Tuesday, July 25, 2017

Published 7/25/2017 04:52:00 PM by with 0 comment

MAJI YA MCHELE HAYAONJWI



Nakuona vile jicho kodo kisa kuangalia eti leo atamchamba nani? Unikome, sipo hapa kumchamba mtu miye! Hapa unapata elimi bibi wewe kama ulikuwa hujui, upo?

Kwanza nikusalimu mwenzangu maana nikiaanza kutiririka utafikiri maji ya mtoni yameachiwa njia na kuingia kwenye makazi ya watu, shoga yangu u salama! Mwenzako kama ulivyoniacha nimejaa tele MC mimi, kama mgojwa basi ni jambo la kuombeana tu!

Tuingie kwenye mada yetu, jamani hivi muoaji wa kweli humuonja mwanamke ndipo amuoe kweli? Mmh! Simpendi jamani mwanamke mwenzangu kugeuzwa chungu cha mboga kuingizwa mkono na kuonja. Utaonjwa na wangapi mwisho wa siku unabaki kituko cha mtaa!

Juzi shoga nilipata malalamiko, msichana mmoja aliyefuatwa na mwanaume mtu mzima ambaye ni mume wa mtu na kumuomba awe mkewe kutokana na mkewe kuwa na matatizo ambayo siwezi kuyaanika hapa.

Kwa kweli mwari huyu alitatizika kuolewa ukewenza kuhofia kujiingiza katika vita ya ndani, lakini yule mwanaume alimuhakikishia kuwa kuoa mke mwingine alipata ruksa kutoka kwa mkewe. Mtoto wa kike kiguu na njia mpaka kwangu na kuniuliza akubali au akatae, loo! Kwa vile najua ukewenza si dhambi nilimweleza akubali.

Baada ya hapo tulipotezana na kuonana juzi akiwa anatokwa na michozi tikwatikwa kama majeruhi wa mafuriko. He! Mwari kulikoni? Nilimuuliza, jibu eti tangu wakati ule ndoa imekuwa kitendawili, kauli ile ilinishtua na kuuliza bado anaye? Jibu, ndiyo. Nilishangaa kasi ya awali na kuamini ndoa ingekuwa ndani ya wiki, lakini umevuka mwaka upo tu!

Mtoto wa kike niliinama chini kuwaza na kuwazua ili kutaka kujua sababu ya mwari wangu kuiona ndoa kama daladala inayopita mbele yake kwenda na kurudi. Kwa vile mimi ni ng’ombe mzee niliyepita mazizi mengi nilipata jibu na kumuuliza.

Tangu wakati ule umeshamuonjesha mwili wako? Jibu lilikuwa lilelile nililowaza kuwa alimpa baada ya msimamo wa muda mrefu na kuamini kumvulia nguo ingeharakisha ndoa kumbe siyo. Siku zote huwa sipendi kumlaumu mtu kwa kosa alilolifanya kwa bahati mbaya, lakini huwa simpendi mtu anayerudia kosa moja mara mbili kama mnyama na mwisho wa siku aombe ushauri, haipendezi.

Jamani wari wangu, mimi nimeamua kutoa elimu ya bure kupitia gazeti hili kwa nini msiichukue. Usiniangalie mimi, angalia ninachokueleza ambacho huwa ni faida kwenu. Jamani hebu basi tuwe na msimamo kujitoa kimwili si njia ya kuharakisha ndoa bali kujidhalilisha.

Mwanaume kama kweli anakupenda na kutaka uwe mwenza wake, kwa nini awe na haraka ya kutaka kukuonja kwanza? Sasa umeonjwa na kuonekana si mtamu ndiyo uachwe? Kwa mtindo huo utaonjwa na wanaume wangapi shoga wewe! Kama ulikuwa hujui mwenzangu, maji ya mchele hayaonjwi na ukilazimisha hutaiona ladha, upo?

Mila na desturi yetu Waafrika ni kuchunguza tabia ya mtu si kuujua utamu wake, jamani haya yametoka wapi kuonjwa ndipo uolewe? Umekuwa pombe ya kienyeji? Ehee heee heeeiyaaa! Hilo nalo neeno!

Nawaasa wanawake wanaojiandaa kuolewa au kuwa na wachumba wasitoe miili yao ovyo, kama wanataka kuitumia wataipata baada ya ndoa, lakini wakijiroga kuitoa basi wajue itakula kwao, watatumiwa na mwisho wa siku kutupwa kama makaratasi ya kufungia maandazi au vitumbua.

 Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa


 CHANZO:GPL
Read More
      edit

Tuesday, July 18, 2017

Published 7/18/2017 01:13:00 PM by with 0 comment

RAYVAN ASEMA MPENZI WAKE AWEZI KUCHUKIA BAADA YA KUIONA VIDEO YAKE AKIWA NA GIGY

Baada ya video yake yenye utata na video vixen Gigy Money kusambaa, msanii wa Bongo Flava Rayvanny amesema Baby Mama wake ‘Fahyma’ hawezi kuchukia.

Mshindi huyo wa tuzo ya BET 2017 akiwa chini ya label ya WCB, ameiambia Times Fm kuwa yeye na mpenzi wake hawachungani, hivyo jambo hilo alilichukulia kawaida.
“Hawezi kuchukia, halafu pia mimi sichungwi am live my life, president of own life, so nobody anaweza akaingilia akasema usifanye hiki, so Fahyma hana noma sometimes anaweza akafanya vitu vyake mimi simuingilii,” amesema Rayvanny.

Kuhusu ukaribu wake na Gigy Money, Rayvanny amesema, “It’s just a joke, Gigy ni mshikaji wangu na ni wa Mbeya pia, namjua before hajanza mbwembwe zake na ni mtu ambaye yupo happy muda wote mimi naona anaenjoy maisha yake”. Rayvanny na Fahyma amejawali mtoto mmoja wa kiume aitwae Jaydan.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

CHANZO: BONGO5
Read More
      edit
Published 7/18/2017 01:03:00 PM by with 0 comment

RAYVAN ASEMA MPENZI WAKE AWEZI KUCHUKIA BAADA YA KUIONA VIDEO YAKE AKIWA NA GIGY

Baada ya video yake yenye utata na video vixen Gigy Money kusambaa, msanii wa Bongo Flava Rayvanny amesema Baby Mama wake ‘Fahyma’ hawezi kuchukia.

Mshindi huyo wa tuzo ya BET 2017 akiwa chini ya label ya WCB, ameiambia Times Fm kuwa yeye na mpenzi wake hawachungani, hivyo jambo hilo alilichukulia kawaida.
“Hawezi kuchukia, halafu pia mimi sichungwi am live my life, president of own life, so nobody anaweza akaingilia akasema usifanye hiki, so Fahyma hana noma sometimes anaweza akafanya vitu vyake mimi simuingilii,” amesema Rayvanny.

Kuhusu ukaribu wake na Gigy Money, Rayvanny amesema, “It’s just a joke, Gigy ni mshikaji wangu na ni wa Mbeya pia, namjua before hajanza mbwembwe zake na ni mtu ambaye yupo happy muda wote mimi naona anaenjoy maisha yake”. Rayvanny na Fahyma amejawali mtoto mmoja wa kiume aitwae Jaydan.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

CHANZO: BONGO5
Read More
      edit

Monday, July 17, 2017

Published 7/17/2017 07:41:00 PM by with 0 comment

MUUGUZI MBARONI KWA KOSA LA KUBAKA


MUUGUZI anayefanya kazi Kituo cha Afya Kata ya Igurubi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Damian Mgaya (26) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumbaka binti wa miaka 18 mkazi wa kitongoji cha Mwagala B, Kijiji cha Mwagala.

Mtendaji wa Kata ya Igurubi, Ntemi James alisema uhalifu huo umefanyika Julai 14, mwaka huu saa 8 hadi alfajiri wakati binti huyo akimuuguza mama yake, Tatu Simbi ambaye amelazwa katika kituo hicho cha afya baada ya kushambuliwa kwa kipigo na mume wake. James alidai mtuhumiwa alimpokea mama wa binti huyo akiwa hoi na ndipo alimpatia matibabu kisha kumlaza katika kituo hicho cha afya huku akimchoma sindano ya usingizi ambayo ilisababisha mama huyo kupitiwa na usingizi.

Mtendaji huyo alidai kuwa muuguzi Damian alipoona mama wa binti huyo amelala, alimwambia waende wote chumba kingine ili akachukue dawa ya mama yake; lakini hata hivyo hakumpa dawa na badala yake alimwambia amchome sindano ili asipate maradhi kwa kuwa mazingira ya hospitali sio mazuri. Baada ya kuambiwa hivyo, binti huyo alikubali kuchomwa sindano mbili na alipochomwa sindano ya kwanza aliishiwa nguvu na alipochomwa sindano ya pili alianguka na kupitiwa na usingizi hadi asubuhi.

Alisema baada ya kuona amelala pasipokuwa na fahamu, muuguzi huyo alianza kumbaka hadi alfajiri alipoamshwa na mama yake huku yeye akiwa hajitambui kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia sehemu zake za siri na mwili wote. Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bonaventura Kalumbete alithibitisha kubakwa kwa binti huyo na muuguzi huyo na kueleza kuwa baada ya kupata taarifa hiyo, alituma timu ya wataalamu ambayo ilibaini binti huyo kubakwa na amelazwa kwenye kituo hicho na hali yake ni mbaya kwani hawezi kutembea.

Aidha, Dk Kalumbete alisema uchunguzi wa awali unaonesha binti huyo alichomwa sindano wakati alikuwa hata haumwi na hizo dawa nazo zimechangia kumsababishia kushindwa kutembea huku akiahidi kuwa baada ya uchunguzi, muuguzi huyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.


Mkuu wa Wilaya ya Igunga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, John Mwaipopo alikiri kukamatwa kwa muuguzi baada ya kupokea taarifa ya kubakwa kwa binti huyo, alimwagiza Mkuu wa Polisi Igunga kumkamata muuguzi huyo Damian Mgaya ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.



Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

CHANZO:GPL
Read More
      edit

Sunday, July 16, 2017

Published 7/16/2017 02:21:00 PM by with 0 comment

MAMBO 4 YA KUJENGA UTAJIRI HATA KAMA UMEZALIWA KWENYE FAMILIA MASKINI



Idadi ya tuliowengi bila  ya kujali ni maskini au tajiri  tumezaliwa katika familia maskini. Hata unapoona wengine wanakuwa wamefanikiwa sana, hiyo haina maana kwamba wao wametakotea katika koo au familia za kifalme, bali ni matokeo ya nguvu na juhudi zao wenyewe.
Kwa mantiki hiyo inamaanisha hivi, ili uweze kupata utajiri, mbali na juhudi binafsi zipo sheria ambazo mtu anatakiwa azifuate ili kufikia lengo hilo. Na kwa kufuata sheria hizo haitajalisha wewe umetokea katika familia gani au umetokea katika nchi au wewe ni wa rangi ipi ni lazima utafanikiwa.
Kwa kusoma makala haya ya leo, utajifunza sheria chache za msingi ambazo mtu unatakiwa uwe nazo au uzifahamu ili zikusaidie kujenga utajiri hata kama umetokea familia maskini. Uwezo wa kufikia utajiri unao tena sana, ni suala la kuamua na kuanza kutekeleza sheria za mafanikio. Sheria hizo ni zipi? Twende pamoja katika somo.
 1. Tengeneza tabia za kukuwezesha kuwa tajiri.
Utajiri haujengwi kwa bahati mbaya hata kidogo. Zipo tabia ambazo unatakiwa uzijenge ili zikusaidie kutengeza msingi imara wa utajiri unaotaka kwenye maisha yako. Tabia ya kujiwekea akiba,  kutunza muda na kujenga maamuzi sahihi ya kimafanikio ni moja ya tabia bora ambazo ukiziendeleza kwa muda zinakupa mafanikio ya wazi.
Angalia sana katika maisha yako usije ukajuta kwa sababu ya tabia zako mbaya ambazo zitakuangusha  na kukufanya ukashindwa kufikia utajiri. Kuwa makini na tabia hizo, jikague na jenga tabia za kukuwezesha kufanikiwa. Kwa kadri unavyojenga tabia hizi kila siku, ndivyo utazidi kukaribia mafanikio yako kwa sehemu kubwa.

2. Fanya kazi kwa juhudi sana.
Ikiwa ndio unaanzia chini kabisa huna kitu, hakuna kitakachoweza kukutoa hapo ulipo zaidi ya kufanya kazi kwa juhudi sana. Hapa inabidi ufanye kazi kwa bidii tena huku ukiwa na nidhamu ya hali ya juu kwa kuhakikisha kila ukipatacho unakitunza vyema na kinakusaidia kufanikiwa kwako.
Kama umeamua kujitoa kisawasawa na kufanya kazi kweli na kuachana na maneno, utafanikiwa. Hii ni sheria inayotumiwa na watu karibu wote wenye mafanikio makubwa duniani. Siku zote watu hao ni wa kufanya kazi kwa bidii kubwa hali inayopelekea kuleta mafanikio yao ya uhakika na kujenga utajiri.
3. Tengeneza vyanzo vingi vya fedha.
Hakuna utajiri unaojengwa kwa kutegemea chanzo kimoja cha pesa, utajiri unajengwa kwa kujiwekea vyanzo vingi vya pesa. Kama una chanzo kimoja cha pesa na una nia ya kuwa tajiri hauataweza kuwa hivyo. Siri au sheria ya kuwa tajiri inakutaka wewe kutengeneza vyanzo vingi vya pesa.
Vyanzo hivyo vya pesa vitaingiza pesa bila kujali sana wewe unafanya kazi moja kwa moja au haufanyi. Matajiri wengi ndivyo wanavyotengeneza utajiri wao na hii ni siri mojawapo ambayo unatakiwa uijue kwa ufasaha. Huhitaji sasa kusita sita , weka vyanzo vingi vya pesa utengeneze utajiri wako.
4. Tambua namna ya kutunza pesa zako.
Itakuwa ni kazi bure kama unatafuta pesa,  hujui namna ya kuzitunza vizuri. Kuna watu ambao tatizo sio namna ya kupata pesa, bali ni jinsi ya kuzitunza pesa hizo. Utakuta mtu anapata pesa kweli, lakini matumizi yake yapo juu sana, hicho ni kitu ambacho ni sumu au kiziuzi cha mafanikio yake moja kwa moja.
Inabidi ufike mahali uwe na nidhamu ya hali ya juu, juu ya pesa zako, achana na matumizi ya hovyo, hayawezi kukufikisha popote. Kila wakati kaa chini na elewa namna ya kujifunza juu ya kutumia pesa zako kwa busara. Pesa zako zisije zikakufanya ukawa kama mwendawazimu, tulia ili ujenge utajiri wako.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

Na.Mi&u



Read More
      edit
Published 7/16/2017 10:56:00 AM by with 0 comment

TANZIA: WAZIRI MWAKYEMBE APATA MSIBA MZITO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amepatwa na msiba mzito wa kufiwa na mkewe, Linah George Mwakyembe Jumamosi hii. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa inasema marehemu alilazwa katika hospitali ya Aga Khan ambapo alikuwa akipatiwa matibabu mpaka kifo kilipomfika.

 soma habari zaidi

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

Na.Mi&u

CHANZO: BONGO5
Read More
      edit

Saturday, July 15, 2017

Published 7/15/2017 07:48:00 PM by with 0 comment

SABABU ZA WAPENZI WENGI KUCHEPUKA



MPENZI msomaji wangu, kasi ya kusalitiana kwa wapenzi imekuwa ikiongezeka kila kukicha kiasi kwamba unapoingia katika uhusiano wa kimapenzi unahisi kama unaingia kwenye matatizo makubwa na hii ni kwa sababu watu siyo waaminifu kabisa kwa wapenzi wao. Unaweza kuwa na mpenzi wako ambaye kila mnapoonana anakueleza kuwa, hawezi kukusaliti na atakuwa na wewe katika shida na raha.

Lakini huyohuyo usishangae siku moja ukamkuta yuko na mtu mwingine. Swali la kujiuliza ni kwamba, kwa nini wapenzi wanachepuka? Hicho ndicho nilichopanga kukizungumzia leo. Yaani nitaainisha baadhi ya mambo ambayo kwa uchunguzi wangu nimebaini ndiyo yanayochangia walio wengi kuchepuka, wawe wako kwenye ndoa au uhusiano wa kawaida.
TAMAA ZA KIMWILI NA PESA
Tamaa hasa ya pesa imekuwa ikiwashawishi watu kushindwa kujizuia kuwasaliti wapenzi wao. Kwa wale ambao wako kwenye ndoa wakati mwingine hasa wanawake wasipopatiwa mahitaji yao muhimu na akatokea jamaa na kumhakikishia kwamba atampatia kila anachotaka, wanakubali mara moja bila kujua kwamba wao ni wake za watu ama wapenzi wa watu na kujikuta wanajenga mazoea. Wengine wanapatiwa kila kitu na waume zao lakini sasa kinachotokea ni tamaa za kimwili tu ambazo zinawasumbua na kujikuta wanatafuta wanaume wengine huku wakidai kuwa wanatafuta ladha tofauti. Hili si kwa wanawake tu hata wanaume pia, unaweza kumkuta ana mwanamke bomba tu mwenye kila kigezo, lakini bado anakuwa
na tamaa za kutafuta kimwana mwingine nje.

TABIA ZISIZORIDHISHA Wapo ambao wanaishi maisha ya ajabu sana, yaani wanaishi katika ndoa ama ndani ya uhusiano wakielekea kwenye kuoana lakini hawaaminiani kabisa, kila mtu anakuwa na wasiwasi juu ya mwenzake. Afadhali sasa iwe kutokuaminiana tu lakini wapenzi wanakuwa hawasalitiani. Kuna wale ambao ni wazi hawatulii katika mahusiano yao, yaani matendo yao tu yanaonesha dhahiri kwamba, uaminifu ni sifuri. Kuwa karibu sana na watu wa jinsia tofauti na kuwa na mawasiliano nao ya siri au mwanamke anapomuwekea mumewe vikwazo katika tendo la ndoa anatarajia akafanye na nani kama siyo kumwambia akatafute wengine nje? Ndiyo maana wanaowanyima unyumba waume zao hata wanaposikia kwamba wanasalitiwa wanakuwa hawana nguvu ya kuwashutumu wapenzi wao, utamshutumuje wakati wewe humtimizii katika mambo flani? Si hivyo tu, kwa wanaume nao wengine wamekuwa wakiwasusa wake zao na kukaa siku mbili ama zaidi bila kuonekana nyumbani ama kama atarudi basi usiku wa manane akiwa amelewa na hana mpango kabisa na mke wake. Katika mazingira hayo unadhani nini kinaweza kutokea kama siyo mwanamke kutafuta mwanaume atakayempatia mapenzi?

KUWEPO KWA MAPENZI YA KILAGHAI
Tunapozungumzia mapenzi tunaweza kuyagawanya katika makundi mawili, mapenzi ya kweli na mapenzi ya uongo. Walio katika mapenzi ya kweli huwezi kuwasikia wamesalitiana. Ila wale walio katika mapenzi ya kudanganyana kusalitiana ni kitu cha kawaida kwao hivyo kujikuta kila siku wakifumaniana.

UDHAIFU KWA WAPENZI Udhaifu ambao umezungumziwa hapa ni wa kimaumbile ambao hata hivyo wataalam wa masuala ya mapenzi wanaeleza kwamba, haiwezi kuchukuliwa kama sababu ya kumsaliti mpenzi wako uliyempenda kwa dhati. Kwa mfano, mwanaume unakuwa ‘Functionless’ yaani jogoo hawiki (tatizo ambalo si la kujitakia) na mke wake hayuko tayari kuendelea kuwa naye hivyo kulazimika kuomba talaka. Lakini mwanaume anakuwa mgumu wa kutoa talaka kutokana na jinsi anavyompenda.

Wengi wao wanachokifanya ni kuendelea kuwa katika ndoa huku wakiangalia uwezekano wa kuwa na uhusiano na mtu mwingine wa nje. Kwa wanawake nao yawezekana mwanamke hazai (tatizo ambalo si la kujitakia pia) na mwanaume anahitaji mtoto, atakachokifanya ni kutoka nje kwa siri lakini pia inaweza kufikia hatua mwanamke akagundua. Kwa kifupi ni kwamba kusalitiana kwa wanandoa kumekuwa kukitokea kutokana na kuwepo kwa mazingira fulani ambayo baadhi yao wamekuwa wakishindwa kujizuia nayo na hivyo kujikuta wanatoka nje ya mahusiano.


Ila sasa nalazimika kwa nguvu zote kuwashauri wale walio katika uhusiano wa kimapenzi, namaanisha wapenzi wa kawaida, wachumba ama wanandoa, tusiwe na tamaa za kijinga na kufikia hatua ya kuwasaliti wapenzi wetu. Hivi unajisikiaje unapomvulia nguo mtu ambaye wala hana ‘future’ na wewe? Hivi na wewe ukifanyiwa hivyo na mpenzi wako utajisikiaje? Elewa maumivu utakayoyapata pale utakaposikia mpenzi wako ana uhusiano na fulani ni hayohayo atakayoyasikia mwenza wako. Kuwa muaminifu, ridhika na unachokipata kwake, muoneshe mapenzi ya dhati naye atafanya hivyohivyo na kujikuta mnayafurahia maisha yenu.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

Na.Mi&u
Read More
      edit

Friday, July 14, 2017

Published 7/14/2017 04:49:00 PM by

AY AMVISHA PETE YA UCHUMBA MPENZI WAKE WA SIKU NYINGI




Rapper Ambwene Yessayah maarufu kama AY ameonyesha kuwa amechoshwa na ukapela.

 Msanii huyo Alhamisi hii ameamua kumvisha pete mchumba wake wa muda mrefu Remy, raia wa Rwanda ambaye ajabu amekuwa naye tangia mwaka 2008.

 Kwa mara yakwanza AY amemtambulisha mpenzi wake huyo Disemba mwaka jana wakati wa birthday ya mrembo huyo.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu wa karibu wa wawili hao. Kwa kitendo hicho tunatarajia kuiona ndoa ya Ay na mpenzi wake huyo siku sio nyingi.


Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.Mi&u

chanzo: bongo 5
Read More
      edit

Wednesday, July 12, 2017

Published 7/12/2017 09:14:00 PM by

RAHA JIPE MWENYEWE YAKUPEWA INA GHARAMA

Bila kujali ni magumu gani unayoyapitia lakini hakikisha raha unajipa wewe mwenyewe ukisubiri kupewa basi jua raha hiyo utailipia.

Mi&u@mimi_na_uhusiano
Read More
      edit
Published 7/12/2017 06:01:00 PM by with 0 comment

SAFARI YA MWISHO YA MTANGAZAJI WA REDIO 93.7 EFM, SETH KATENDE MAARUFU BIKIRA WA KISUKUMA


Jeneza lenye mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni, likiwa katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam kunakofanyika misa ya kuaga mwili wake hivi sasa, ambapo baada ya kumalizika kwa misa hiyo, Mwili wa Marehemu utapumzishwa kwenye nyumba yake ya Milele katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam mchana wa leo.

Sehemu ya Waombolezaji wakiwa katika Viwanja Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam kunakofanyika misa ya kuaga mwili wake hivi sasa, ambapo baada ya kumalizika kwa misa hiyo, Mwili wa Marehemu utapumzishwa kwenye nyumba yake ya Milele katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam mchana wa leo.


Read More
      edit

Tuesday, July 11, 2017

Published 7/11/2017 10:56:00 AM by

NIACHE MASOMO ILI NIFANYE BIASHARA


Nina mke na mtoto mmoja. Kwa sasa nimeajiriwa kama mhasibu msaidizi katika kampuni moja hapa Dar es Salaam. Mwaka mmoja baada ya ajira niliamua kujiunga na masomo ya CPA ili kuongeza thamani ya taaluma yangu ya uhasibu. Changamoto yangu kipato hakitoshi masomo magumu na yanachukua muda zaidi kutokana muda mwingi kuwa ofisini. Hivyo nafikiria kuachana na masomo na hiyo fedha ambayo naiwekeza kwenye masomo ya CPA nafikiria niiwekeze kwenye biashara ingawa natamani kuendelea na masomo ya CPA. Naomba ushauri maana naona umri unazidi kwenda (nina miaka 33) niachane na CPA na kutafuta biashara ya kufanya na kuweka juhudi zaidi huko? Ahsnte – 

Pole sana kwa changamoto hiyo unayopitia. Ni wakati mgumu sana uliopo, kama umeajiriwa, una familia, kipato kidogo na kama hayo hayatoshi, una masomo magumu ambayo pia yanakugharimu.
Ni wakati mgumu sana, lakini kabla ya kufanya maamuzi yoyote, lazima ukae chini na kutafakari kwa makini maisha yako na ndoto zako kubwa, yapi maono ya maisha yako, kupanga vipaumbele vyako vizuri na kisha kuweka mkakati ambao utaufanyia kazi, kwa nidhamu ya hali ya juu sana.
Hivyo, kabla hujafanyia kazi ushauri ambao nitakupa hapa, kaa chini kwanza uangalie maisha yako na maono yako. Kisha angalia hatua mbayo utaichukua.
Baada ya hayo, ushauri wangu ninaokupa ni huu; FANYA VYOTE KWA PAMOJA.
Ndiyo, namaanisha ufanye vitu vyote hivyo kwa pamoja. Yaani una familia, umeajiriwa, una masomo na unafikiria kuhusu biashara. Badala ya kutaka kuacha masomo ili ufanye biashara, fanya masomo na fanya biashara. Huenda hukutegemea jibu hili na huenda una wasiwasi haiwezekani, lakini nakuambia inawezekana kama kweli utaamua liwezekane.
Nina amini masomo yako ya CPA hayatachukua zaidi ya miaka mitatu, hivyo basi rafiki, nataka ujitangazie miaka mitatu ya vita. Hii inakwenda kuwa miaka mitatu ya tofauti kabisa kwenye maisha yako, miaka mitatu ya kuyajenga upya maisha yako.
Kwenye miaka hii mitatu, jipe ruhusa kabisa ya kwenda kinyume na maisha yote ya kijamii, kwa sababu jukumu lililopo mbele yako siyo dogo, ni kubwa sana, hivyo linakuhitaji na wewe uwe na maamuzi ambayo wengine hawatakuelewa.
Kwa uzoefu wangu binafsi na kupitia watu ambao nimewashauri, nimekuja kugundua karibu kila mmoja wetu ana uzembe fulani ambao unamrudisha nyuma. Licha kweli ya maisha kuwa magumu, kipato kidogo na kazi kuwa nyingi, bado tuna uzembe ambao tunaufanya, na uzembe huu unaturudisha nyuma.
Kwa mfano, utakuta mtu pamoja na changamoto alizonazo, bado anapata muda wa kuangalia tv, kusoma magazeti, kusikiliza redio. Bado ana muda wa kufuatilia mpira, anakaa kabisa chini dakika 90 kuangalia mpira. Bado ana marafiki anaokutana nao jioni na wanakaa kupiga stori, labda wakipata vinywaji. Mtu huyu huyu yupo kwenye mitandao ya kijamii, analala muda wa zaidi ya masaa sita. Mtu huyo unakuta siku za kazi ni tano, jumatatu mpaka ijumaa, na jumamosi labda nusu siku, halafu jumapili anapumzika. Mtu huyo huyo ana mambo mengi ambayo yanampotezea fedha lakini hakuna hatua anazochukua. Na mambo yanapokwenda hivi, lazima maisha yazidi kuwa magumu.
Hivyo hatua za kuchukua ni hizi;
  1. Badili kabisa mfumo wako wa maisha.
Tenga miaka hiyo mitatu kama nilivyokueleza hapo juu, miaka hiyo hakikisha unaimaliza cpa, unaongeza kipato chako kupitia biashara, na kuimarisha maisha yako.
Weka thamani kubwa sana kwenye muda wako, usipoteze hata dakika yako moja. Punguza watu na mambo mengine yoyote ambayo siyo muhimu kwako. Kama kuna mtu ambaye hatakuelewa kwa mabadiliko ya maisha utakayofanya, siyo muhimu, achana naye. Kaa na wale watu wanaoelewa unakoenda, na wanakuunga mkono na kukusaidia. Achana na watakaokukatisha tamaa, na kwa taarifa tu, watakuwa wengi.
  1. Chagua biashara ambayo utaifanya.
Chagua biashara ambayo unaweza kuifanya, kwa kuanzia hapo ulipo sasa. Na kwa kuwa muda wako ni mdogo, nakushauri uanzishe biashara ya huduma, ambapo utatoa ulichonacho kwa wengine.
Kwa mfano wewe umesema ni mhasibu, sasa angalia unawezaje kutumia uhasibu wako kama huduma na kuiuza kwa wengine.
Je unaweza kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kuandaa mahesabu ya biashara zao?
Je unaweza kupata kazi ya muda wa ziada kazini kwako au sehemu nyingine ambayo unaweza kutoa thamani zaidi?
Je unaweza kutoa huduma ya kuwafundisha watu wengine wanaojifunza uhasibu au kitu kingine ambacho unaweza kufundisha?
Je unaweza kuanzisha biashara nyingine ndogo ukapata mtu wa kuifanya kwa karibu na wewe ukapata muda wa kuifuatilia kila siku?
Endelea kujiuliza maswali hayo, kulingana na mazingira yako mpaka upate jibu lenye kuweza kufanyika. Lazima upate jibu na kuanza kulifanyia kazi mapema.
  1. Panga ratiba ya kila siku ambayo utaisimamia vizuri.
Kitu muhimu sana ambacho unapaswa kufanya, ni kupangilia ratiba yako ya kila siku. Na anza na mpango wa siku ambao una mambo utakayoyafanya kila siku. Kwa mfano kwako wewe, kazi, masomo, biashara na familia ni mambo ambayo lazima uyafanye kila siku.
Hivyo hakikisha kila siku ya kazi, unatenga muda ambao utakuwa wa kufanya kazi.
Katika siku nyingine zote za wiki, panga muda wa kusoma masomo yako, na pia panga muda wa kufanya kazi kwenye biashara yako. Hili ni kila siku, kumbuka kwa sasa huna siku ya mapumziko, utaendesha maisha yako siku saba za wiki, na siku ambayo huendi kazini ndiyo unazitumia vizuri zaidi.
Panga kuamka mapema kuliko ulivyozoea, aka masaa mawili au hata moja kabla ya muda wako wa kawaida wa kuamka. Na muda huo utumie kusoma, kila siku. Unapokuwa kazini, muda wowote unaopata wa mapumziko, usiupoteze, badala yake utumie kusoma. Jioni ukitoka kazini, usipoteze muda, weka muda huo kwenye biashara yako.
Kusoma na biashara vikweke kwenye ratiba yako ya kila siku. Najua watu wengi huwa hawasomi mpaka mitihani ikaribie, wewe usiwe mtu wa aina hii. Kuanzia siku ya kwanza unapojiandikisha na masomo na kupata mtaala, panga ratiba ya kila siku utasoma nini mpaka unapofikia wakati wa mtihani. Kwa njia hii utakuwa na maandalizi mazuri na mambo yako mengine yataenda. Kama ukiweza kujijengea nidhamu, unaweza kuweka muda wako kwenye kujisomea mwenyewe na kuepuka kuhudhuria madarasa ambayo yatakuhitaji kulipa fedha zaidi.
  1. Jenga nidhamu ya hali ya juu sana, mambo hayatakuwa rahisi.
Kusoma hapa itakuwa rahisi, na unaweza ukaona eh, nitafanya hivi. Lakini siku ya kwanza kuanza kufanya tu, dunia yote itakupinga. Utafika wakati wa kuamka na utajiambia kwa nini niamke leo, nitaamka kesho. Utafika kazini na kupewa majukumu zaidi. Utapanga ratiba ya kusoma na kuona mtihani bado upo mbali, utasoma tu.
Dunia inakusubiri ikuangushe, hivyo jiandae vizuri sana, tena sana. Na usikubali kwa namna yoyote ile kuvunja kile ulichopanga. Kwa lolote linalotokea ambalo hukutegemea, jipange kuhakikisha mambo yako yanaenda kama ulivyopanga.

Jambo moja naweza kukuhakikishia ni kwamba, maisha yatakuwa magumu, lakini kwa uhakika zaidi ni kwamba hutakufa, utazidi kuwa imara na maisha yako yatakuwa bora zaidi.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.Mi&u

Read More
      edit
Published 7/11/2017 10:01:00 AM by

MAGAZETI YA LEO JULY 11, 2017






Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

Na.Mi&u

CHANZO: GPL
Read More
      edit

Sunday, July 9, 2017

Published 7/09/2017 01:19:00 PM by

PICHA ZA HARUSI YA PROFESA JAY NA MKEWE GRACE










Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

Na.Mi&u

CHANZO: MILARD AYO
Read More
      edit

Friday, July 7, 2017

Published 7/07/2017 09:41:00 PM by

NAHISI KUJITOA ROHO KISA MKE WANGU AU NIMFANYAJE?




Nina miaka zaidi ya 7 kwenye ndoa ya mke mmoja na watoto watatu ambao wengine ni wakubwa wakiwa ngazi ya sekondari kimasomi.
Kuna wakati ndoa yangu ilikuwa na migogoro ya hapa na pale kwa sana Kiasi kwamba ikafika sehemu mke wangu akatoroka nyumbani kwa kusomba kila kitu wakati mimi nikiwa kwenye mizunguko yangu.


Maisha yaliendelea kwa muda nikiwa pekee yangu lakini baadaye mke wangu alirejea nyumbani. Ila kuna kitu nilikigundua kwake alivyotoroka na alivyorudi kulikuwa na mabadiliko sana, kwanza amekuwa na kibuli na dharau hasa. Nilivumumilia.


Kuna wakati maisha yaliyumba sana kwa upande wangu kwa sababu niliacha kazi niliyokuwa nayo. Kwa kuwa watu mtaani walikuwa wanajua kazi ambazo ninazifanya, mmoja wa jirani yetu akaniambia anipe kazi ya ulinzi kwake, ila bahati nzuri nikawa nimepata kazi kwingine.


Yule mwanaume, mkewe na mke wangu ni marafiki walioshibana sana. Baada ya kuona maisha yetu hayako sawa, yule mama aliongea na mke wangu ili twende tukaishi kwenye nyumba yao iliyoko shamba, tukakubali.
Baada ya muda kupita nikagundua kuwa yule baba mwenye nyumba ninayoishia anatembea na mke wangu. Kumbe siku zote migogoro na mifarakano na mke wangu yeye ndiye hasa aliyekuwa anahusika.


Nimeumia sana, natamani hata nijichome kisu kwa hasira nilizonazo, kumbe jamaa alinipa msaada ili atembee na mke wangu, inaniuma sana. Natamani nichukue maamuzi magumu lakini watoto wangu wananiuma na ninawapenda sana.
Naomba ushauri wako wa mwisho ili nijue nini chakufanya.


Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.Mi&u


Read More
      edit