Thursday, December 31, 2015

Published 12/31/2015 07:09:00 PM by with 0 comment

NIMETOA MIMBA ZAKE 2!





Najua nimefanya kitendo kibaya sana, lakini haikuwa akili yangu ni akili ya mapenzi, mimi ni msichana wa miaka 21 nina mpenzi wangu ninayempenda na yeye ananipenda sana na anahitaji kunioa. TatIzo lake ni kwamba kila nikipata mimba ananishauri nitoe mpaka sasa nishatoa mimba zake 2.
Je, kwa kitendo hicho atakuwa na mapenzi ya dhati kweli na mimi au ananitumia ....?? Naomba ushauri wenu.
 Na:Timotheo Mjuni-M&U

Read More
      edit
Published 12/31/2015 07:01:00 PM by with 0 comment

KWA TABIA HII WANAWAKE NI WAVUMILIVU AISEE!


Mimi ni binti nimeolewa yapata miezi 10 sasa niko kwenye ndoa, kuna kipindi naiona ndoa chungu na ninatamani hata kuachikakwanisina furaha ninapokuwa faragha na mume wangu kutokana na harufu kali ya pombe, sigara na hata jasho la mume wangu. 
Kuna wakati anamaliza hata siku 2 hajaoga, kwa kifupi ni mtu asiyejali usafi, nimejaribu kumwambia anasema nisimpangie.
Naomba ushauri wadau nifanyeje?

 Na:Timotheo Mjuni-M&U

Read More
      edit

Monday, December 28, 2015

Published 12/28/2015 12:15:00 PM by with 0 comment

MAPENZI BHANA!...



DENTI ATOROSHWA, AWEKWA KINYUMBA

Boniphace Ngumije

Dunia imekwisha! Binti mwenye umri wa miaka 14 (jina linahifadhiwa kimaadili), mkazi wa Majohe-Kwawarioba, Gongo la Mboto jijini Dar ambaye ni mwanafunzi (denti) wa kidato cha kwanza katika shule moja ya sekondari iliyopo maeneo hayo, anadaiwa kutoroshwa nyumbani kisha kuwekwa kinyumba.

Kwa mujibu wa mama mzazi wa denti huyo, Edna Zacharia, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo juhudi zote alizozifanya kumtafuta mwanaye huyo ziligonga mwamba huku tetesi za mhusika aliyetenda tukio hilo akiwa nazo.

 Binti huyo anayedaiwa kuwekwa kinyumba.

Mzazi huyo alisema kuwa binti yake huyo alianza kufanya jaribio la kutoroka siku moja kabla ya kutimiza azma yake ambapo tofauti na utaratibu wa kawaida, siku hiyo alirejea nyumbani kwa kujifichaficha.

Mama huyo aliendelea kueleza kwamba, baada ya kumhoji mwanaye, alimwambia alikuwa amepoteza shilingi 500 ya mama huyo, hivyo aliogopa kuonekana mbele yake akihofia kupewa adhabu.

Alisema alimsamehe mwanaye na akamwambia aende kulala na mdogo wake lakini kwa kuwa azma yake ilikuwa kutoroka, siku iliyofuata mama huyo aliporejea kutoka kwenye majukumu yake, hakumkuta na baadhi ya nguo zake hazikuonekana.

“Baada ya saa 24 niliripoti tukio hilo kwenye Kituo cha Polisi cha Majohe, nikaandikisha taarifa, tukaanza kumsaka usiku na mchana nikisaidiana na ndugu zangu, tulipata taarifa kuwa yupo kwa kijana muuza mkaa anayefahamika kwa jina la Issa anayeishi Mabibo-External (Dar), tukaenda polisi na kufunguliwa jalada namba STK/RB/1835/15 -KUTOROSHA BINTI CHINI YA HIMAYA YA WAZAZI),” alisema mama huyo.
Edna alisema katika harakati za kumtafuta mwanaye huyo, aliwataarifu baadhi ya ndugu zake akiwemo kaka yake, Damian Ndelwa ambaye mkewe ndiye alikuwa anafahamu mahali alipoonekana binti huyo, ndipo wakakusanyana na baadhi ya watu wake wa karibu kisha kwenda kuvamia kwenye eneo la tukio.

Hata hivyo, mtuhumiwa na denti huyo walikimbia ndipo ndugu hao wakachukua uamuzi wa kwenda kituo cha polisi kilichopo karibu walikoambiwa waendelee kumtafuta kwa kuwa wana RB.

Kuhusu shuleni, Edna alisema mwalimu mkuu na walimu wengine walimshauri kwenda kutafuta msaada kwenye taasisi ya haki na sheria lakini alidai alipofika huko walimrudisha polisi wakimsisitiza kuendelea kumtafuta na kuripoti polisi ikiwa hatapatikana.

Mama huyo aliwaomba watu watakaomuona wawasiliane naye kupitia namba za simu zake za mkononi 0788 291 318, 0769 737 447 au 0672 506 746 au watoe taarifa kwenye kituo cha polisi kilichopo karibu.

Imewekwa na Timotheo Mjuni;M&U

Chanzo:GPL
Read More
      edit
Published 12/28/2015 11:50:00 AM by with 0 comment

UMEUMIZWA NA MAPENZI, SOMA HAPA




UMEUMIZWA, ACHA YAPITE, MAISHA LAZIMA YASONGE

Kujuliana hali ni jadi yetu. Uhali gani mpenzi msomaji wangu? Ni Jumatatu nyingine murua iliyojaa mishemishe za maandalizi ya Sikukuu ya Krismasi, nami nakutakia maandalizi na mnuso mwema.


Wadau wangu, katika mapenzi haijalishi umeumizwa kwa namna gani, iwe kwa kutukanwa, kufumaniwa, kupigwa, kunyanyaswa, kejeli na kila aina ya kuumizwa na mpenzi wako uliyempenda, amini nakuambia, ulipaswa uumie hivyo ili ujifunze au ung’amue kitu f’lani katika ulimwengu wa mapenzi.

Yakupasa pia kuamini kuwa katika historia yako ya maisha hasa ya uhusiano wa kimapenzi ndivyo ulivyoandikiwa kuwa ni lazima ukutane na masaibu hayo ili kutimiza ukurasa wa kitabu chako katika uso wa dunia.

Kila kukicha watu wapya wanaingia kwenye uhusiano, vilevile kuna wengine wanatoka katika uhusiano kwa kuchoshwa na maumivu ya mapenzi hayo, mambo yote

anayotokea katika uhusiano wako yalipaswa na yanapaswa kutokea ili dunia iendelee kama kawaida yake. Usijilaumu sana na kujiona kama mkosaji kwa kuwa tu, eti

meachwa na yule uliyempenda, weka akilini mwako neno hili ‘pamoja na maumivu yote ya mapenzi, lazima maisha yasonge’, haijalishi umeumizwa kwa kiasi gani, swali la msingi la kujiuliza ni je, wewe ndiye wa kwanza kuumizwa kwenye mapenzi? Kama ndiyo wa kwanza basi unaweza kufikiria kukata tamaa, ingawa sikushauri kufanya hivyo hata kama utakuwa wa kwanza.

Pia jihoji katika fikra zako kama siyo wa kwanza, kwa nini uumie na uteseke sana wakati unaona unakoelekea? Unashindwa nini kujiongoza na kufikia hatua ya kushindwa hata kula au kuzungumza na wenzako?
Ni kweli mapenzi yanaumiza sana kuliko kitu chochote unachokifahamu. Maumivu yake ni zaidi ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali, kiukweli maumivu haya ya mapenzi hayaelezeki, mtu pekee anayewaza kueleza maumivu haya yalivyo ni yule aliyokutana nayo, naye hawezi kueleza mfano wake bali vile alivyoumia na kuteseka dhidi ya mapenzi.

Jaribu kufikiria, je, kusingekuwa na mapenzi ungeumia kwa ajili yake? Je, kama usingezaliwa ungeyafahamu vipi hayo mapenzi ambayo leo unayataka?
Kimsingi achana na mawazo hayo, hata kama yanakujia, jitahidi kuyaepuka na kuwaza ni namna gani utasimama tena upya katika maisha yako.

Jikubali, kwamba, unaweza kutimiza na kufikia ndoto zako bila yeye, pengine mwenza wako ndiye aliyekuwa kauzibe ili wewe usifikie malengo yako.

Mpenzi msomaji napenda ‘kushea’ na wewe makala haya, tafadhali tuma maoni yako ni namna gani ulivyoumizwa na kuweza kujiongoza katika kukabiliana na maumivu hayo na wiki ijayo yatatoka kwenye safu hii ya XXlove.

Tukutane tena wiki ijayo kwa mada nzuri na tamu. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook, Whatsapp na Instagram.

GPL
Read More
      edit
Published 12/28/2015 11:37:00 AM by with 0 comment

UMEUMIZA NA MAPENZI SOMA HAPA



UMEUMIZWA, ACHA YAPITE, MAISHA LAZIMA YASONGE-2




Hongera sana mpenzi msomaji kwa kuifikia, kuifurahia na kuimaliza Sikukuu ya Krismasi vizuri ni jambo jema sana na la kumshukuru Mungu.

Niwape faraja na tumaini jipya wale wote wanaofunguka kutokana na makala za uhusiano kupitia safu yetu hii pendwa ya XXLove.

Yafuatayo ni sehemu ya maoni yenu wapenzi wasomaji yaliyotokana na mada yetu ya wiki iliyopita ya ‘Umeumizwa, Acha Yapite, Maisha Yasonge’.

MSOMAJI WA MBEZI BEACH, DAR
Mada nzuri sana, inafundisha, mimi ni mfano; nilikuwa na mchumba wangu tuliyependana ila nilipopata matatizo alinisaliti na kuchukuliwa na mtu mwingine. Hivi sasa amepewa ujauzito. Pamoja na matatizo yangu hanipigii simu wala kutuma ujumbe.

NAITWA EVA JONAS
Mwandishi Mungu akupe maisha marefu, XXLove imenibadili fikra na akili yangu, nilikuwa mtu wa kulia na kuwaza kila siku. Lakini niliposoma mada ya wiki iliyopita nimekuwa mpya kabisa.

JINA KAPUNI
Nimependa mada yako, mimi ni mama wa mtoto mmoja, nina mwaka mmoja kwenye uhusiano ila kwa sasa nimetokea kumchukia mume wangu, hata hamu ya kuwa naye faragha sina, hisia inakuwa ndogo, nifanyeje?

WARDA WA DAR
Nimeishi na mume wangu lakini hivi karibuni kaniacha yapata mwaka sasa, nashindwa kuzoea, nahitaji kuonana na wewe, nina mengi nahitaji unishauri.

JINA KAPUNI- MBAGALA, DAR
Mtaalam kuhusu mzazi mwenzangu, mpaka leo kimya ila nimependa sana mada yako, imenifariji, mapenzi yanaumiza ila kikubwa ni kukubaliana na hali halisi.

BINTI WA KITANGA
Nilishaumizwa sana na hapa nilipofikia sihitaji mwanaume yeyote, najihisi nina nuksi, nimetendwa na wanaume wanne, nifanyeje mtaalam?



MAMA WA FAMILIA
Mimi ni mama wa mtoto wa miezi sita, nimeolewa na nilikuwa namuamini sana mume wangu, juzi nimegundua kuwa tuko wanawake wanne au watano katika uhusiano, kiukweli roho yangu imemkinai sana, namchukia kweli.Mada yako imenifurahisha sana, umenitia moyo kweli, sasa nifanyaje ili aniache?

JINA KAPUNI
Hongera kwa kutuelimisha, naomba unisaidie; mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 21, nilizaa na jamaa f’lani, cha ajabu mwenzangu alianza kubadilika, ghafla akakata mawasiliano, nilishamuomba sana msamaha lakini alikataa, ndugu walinitenga kisa yeye, kibaya zaidi moyo wangu hauko tayari kumsahau na kumpenda mwingine.
Labda alinikimbia kwa sababu ya ujauzito, kama ndivyo basi aje tulee mtoto wetu, ninaomba ushauri.

ROSE WA DODOMA
Nimefarijika sana, mimi ni mmoja wa wanawake niliyepita mateso ya mapenzi, yanaumiza sana, unaweza kumpenda mwanaume ukajidanganya ni wako peke yako kumbe mwenzio ana fikra zake.
GPL

Read More
      edit

Saturday, December 26, 2015

Published 12/26/2015 09:19:00 PM by with 0 comment

WAZIRI NAPE KATIKA UBORA WAKE WA KUIMBA PAMBIO

Tazama Video ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiimba moja ya pambio katika Tamasha la Krismasi lililofanyika jana Ukumbi wa Diamond Jublee, jijini Dar.
Read More
      edit

Wednesday, December 23, 2015

Published 12/23/2015 10:08:00 PM by with 0 comment

SINA HAMU YA KUKUTANA FARAGHA NA MKE WANGU, NAMCHUKIA

Mimi ni kijana, nilikutana na mke wangu kwenye graduation miaka 2 iliyopita, tulipendana na kuanzisha uhusiano, wakati huo yeye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha tatu, katika mapenzi nilijikuta nimempa ujauzito ikabidi aache shule, kwa kuwa sikuwa na nia naye mbaya nilienda kwa wazazi wake na kuzungumza nao, wakakubali niishi naye.
Tuna mwaka sasa na tumefanikiwa kupata mtoto mmoja, lakini kusema ukweli nina muda sasa sijihisi hamu yoyote ya kukutana faragha na mke wangu, sijui nini tatizo?!, naomba ushauri wenu nifanye nini? na bado nampenda sana mke wangu.
Read More
      edit

Tuesday, December 22, 2015

Published 12/22/2015 07:16:00 PM by with 0 comment

CHANZO MAPENZI




Mo Music kafikishwa Mahakamani Dodoma… chanzo ni Mwanamke

HIVI ndivyo mapenzi yanavyorani dunia, mwimbaji wa hit single ya ‘basi nenda‘ ambaye sasa hivi anatambana na kwenye vituo mbalimbali vya Radio kupitia single ya ‘skendoMo Music, anasema mwaka 2015 kwake umemalizika na huzuni baada ya kushtakiwa Mahakamani kwa kisa kilichoanzia kwa Mwanamke, kesi yake imetajwa December 21 2015.
Alikua ni mpenzi wake wa zamani, toka wameachana ni zaidi ya miezi nane imepita na Mwanamke huyo alikwenda kwa Mwanaume mwingine na kuchukua mamilioni ya pesa alafu mwisho wa siku  Mo Music amekuja kutajwa kuhusika na upoteaji wa pesa hizo.
Chanzo: Millard Ayo.
Read More
      edit