Kazi yake ya bodaboda, uaminifu,
ustaarabu na upole aliokuwa nao kwa wateja wake ndiyo hasa uliomfanya Joakim
kuwa na wateja wengi sana katika eneo lake la kazi (Kijiwe kama wengi
wanavyoita), lililopo Sinza Makaburini jijini Dar.
Wafanyakazi, wanafunzi,
wafanyabiashara na wengineo wanaoishi maeneo hayo ya
jirani walipenda sana kumtumia Joakim
katika shughuli zao mbalimbali kama kuwabebea mizigo yao na kuwapelekea
nyumbani hata kwenye mishemishe zao za kila siku, jina lake likafahamika na kuwa
maarufu sana miongoni mwa wafanyabiashara ya usafiri wa pikipiki maaruku kama
'bodaboda,'na kujikua akibadilishwa jina na wateja wake kutoka Joakim na
kufupishwa kwa kuitwa Kim.
Ugumu wa maisha ndiyo ambao ulipelekea
Kim kutoroka kijini kwao Mkoani Morogoro na kukimbilia jijini Dar ili
kujikwamua katika ugumu wa maisha aliokabiliana kama ilivyo kwa Watanzania wengi.
Alipofika jijini haku na ndugu yeyote wala jamaa jambo lililopelekea miezi kadhaa
kulala katika Kituo cha Mabasi yaenda Mikoani cha Ubungo, na hatimaye akawa
maarufu sana kituoni hasa kutokana na kujishughulisha kazi ya kubeba mzigo ya
abiria kama wafanyavyo vijana wengine.
Aliendela na kazi hiyo kwa uamini kwa
sababu ni sehemu ya talanta yake aliyozaliwa nayo, na aliaminika zaidi na hata
baadhi ya vijana wenzake na hata viongozi wa kituo hicho, hasa katika kufanya
kazi na kupata hesa ya
halali kuliko kumtendea mabaya
binadamu mwingine.
Maisha yalizidi kusonga na akiendelea
na kazi ya ukuli kwa kubeba mizigo ya abiria wanaoingia kwa wingi na kutoka Kituo
cha Ubungo kila siku.
Baada ya kukaa kwa muda mrefu akifanya
kazi ya ukuli akabaini ili aweze kukabiliana na kasi ya Serikali ya Awamu ya
Tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli inabidi afikirie namna ya kujikwamua au
kufanya kazi nyingine ambayo itamsaidi maisha yake. Kitu cha kwanza
harakaharaka alichokifikiria kukifanya ni kujifunza udereva kwani elimu yake ya
darasa la nne ndiyo ilimpa shaka sana ya kupata kazi nyingine.
Alijipinda kwa miezi sita akipigana
huku na kule kuhakikisha amepata shilingi laki moja ambayo itamsaidia kulima
hela kwa mmoja wa madereva wa pikipiki ili amfundishe lakini pia hela ile
imsaidie katika matumizi yake ya kila siku. Hatmaye Kim alifanikiwa kutunza kiasi cha pesa alichokihitaji na ndipo hapo
alipopata nguvu ya kwenda kwa Yule dereva wa pikipiki aliyekuwa anamfikiria na
kuongea naye kuhusu kumfundisha kuendesha.
Kwa kuwa hakuwa anatania alifika na
kuongea naye kasha akatoa noti ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi yule dereva
wa pikipiki na kumwambia anaomba awe anamfundisha kuendesha kama yeye, jamaa
alikubali kwa haraka na kumuona Kim kama mtu aliyejua shida yake ya siku hiyo
kwani pamoja na siku kuwa inaelekea kuisha hakuwa amekamilisha hesabu ya bosi
wake jambo lililokuwa linamuumiza sana akili na kufikiria mtu wa kumkopa
ilimradi tu akamilishe hesabu ya bosi wake.
Walipanga siku na muda wa kuanza kujifunza
namna ya kuendesha pikipiki na hatimaye baada ya mwenzi mmoja Kim akawa
amefahamu kuendesha pikipiki na kuifanya roho yake kuwa na shauku ya kupata pikipiki
ya kuendesha kama njia moja wapo ya kufanya biashara na ikiwezekana aache
kabisa pale Ubungo.
Haikuwa kazi ngumu sana kwa Kim kupata
pikipiki kwani yuleyule mwalimu wake wa kuendesha ndiye aliyemsaidia kupata
pikipiki kwa kumuunganisha na mmoja wa mama ambaye alikuwa amenunu pikipiki
mbili baada ya kupata kiinua mgongo chake. Mama Yule alipomuona Kim alivutiwa
naye na nkumuamini kasha akampa pikipiki yake kwa sharti la kuitunza na
kuipenda kama yak wake.
Ni Alfajiri ya Jumatatu Kim aaliamaka
kwenda kwa mama mwenye pikipiki na kuichukua kasha kuelekea nayo katika kijiwe
kilichopo Sinza Makaburini na kupaki pikipiki yake mpya kwa ajili ya kusubiri
wateja kama wafanyavyo wenzake, baada ya wiki, mwezi na hatimaye miezi Kim
alikuwa kishafahamika sana na kuwa na wateja kibao wa kuwasafirisha sehemu
mbalimba za Jiji la Dar.
Ni mwaka sasa umekatika Kim akiwa amefanikiwa kuwa na geto lake nzuri
lenye godolo moja, kitivi cha kiaina ba baadhi vyombo vya kuwekea maji pindi
anaporudi kutoka kwenye mizunguko yake. Akiwa bado yuko eneo lake la kazi
akijiandaa kuondoka ghafla akatokea msichana mmoja mzuri sana kimuonekano
lakini alikuwa amevaa nusu uchi, wakati Kim akiendelea kumshangaa mrembo yule,
akazidi kushangaa zaidi kuona mrembo yule anazidi kumsogelea. Wakati huo
ilikuwa ni majira ya saa 3 usiku, wenzake wakiwa wameishatawanyika makwao.
Je, mrembo yule atakuwa ni nani? na
anataka nini kwa Kim?
Na M&U
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.