Nina miaka zaidi ya 7 kwenye ndoa ya mke mmoja na
watoto watatu ambao wengine ni wakubwa wakiwa ngazi ya sekondari kimasomi.
Kuna wakati ndoa yangu ilikuwa na migogoro ya hapa na
pale kwa sana Kiasi kwamba ikafika sehemu mke wangu akatoroka nyumbani kwa
kusomba kila kitu wakati mimi nikiwa kwenye mizunguko yangu.
Maisha yaliendelea kwa muda nikiwa pekee yangu lakini
baadaye mke wangu alirejea nyumbani. Ila kuna kitu nilikigundua kwake alivyotoroka
na alivyorudi kulikuwa na mabadiliko sana, kwanza amekuwa na kibuli na dharau hasa.
Nilivumumilia.
Kuna wakati maisha yaliyumba sana kwa upande wangu kwa
sababu niliacha kazi niliyokuwa nayo. Kwa kuwa watu mtaani walikuwa wanajua
kazi ambazo ninazifanya, mmoja wa jirani yetu akaniambia anipe kazi ya ulinzi
kwake, ila bahati nzuri nikawa nimepata kazi kwingine.
Yule mwanaume, mkewe na mke wangu ni marafiki
walioshibana sana. Baada ya kuona maisha yetu hayako sawa, yule mama aliongea
na mke wangu ili twende tukaishi kwenye nyumba yao iliyoko shamba, tukakubali.
Baada ya muda kupita nikagundua kuwa yule baba mwenye
nyumba ninayoishia anatembea na mke wangu. Kumbe siku zote migogoro na
mifarakano na mke wangu yeye ndiye hasa aliyekuwa anahusika.
Nimeumia sana, natamani hata nijichome kisu kwa hasira
nilizonazo, kumbe jamaa alinipa msaada ili atembee na mke wangu, inaniuma sana.
Natamani nichukue maamuzi magumu lakini watoto wangu wananiuma na ninawapenda
sana.
Naomba ushauri wako wa mwisho ili nijue nini
chakufanya.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa
ku-Bonyeza Hapa
Na.Mi&u