Tuesday, March 29, 2016

Published 3/29/2016 07:09:00 PM by with 0 comment

USALITI WA MME WANGU UNAVYONITESA FARAGHA





Mimi ni mwanamke wa miaka 36, nina mme na watoto 3, sikuwahi kumjua mume mwingine zaidi ya huyu aliyeninitoa usichana wangu (bikra) na kunioa, sijawahi kumsaliti hata mara moja ila yeye kabla hajanioa aliwahi kuoa na kupata mtoto mmoja (kwangu atakuwa wa nje) ila baadaye aliachana na huyo mwanamke kwa talaka na wakati anamuacha kumbe yule mwanamke alikuwa mjamzito.

Baada ya muda alijifungua na mume wangu alikuwa akienda kimyakimya kwa mwanamke yule, niligundua na kumuuliza, akaniambia huwa anakwenda kumuangalia mtoto wake na si kingine, nikasema sawa hila hivi karibuni nimegundua ana mwanamke mwingine tena, roho ikaniuma sana kwani najitahidi kumfanyia kila anachostahili kama mwanaume lakini wapi, nampa penzi zuri kwa staili zote, nampikia chakula kizuri, nambembeleza lakini naona halidhiki, kiukweli imeniumiza na kuniathiri kisaikolojia.
Kuna siku alihisi kama nimegundua akanibembeleza na kuniomba msamaha kuwa hatorudia tena, nimemsamehe lakini tatizo linakuja pale tunapokuwa faragha, mimi huwa linaniijia tukio lile la mwanamke wake wa pili na kujikuta nikipoteza ladha ya penzi na kuanza kulia kwa uchungu wa kunisaliti, imefika mpaka kipindi sikojoi tena wakati awali alikua akinikojolesha mara kwa mara.

Kinachonishangaza akiwa kazini nakuwa na hamu naye na ashiki hunipanda sana, nikifanya naye mapenzi ya kwenye simu (kwa njia ya simu) naridhika kuliko akinifanya laivu. Unanishauri nifanyeje kwa tukio hili?.
 Na:M&U
Kwa Ushaur, habari, simulizi, machombezo na mikasa ya kweli ya MAPENZI tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com ,Insta:mimi_na_uhusiano au like Facebook page yetu ya Mimi na Uhusiano
      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.