Wednesday, December 23, 2015

Published 12/23/2015 10:08:00 PM by with 0 comment

SINA HAMU YA KUKUTANA FARAGHA NA MKE WANGU, NAMCHUKIA

Mimi ni kijana, nilikutana na mke wangu kwenye graduation miaka 2 iliyopita, tulipendana na kuanzisha uhusiano, wakati huo yeye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha tatu, katika mapenzi nilijikuta nimempa ujauzito ikabidi aache shule, kwa kuwa sikuwa na nia naye mbaya nilienda kwa wazazi wake na kuzungumza nao, wakakubali niishi naye.
Tuna mwaka sasa na tumefanikiwa kupata mtoto mmoja, lakini kusema ukweli nina muda sasa sijihisi hamu yoyote ya kukutana faragha na mke wangu, sijui nini tatizo?!, naomba ushauri wenu nifanye nini? na bado nampenda sana mke wangu.
      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.