“KILA JAMBO LINA WAKATI WAKE”
Wakati
au muda ni kitu ambacho hakina mipaka. Hakuna jambo au kitu kisichokuwa
na wakati wake na mwisho wake. Kwa maana kuwa, muda/time ndio suluhisho
la mambo mengi. Kila jambo lina mwisho na wakati wake. Hata shida ulizo
nazo zina kikomo chake ambacho zitaisha. Kila unapokuwa katika kipindi
kigumu tambua kuwa kipindi hicho kitapita tu kwani kina mwisho wake.
Lakini pia kumbuka kuwa hata unapokuwa katika kipindi cha raha, nacho
kina mwisho wake. Hivyo ukiwa katika tafakari hizo katika shida na raha,
ridhika na kila ulichonacho.
2 - “UNAWEZA KUWA NA FURAHA PALE UNAPOAMUA KUWA NA FURAHA, KWANI FURAHA NI MTAZAMO WA MTU NA SIO UHALISIA KAMILI”
Umeshawahi
kujiuliza furaha maana yake ni nini? Inaweza ikawa na maana tofauti kwa
watu tofauti mfano, wapo wanaoona furaha ni pesa, wengine huona furaha
ni kutenda mema, wengine hutafsiri furaha ni raha, urembo au chochote
ambacho wanaona kinawapa furaha. Lakini ukweli ni kuwa, furaha ni fikra.
Unaweza kuwa na furaha pale unapoamua kuwa na furaha hata kama
mazingira na hali iliyokuzunguka inakupa huzuni. Angalia katika maisha
yako, shukuru kwa kila jambo na weka mtazamo chanya katika mawazo na
fikra zako.
3 - “SHUKURU KWA KILA JAMBO”
Kila
kitu kina faida na hasara yake. Badala ya kulaumu kila kitu katika
maisha yako unaweza kuangalia katika upande mwingine. Mfano, badala ya
kuumia na kupoteza muda katika kufikiria ni changamoto gani unazo katika
maisha unaweza kubadilisha mtazamo wako na kuangaliza faida za
changamoto katika maisha na kuacha kuwaza maumivu yake. Changamoto
hutujenga katika maisha na bila changamoto huwezi kuendelea mbele.
Tuzidi kuchukuru kwa kila jambo katika maisha.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa