Mpenzi msomaji, wiki iliyopita
niliishia pale fundi Yassin alipomtambulisha Nelly kwa Zakayo aliyekuwa
akimsaidia kazi na kwamba wangekuwa wote kazini jambo ambalo Zakayo hakuamini
kufuatia muonekano wa kisharobaro wa Nelly. Je, kilifuatia nini? Songa mbele…
Baada ya utambulisho huo, fundi na
vijana wake waliendelea na safari ya kwenda site lakini Zakayo alikuwa bado
aamini kama Nelly aliyeonekana sharobaro angefanya kazi ya kubeba zege.
Walizidi kupiga stori za hapa na pale
huku Nelly akistaajabu majumba makubwa ya kisasa yaliyojengwa ambapo fundi
Yassin akawa anamuonesha majengo kadhaa ambayo alikuwa amechangia kuyajenga.
Baada ya kutembea kama dakika saba
hivi, Nelly alishangaa wakiwa wapo kwenye bonge ya jumba lenye geti kubwa
jeusi, fundi Yassin akamwambia walikuwa wamefika site.
Kauli ya fundi huyo ilimshangaza Nelly
kwa sababu hakuona nyumba iliyokuwa ikijengwa lakini hakumwuliza hadi fundi
Yassin alipobonyeza kengele ya getini ndipo alitokea binti mmoja mrembo
akafungua, Nelly alipomuona moyo wake ulipiga paa!
“Kumbe ni wewe fundi umekuja,
karibuni!” mrembo huyo alimwambia fundi Yassin huku akimtupia macho Nelly.
“Asante Doreen, vipi bosi yupo?” fundi
Yassin alimwuliza Doreen.
Baada ya kuulizwa hivyo, msichana huyo
ambaye alikuwa akimwangalia Nelly kwa kuibia alimfahamisha kwamba baba na
mama yake walisafiri alfajiri ya siku
hiyo kwenda Arusha.
“Eh! Mbona jana hakuniambia na vipi
kuna maagizo aliyokuachia?” Fundi Yassin alimwuliza Doreen.
“Kaniambia kila kitu mtazungumza kwenye
simu,” Doreen alimfahamisha fundi.
Baada ya kuambiwa hivyo fundi
alimtambabulisha Nelly kwa Doreen na kumwambia watakuwanaye pale kazini kisha
akamtambulisha Doreen kwa kijana huyo mwenye dimponsi.
“Yaani naye ni fundi au amekuja
kutembea ni ndugu yako?” Doreen alimwuliza fundi kwani kwa jinsi alivyomuona
Nelly hakufanana kabisa na kazi za ujenzi alizokuwa akizifanya fundi Yassin.
“Yeah! Atakuwa ananisaidia kazi kama
wanavyofanya akina Zakayo na wenzake,” fundi Yassin alimfahamisha Doreen bila
kujua ni namna gani Nelly aliumia moyoni.
“Da yaani fundi badala ya kusema mimi
ndugu yake nimekuja kutembea anaweka wazi kila kitu kwa huyu mtoto mkali,
kaharibu kinoma!” Nelly alizungumza kimoyomoyo.
Baada ya fundi kutoa kauli hiyo, Doreen
ambaye hakuamini kama ni kweli Nelly alikuwa fundi alifunga geti kisha
alimwambia fundi Yassin alikuwa ndani na kama watahitaji kitu wamwite Anne
ambaye alikuwa msichana wao wa kazi.
Wakati fundi Yassin akitoa utambulisho
huo, Zakayo alikuwa amekwisha zunguka nyumba ya nyumba hiyo ambako kulikuwa na
jengo lingine lililokuwa likijengwa.
“Nelly hapa ndipo site ninapofanya kazi
mwezi wa pili sasa, nyumba yah ii nyumba bosi wangu anaangusha mjengo
mwingine,” fundi Yassin alimwambia Nelly.
Fundi alimwongoza Nelly hadi eneo hilo
ndipo kijana huyo mwenye dimponsi ambaye akili yake ilikuwa kwa Doreen alibaki
akishangaa ukubwa wa jumba la yule bosi na ingine aliyokuwa akijenga kwa nyuma
yake.
“Kweli kuna watu wana fedha jamani,
mijengo yote hii ya mtu mmoja?” fundi Yassin alimwuliza fundi.
“Wewe unashangaa nyumba hii, ukienda
huko mbele ndiyo balaa watu wamefanya kufuru balaa,” fundi Yassin alimwambia
Nelly.
Walipofika kwenye nyumba ya pili ambayo
ilikuwa ikiwekwa malumalu, walimkuta kijana mwingine akipanga malumalu,
alipomuona fundi Yassin alimwamkia.
Baada ya kumwamkia, alimtazama kwa
makini Nelly na kumwambia; “Vipi Mambo?”
“Poa, za kazi?” Nelly alimsabahi.
“Nzuri, karibu!” kijana huyo
alimkaribisha Nelly aliyesema asante.
“Hatuni, huyu hapa anaitwa Nelson
Nzamba lakini tunapenda kulikatisha jina lake na kumwita Nely, ni jirani yangu
tutakuwanaye pamoja kwenye kazi zetu,” fundi Yassin alimtambulisha Nelly kwa
Haruni.
Kufuatia utambulisho huo, kama
ilivyokuwa kwa Zakayo, Haruni hakuamini kwa muonekano wa Nelly kama alifanana
na kazi za kukoroga zege, akamwuliza:
“Fundi bwana kwa masihara umezidi,
yaani atakuwa akikoroga zege na kukubeba matofali, malumalu kama sisi?”
“Ndiyo, kwani unamuonaje?” fundi
alimwuliza Haruni.
“Hata mimi nimemuuliza kama wewe kaniambia hivyohivyo,” Zakayo
akadakia.
“Kama nilivyowaleza naye tutakuwa
tunafanya naye kazi,” fundi Yassin aliwaambia.
Kule ndani, Doreen kama ilivyokuwa kwa
akina Harunu na Zakayo, akawa haamini kabisa kama Nelly ni fundi.
“Huyo kijana piga ua garagaza siyo
fundi, nahisi atakuwa kaja kumpeleleza baba yangu, sijawahi kumuona sharabaro
tena anayevaa miwani na mwenye dimponsi anafanya kazi za ujenzi,” Doreen
aliwaza.
Usikose
sehemu inayofuatia ya chombezo hii
NELLY MUOSHA MAGARI POSTA-5
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.