nini kilifuatia baada ya kutelekezwa
gesti kwa mara ya pili.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
@@@