Katika ulimwengu wa sasa ambao ajira zimekuwa ngumu na shida kupatikana, ujasiriamali na biashara vimekuwa ndio kimbilio la wengi. Watu wengi wanaingia kwenye biashara kama njia kuu ya kujipatia kipato.
Pamoja na biashara kuonekana kuwa kimbilio la wengi sio wote wanaoingia kwenye biashara wanafanikiwa. Tafiti zinaonesha kwamba asilimia tisini ya biashara zinazoanzishwa zinakufa mwaka mmoja baada ya kuanzishwa. Na hata hizo zinazovuka mwaka mmoja asilimia tisini hufa baada ya miaka mitano. Hivyo kama mwaka huu zimeazishwa biashara mia moja basi miaka mitano ijayo ni biashara moja tu itakayokuwa bado inadumu.
Kwa nini biashara nyingi zinashindwa kudumu?
Biashara nyingi zinakufa kutokana na ukosefu wa elimu muhimu kuhusiana na biashara na ujasiriamali. Watu wengi wanaoingia kwenye biashara wanaingia kwa kuangalia tu ni kitu gani watu wengine wanafanya na wao kufanya hivyo hivyo.
Biashara ni rahisi sana kufanya ila ni ngumu kuendesha na kuikuza mpaka iweze kukupa faida kubwa sana. Ili uweze kuendesha na kukuza biashara itakayokupa faida kubwa ni muhimu kuchukua muda na kujifunza vitu vya muhimu vinavyohusiana na biashara.
Leo tutajifunza misingi mitano muhimu ya biashara ambayo kila biashara inatakiwa kuizingatia. Wewe kama mjasiriamali una jukumu la kujifunza na kufuata misingi hii ili uweze kufikia malengo yako kwenye ujasiriamali na biashara.Misingi mitano muhimu ya biashara.
Ili biashara yoyote iweze kudumu na kukua inahitaji kufuata misingi ifuatayo.- Kutengeneza thamani.
- Soko.
- Kuuza.
- Kufikisha thamani.
- Fedha.
Misingi hii mitano ni muhimu sana kwa biashara. Hakuna msingi ambao unaweza kusema ni muhimu zaidi ya mwingine, yote inategemeana. Ili biashara yoyote iweze kudumu ni muhimu kuzingatia misingi hiyo.
BY: TATU KIONDO