UMEUMIZWA, ACHA YAPITE, MAISHA LAZIMA
YASONGE
Kujuliana
hali ni jadi yetu. Uhali gani mpenzi msomaji wangu? Ni Jumatatu nyingine murua
iliyojaa mishemishe za maandalizi ya Sikukuu ya Krismasi, nami nakutakia
maandalizi na mnuso mwema.
Wadau
wangu, katika mapenzi haijalishi umeumizwa kwa namna gani, iwe kwa kutukanwa,
kufumaniwa, kupigwa, kunyanyaswa, kejeli na kila aina ya kuumizwa na mpenzi
wako uliyempenda, amini nakuambia, ulipaswa uumie hivyo ili ujifunze au
ung’amue kitu f’lani katika ulimwengu wa mapenzi.
Yakupasa
pia kuamini kuwa katika historia yako ya maisha hasa ya uhusiano wa kimapenzi
ndivyo ulivyoandikiwa kuwa ni lazima ukutane na masaibu hayo ili kutimiza
ukurasa wa kitabu chako katika uso wa dunia.
Kila
kukicha watu wapya wanaingia kwenye uhusiano, vilevile kuna wengine wanatoka
katika uhusiano kwa kuchoshwa na maumivu ya mapenzi hayo, mambo yote
anayotokea
katika uhusiano wako yalipaswa na yanapaswa kutokea ili dunia iendelee kama
kawaida yake. Usijilaumu sana na kujiona kama mkosaji kwa kuwa tu, eti
meachwa
na yule uliyempenda, weka akilini mwako neno hili ‘pamoja na maumivu yote ya
mapenzi, lazima maisha yasonge’, haijalishi umeumizwa kwa kiasi gani, swali la
msingi la kujiuliza ni je, wewe ndiye wa kwanza kuumizwa kwenye mapenzi? Kama
ndiyo wa kwanza basi unaweza kufikiria kukata tamaa, ingawa sikushauri kufanya
hivyo hata kama utakuwa wa kwanza.
Pia
jihoji katika fikra zako kama siyo wa kwanza, kwa nini uumie na uteseke sana
wakati unaona unakoelekea? Unashindwa nini kujiongoza na kufikia hatua ya
kushindwa hata kula au kuzungumza na wenzako?
Ni
kweli mapenzi yanaumiza sana kuliko kitu chochote unachokifahamu. Maumivu yake
ni zaidi ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali, kiukweli maumivu haya ya mapenzi
hayaelezeki, mtu pekee anayewaza kueleza maumivu haya yalivyo ni yule
aliyokutana nayo, naye hawezi kueleza mfano wake bali vile alivyoumia na
kuteseka dhidi ya mapenzi.
Jaribu
kufikiria, je, kusingekuwa na mapenzi ungeumia kwa ajili yake? Je, kama
usingezaliwa ungeyafahamu vipi hayo mapenzi ambayo leo unayataka?
Kimsingi
achana na mawazo hayo, hata kama yanakujia, jitahidi kuyaepuka na kuwaza ni
namna gani utasimama tena upya katika maisha yako.
Jikubali,
kwamba, unaweza kutimiza na kufikia ndoto zako bila yeye, pengine mwenza wako
ndiye aliyekuwa kauzibe ili wewe usifikie malengo yako.
Mpenzi
msomaji napenda ‘kushea’ na wewe makala haya, tafadhali tuma maoni yako ni
namna gani ulivyoumizwa na kuweza kujiongoza katika kukabiliana na maumivu hayo
na wiki ijayo yatatoka kwenye safu hii ya XXlove.
Tukutane
tena wiki ijayo kwa mada nzuri na tamu. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa
Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook, Whatsapp na Instagram.
GPL
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.